Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Unataka KUFAULU MITIHANI Kwa KIWANGO cha Juu?…
i. Tafuta mtu wa kumfundisha
iii. Tumia ramani na michoro
iv. Kitabu cha kumbukumbu/ubao wa kumbukumbu
v. Tumia kadi
vi. Pumzisha akili yako
Katika Makala Hii Tutazungumzia Mkakati Wa Kwanza
– Tafuta Mtu Wa Kumfundisha
Unapomfundisha mwingine ambacho umeelewa, ni njia ya kujifundisha mwenyewe mara ya pili.
Kumfundisha mwenzio sio kupoteza muda lakini ni kuwekeza katika ubora wako.
Ukiwa unamfundisha mwenzako utakuja kugundua kuwa kuna maeneo ambayo yalikuwa ni magumu kwako kukumbuka.
Na hivyo unausaidia ubongo wako uweze kutunza kumbukumbu ya kudumu kutokana na nguvu ya kurudia.
Njia nzuri ya kujua kuwa uko vizuri katika somo fulani tafuta mtu ambaye anahitaji kufudishwa na tengeneza muda wa utulivu wa kumfundisha.
Katika kufundisha utakugundua vitu vingi sana ambavyo vitakusaidia katika maandalizi yako ya mitihani.
Jaribu kuangalia wanafunzi wanaofanya vizuri utagundua kuwa wapo tayari kufundisha wengine.
Na kadri wanavyofundisha wengine ndivyo wanavyoongeza kupata ufaulu mzuri.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.