Ibada ya Kweli!!!

Ibada maana yake ni kuonesha, upendo, unyenyekevu, utiifu, kujitoa kwa moyo wote na heshima kwa Mungu au miungu.

Ibada uambatana na utoaji wa sadaka, nyimbo za kumtukuza au kunyenyekea mbele ya Mungu anayeabudiwa.

Israeli in taifa pekee ulimwenguni ambalo lilimuabudu Mungu wa kweli, kwa miaka mingi kabla ya kuiga mataifa mengine na kuanza kuabudu miungu mingine na masanamu.

Hapo ndipo Mungu aliwakataa, akazikataa sadaka zao, na nyimbo zao. Akaikataa ibada yao kwa ujumla.

📖Amosi 5:21 Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini.
Amosi 5:22 Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.
Amosi 5:23 Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu.

👉Bwana Yesu alipokuja akatangaza ujio wa ibada ya rohoni.
*
✍ KWA NINI IBADA YA ROHONI*

Hapo mwanzo Bwana (maana wa Mungu) yeye aliyekuwa na mwili ndiye aliyepokea sadaka, akapigiwa magoti na kusujudiwa.

📖 Mithali 8:24 Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa, Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji.
Mithali 8:30 Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku; Nikifurahi daima mbele zake;
Mithali 8:31 Nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu; Na furaha yangu ilikuwa pamoja na wanadamu.

📖Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Yohana 1:2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
Yohana 1:3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

👉Lakini sasa huyu mwenye mwili aliyependa kusujudiwa, kuimbiwa, kupewa sadaka amepumzika, Baba yake amemwambia apumzike ili yeye awakusanye wale watu wabaya ambao majina yao hayamo katika kitabu cha uzima. Watu wapendao uongo moyoni mwao.

📖Zaburi 110:1 Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.

👉Sasa huyu Baba ni Roho, hataki sadaka, wala nyimbo zenu isipokuwa wimbo mmoja. Wimbo wa Mwanakondoo, (Pasaka) maana wa Musa ulishaimbwa na waliotutangulia.

📖Ufunuo wa Yohana 15:3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.

👉Sadaka aipendayo ni ya kuwasaidia wasionacho (matendo ya Rehema)

📖Mathayo 25:34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
Mathayo 25:35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
Mathayo 25:36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
Mathayo 25:37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
Mathayo 25:38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
Mathayo 25:39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
Mathayo 25:40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
Mathayo 25:41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Mathayo 25:42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
Mathayo 25:43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
Mathayo 25:44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
Mathayo 25:45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
Mathayo 25:46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

👉IBADA YETU SASA SI KWA BWANA BALI NI KWA BABA MUNGU, baba yake Bwana.

📖Mathayo 6:6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Mathayo 6:9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,

BASI TUABUDU MIOYONI MWETU HATA JIRANI YAKO ASIJUE UNASALI SAA NGAPI BALI MATENDO YAKO YA ADILI YAWE NDIO NURU KWA WENGINE KUTHIBITISHA IMANI YAKO KWA MUNGU WA KWELI.

1 Lisikieni neno hili nilitamkalo liwe maombolezo juu yenu, enyi nyumba ya Israeli.2 Bikira wa Israeli ameanguka;hatainuka tena;Ameangushwa katika nchi yake;hakuna mtu wa kumwinua.3 Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu, utasaziwa watu mia, na mji uliotoka wenye watu mia, utasaziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli.4 Maana BWANA awaambia hivi nyumba ya Israeli, Nitafuteni mimi, nanyi mtaishi;5 bali msitafute Betheli, wala msiingie Gilgali, wala msipite kwenda Beer-sheba; kwani Gilgali hakika yake itakwenda utumwani, na Betheli itakuwa ubatili.6 Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli.7 Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini,8 mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake;9 yeye aletaye uharibifu wa ghafula juu yao walio hodari, hata uharibifu uipate ngome.10 Wao humchukia yeye akemeaye langoni, nao humzira anenaye maneno ya adili.11 Basi, kwa kuwa mnamkanyaga maskini, na kumtoza ngano; ninyi mmejenga nyumba za mawe yaliyochongwa, lakini hamtakaa ndani yake; ninyi mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu, lakini hamtakunywa divai yake.12 Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.13 Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.14 Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo BWANA, Mungu wa majeshi, atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo.15 Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba BWANA, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.16 Kwa ajili ya hayo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maombolezo katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza.17 Tena katika mashamba yote ya mizabibu kutakuwako kulia; kwa maana mimi nitapita katikati yako, asema BWANA.Siku ya BWANA; Siku ya Giza18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya BWANA; kwani kuitamani siku ya BWANA? Ni giza, wala si nuru.19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.20 Je! Siku ya BWANA haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.21 Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini.22 Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.23 Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu.24 Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama maji makuu.25 Je! Mliniletea dhabihu na sadaka jangwani muda wa miaka arobaini, enyi nyumba ya Israeli?26 Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyizia wenyewe.27 Kwa sababu hiyo nitawahamisha, hali ya kufungwa, mwende mbali kupita Dameski, asema BWANA, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment