Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Sudani, dhuluma za Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kinachoongozwa na Jenerali Mohamad Hamdane Daglo, anayejulikana kama Hemedti, zinaendelea kwa siku ya kumi mfululizo katika jimbo la Al-Jazirah, katikati mwa nchi hiyo. Mwanamume mmoja anashuhudia mambo ya kutisha aliyoyapata, baada ya kuasi kwa kiongozi wa kijeshi kutoka eneo hili kutoka RSF.

Tangu Abu Akla Kikel, kiongozi wa kijeshi kutoka Jimbo la Al-Jazirah la mashariki kutoroka Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), ambaye alijiunga na jeshi la Sudani la Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, dhuluma katika eneo hilo imeathiri miji na vijiji kadhaa, na raia wanalengwa kwa makusudi.
Siku ya Jumanne, Oktoba 29, watu kadhaa waliuawa katika kijiji cha al-Hilaliya. Kulingana na mashirika yasiyo ya kiraia ya ndani, idadi ya waathiriwa waliouawa katika siku kumi zilizopita mashariki mwa Al-Jazirah ni zaidi ya watu 400.
Wanamgamo hao wanaua, wanapora na kuwalazimisha wakaazi kukimbia. Chama cha Madaktari wa Sudani kimesema kwamba RSF iliua watu wanne na kushambulia timu ya madaktari siku ya Jumanne, kabla ya kupora hospitali ya Wad al-Fadl, mji ulioko mashariki mwa Al-Jazirah.
“RSF inatishia wale wote wanaokataa kuondoka”
“Tangu kuasi kwa Abou Akla Kikel, RSF imeanzisha kampeni ya kulipiza kisasi, na mauaji ya kikatili. Walianza kutoka mji wa Rofaa na kuelekea Tamboul. Vijiji vyote vilivyo katika eneo hilo vimekuwa na mauaji ya kikatili, ubakaji na uporaji, na kusababisha watu kulazimika kuyahama makazi yao,” anashuhudia mtu mmoja ambaye bado jina lake halijafahamika kwa sababu za kiusalama, akizungumza na Houda Ibrahim. Alikuwa ametoroka Al-Fasher na alilazimika kutoroka tena. Alipoteza watu ishirini wa familia yake.
“RSF inatishia yeyote anayekataa kuondoka. Wakati mwingine wanamgambo hawa hwanaua watoto. Hivi sasa, vijiji vingi vya mashariki mwa Al-Jazirah viko tupu. Wakazi hao walikimbia, na kuacha kila kitu walichokuwa nacho. Hakuna huduma za matibabu tena, hakuna maji ya kunywa tena. RSF iliiba paneli za jua ambazo zilikuwa zikisaidia vituo vya maji, “anasema.
“Hali ni ya kusikitisha na ulimwengu hauchukui hatua. Hakuna anayezungumza kuhusu kile kinachotokea Tamboul, huku RSF ikiendelea kutekeleza shughuli hizi za kulipiza kisasi,” anahitimisha shahidi huyu.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.