Faida 5 Za Maumivu-Unataka Kupona MAUMIVU ya MOYO?…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Yanakupa Ujasiri wa Kufanya Maamuzi

ii. Yanakusaidia kuwajua watu sahihi.

iii. Yanakusaidia kujua udhaifu wako

iv. Yanakupa mwelekeo mpya wa maisha.

v. Inaweza kuwa chanzo cha hamasa ya kufanya jambo.

Katika Makala Hii Tutazungumzia Faida Ya Nne.

– Yanakupa mwelekeo mpya wa maisha.

Maumivu mengi ambayo tunakutana nayo, huwa yanatusaidia kutafakari juu ya mwelekeo wa maisha yetu.

Kuna watu ambao walibadili kabisa mwelekeo wa maisha yao ya kimahusiano, baada ya kukutana na aina fulani ya maumivu.

Yani, waliamua kuachana na mahusiano waliyokuwa nayo au walifanya maamuzi juu ya mahusiano mapya.

Kitu cha ajabu ni kuwa kuna watu ambao baada ya kuchukua maamuzi hayo, hapo baadaye walifurahia kwa sababu waligundua walikuwa wanakosa kitu kikubwa sana kwenye maisha yao.

Yani waligundua kuwa, maamuzi waliyoyachukua yaliwapa furaha zaidi, amani zaidi na mafanikio ya haraka kuliko mambo waliyokuwa wanafanya hapo mwanzoni.

Tafakari vizuri, inawezekana maumivu unayoyapitia hapo ofisini kwako, kwenye mahusiano, kwenye biashara n.k…

…kazi yake kubwa ni kukusaidia kupata mwelekeo mpya au kufungua ukurasa mpya wa maisha yako.

Kama unataka kujifunza Mbinu Za Kupona MAUMIVU ya MOYO..

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment