Ziara ya Macron Morocco: Makubaliano ya hadi euro bilioni 10

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kiasi kilichotangazwa na Élysée kimekaribishwa nchini Morocco: mikataba na uwekrzaji vilivyotiwa saini wakati wa ziara hiyo vinapaswa kwenda “hadi euro bilioni kumi”, kulingana na Ikulu ya Elysée. Miongoni mwa makubaliano muhimu zaidi yaliyotangazwa siku ya Jumatatu jioni, ambayo yanahusu kampuni za Alstom na Egis kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya pili ya njia ya treni ya mwendo kasi ambayo inapaswa kuunganisha Tangier hadi Marrakech.

Mfalme wa Morocco Mohammed wa 6, kulia, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakisalimiana na umati wa watu wakati wa ziara rasmi ya rais wa Ufaransa nchini Morocco, katika mji mkuu wa Rabat, Jumatatu, Oktoba 28, 2024.
Mfalme wa Morocco Mohammed wa 6, kulia, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakisalimiana na umati wa watu wakati wa ziara rasmi ya rais wa Ufaransa nchini Morocco, katika mji mkuu wa Rabat, Jumatatu, Oktoba 28, 2024. AP – Mosa’ab Elshamy

Sekta nyingine ya kimkakati, hidrojeni ya kijani, makubaliano na TotalEnergies yatafikia euro bilioni 2 ili kuendeleza eneo hili. Nishati mbadala, jua, pia zinatambuliwa kama sekta inayoahidi ya ushirikiano kati ya Ufaransa na Morocco.

Nchi hizi pia zimetia saisi kweye mkataba uliofikiwa na kampuni ya Ufaransa ya Safran kwa ajili ya kuanzisha eneo la matengenezo na ukarabati wa injini ya ndege huko Casablanca. Uwekezaji wa euro milioni 130 katika mji mkuu wa kiuchumi ambao umekuwa kitovu cha usafiri wa anga katika miaka ya hivi karibuni. Hatimaye, shirika la usafiri wa baharini CGM-CMA litaungana na Marsa Maroc kuandaa na kuendesha nusu ya kituo cha kontena cha Nador West Med kaskazini mwa Morocco kwa miaka 25. Hata hivyo, wataalamu wanatuhimiza tuwe waangalifu kuhusiana na matangazo haya, ambayo yanasalia kwa sehemu kubwa ya matamko ya nia, anasema mwandishi wetu wa Rabat, François Hume-Ferkatadji.

Wale walio karibu na rais wa Ufaransa wanaelezea ziara hii kama “kiongeza kasi cha chembe”, njia ya kusema kwamba inaruhusu baadhi ya mazungumzo kusonga mbele kwa haraka zaidi au “kuona nini kinaweza kuzuia baadhi ya masuala”.

Baada ya muda wa miaka mitatu wa mafarakano, mjumbe wa wajumbe wa Ufaransa anataka kuamini kwamba huu ni “mwisho mafarakano” kati ya Ufaransa na Morocco. Emmanuel Macron na Mohammed VI kwa namna fulani wamefahamisha hili kwa kutia saini pamoja tamko la “ushirikiano wa kipekee ulioimarishwa”. Na zaidi ya yote, walikubaliana juu ya ziara ya serikali ya Mohammed VI kwenda Ufaransa mnamo 2025.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment