Canada: Ruksa kwa wakazi wa Quebec wanaougua sana kuamua juu ya mwisho wa uhai wao

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Tangu mwaka wa 2014, sheria ya Quebec tayari imetoa usaidizi wa kufariki kwa ajili ya watu ambao wanataka kufariki mapema. Siku ya Jumatano, Oktoba 30, watu wa Quebec ambao wamepokea utambuzi wa ugonjwa mbaya na usiotibika unaosababisha mtu kutofanya kazi yoyote sasa wanaweza pia kuwasilisha ombi la mapema la usaidizi wa kimatibabu kwa kumaliza uhai wao.

Picha ya jiji la Montreal, Quebec.
Picha ya jiji la Montreal, Quebec. Getty Images – Eduardo Fonseca Arraes

Sandra Demonigny anazingatia ombi lake analotarajia la usaidizi wa kimatibabu kwa kumaliza uhai wake. Mtu huyu wa miaka arobaini aligunduliwa na ugonjwa wa Alzeima ulioanza mapema, kama babake kabla yake. Anataka kufariki mapema.

“Sitaki kuwa tegemezi kwa sababu kuna mtu ambaye yuko namo kila wakati. Kwangu, sioni thamani yoyote kwa maisha yangu, haswa nikijua kuwa hali itazidi kuzorota,” anasema.

Hatari ya kosa la jinai kwa wauguzi?

Wakazi wa Quebec ambao wangependa kunufaika na ombi hili la mapema waliweka vigezo vinavyolingana na matakwa yao ya mwisho wa uhai wao. Hata hivyo, sheria ya Quebec haikupata kibali kutoka kwa serikali ya Canada. Hii inasumbua madaktari na wauguzi wengi, kwa sababu kwa nadharia, wanaweza kushtakiwa kwa mauaji.

Katika mojawapo ya hospitali za Quebec, Alain Naud hufanya kazi ya usaidizi wa kitiba kwa kutoa uhai wa mtu anayetaka kufariki mapema: “Hofu yangu ni kwamba kuna kundi la wanadini, ambao wanaamua kukusanyika kufuatilia madaktari ambao watahusika na kitendo hiki. Kwa upande wa madaktari, lazima tuwe na hakikisho kwamba tutatetewa au kulindwa ikiwa hii itatokea. “

Kukosekana kwa mashauriano na serikali kuu kunaweza kupunguza idadi ya madaktari wanaotekeleza  ombi la mapema la kumsaidi mtu kufariki.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment