Waziri wa ulinzi wa Israel asema uteuzi wa kiongozi mpya wa Hezbollah ni wa muda mfupi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amerusha kwenye kurasa wake wa X picha ya Naïm Qasim, katibu mkuu mpya aliyechaguliwa wa Hezbollah, ikiambatana na ujumbe: “Uteuzi wa muda. Hatadumu kwa muda mrefu. “

Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant anatoa taarifa kwa waandishi wa habari katika makao makuu ya Israel Aerospace Industries (IAI) karibu na uwanja wa ndege wa Ben Gurion.
Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant anatoa taarifa kwa waandishi wa habari katika makao makuu ya Israel Aerospace Industries (IAI) karibu na uwanja wa ndege wa Ben Gurion. © AFP / GIL COHEN-MAGEN

Kiongozi wa awali wa HezbollahHassan Nasrallah, na yule aliyetarajiwa kumrithi, Hachem Safieddine, wote waliuawa na Israel.

Wakati huo huo jeshi la Israel limetangaza vifo vya wanajeshi wake wanne waliouawa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na hivyo kufikisha idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa katika ardhi ya Palestina kufikia 367 tangu kuanza kwa operesheni yake ya ardhini tarehe 27 Oktoba 2023.

Wizara ya Afya ya Hamas yatangaza idadi mpya ya vifo vya watu 43,061

Wizara ya Afya ya serikali ya Hamas huko Gaza imetangaza siku ya Jumanne idadi mpya ya vifo vya watu 43,061 waliouawa katika ardhi ya Palestina tangu kuanza kwa vita na Israel zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Takriban watu 41 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita, imesema katika taarifa yake, na kuongeza kuwa watu 101,223 wamejeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita, vilivyosababishwa na shambulio ambalo halijawahi kutokea dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7, 2023.

Watu 93 wauawa katika shambulio la Israel dhidi ya jengo la makazi huko Beit Lahia

Ulinzi wa Raia huko Gaza umetoa idadi mpya ya watu 93 waliouawa usiku wa manane katika shambulio la usiku la Israeli kwenye jengo la makazi huko Beit Lahia, kaskazini mwa ardhi ya Palestina. “Idadi ya mashahidi kutokana na mauaji ya makazi ya familia ya Abounasr huko Beit Lahia inafikia 93, na karibu watu 40 bado hawajulikani walipo chini ya vifusi,” amesema Mahmoud Bassal, msemaji wa Ulinzi wa Raia.

Wafanyakazi wa idara ya uokoaji wakiondoa mwili kutoka kwenye vifusi vya jengo lililokumbwa na shambulio la Israel huko Beit Lahia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 29, 2024.
Wafanyakazi wa idara ya uokoaji wakiondoa mwili kutoka kwenye vifusi vya jengo lililokumbwa na shambulio la Israel huko Beit Lahia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 29, 2024. AFP – –

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment