Kenya: Seneta mmoja apendekeza kuongeza muda wa kuhudumu kwa maafisa waliochaguliwa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muda wa mihula ya viongozi waliochaguliwa, ikiwa ni pamoja na ule wa rais, unajalidiliwa nchini Kenya. Seneta mmoja amewasilisha pendekezo la kufanyia marekebisho katiba na kuongeza muda wa muhula wa rais na ule wa wabunge kutoka miaka 5 hadi 7. Pendekezo ambalo limesababisha mgawanyiko ndani ya kambi ya rais na ambalo haliungwi mkono na Wakenya wote.

Mtazamo wa jumla wa Bunge la Kenya mjini Nairobi, Machi 26, 2015.
Mtazamo wa jumla wa Bunge la Kenya mjini Nairobi, Machi 26, 2015. SIMON MAINA / AFP

Nchini Kenya, rais anahudumu kwa mihula miwili ya miaka mitano. Seneta aliyetoa pendekezo hilo anazingatia muda huu kuwa mfupi sana kumruhusu mkuu wa nchi kutekeleza mpango wake. Kulingana na seneta huyo, kuongeza muhula wa uongozi wa rais na wabunge hadi miaka saba pia kungepunguza gharama zinazohusiana na uchaguzi.

Pendekezo limesababisha mgawanyiko hata ndani ya kambi ya rais. Chama cha William Ruto, anachotoka Seneta Samson Cherargei, kimegawanyika kufutia pendekezo hilo. Katibu mkuu wake ameuchukulia mswada huo kama “maudhi na limepitwa na wakati”, na kuutaja kuwa “unakiuka maadili ya kikatiba” ya nchi. Kiongozi wa walio wengi katika Bunge la taifa pia amepinga pendekezo hilo, Kama wanachama kadhaa wa upinzani. Baadhi wanabaini kwamba suala hilo liko mbali na vipaumbele vya nchi na kwamba miaka mitano ya sasa inatosha. Wengine wanahofia kwamba marekebisho hayo ya katiba yatakuwa chanzo cha kukosekana kwa utulivu wa kisiasa.

Mada kwa hali yoyote husababisha majibu kwa maoni ya umma. Wakenya walikuwa na mwezi mmoja kuwasilisha maoni yao kwa Bunge la Seneti. Benge la Seneti la Kenya mlilipokea majibu zaidi ya 240,000. Sanduku la barua rasmi lilijaa na anwani ya pili ilibidi iwasilishwe. Kamati ya Bunge la Seneti sasa itachunguza majibu yaliyopokelewa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment