Hatua ya Israeli kupiga marufuku shirika la UNRWA yashutumiwa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hatua ya bunge la Israel kupitisha sheria mpya inayopiga marufuku shughuli zote za Tume ya Umoja wa Mataifa katika nchi yake, kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, imezua shutuma mbalimbali duniani.

UNRWA imekuwa ikitoa msaada wa wakimbizi wa Palestine.
UNRWA imekuwa ikitoa msaada wa wakimbizi wa Palestine. © Mohammed Salem / Reuters

Licha ya onyo kutoka kwa Marekani ambaye ni mshirika wa karibu wa Israeli na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wabunge wa Israeli kwa wingi wamepitisha sheria hiyo tata, kupinga marufuku Tume hiyo ya UNRWA nchini Israeli na Mashariki mwa Jerusalem.

Tume hiyo imekuwa ikitoa misaada ya kibinadamu kama huduma za afya, elimu na misaada nyingine kwa wakimbizi wa Kipalestina kwa miongo zaidi ya saba.

Israeli inasema hatua ya kupitishwa kwa sheria hiyo ni kutokana na madai ya ushirikiano wa karibu kati ya kundi la kigaidi la Hamas na Tume hiyo, na hivyo haiwezi kuruhusu iendelee na shughuli zake.

Israeli imekuwa ikiituhumu UNRWA kwa kuhusika na vitendo vya kigaidi katika Ukanda wa Gaza pamoja na kuwaunga mkono wapiganaji wa Hamas.
Israeli imekuwa ikiituhumu UNRWA kwa kuhusika na vitendo vya kigaidi katika Ukanda wa Gaza pamoja na kuwaunga mkono wapiganaji wa Hamas. © Amr Abdallah Dalsh / Reuters

Kundi la Hamas limelaani hatua hiyo ya Israeli na kuelezea kama kitendo kingine cha uvamizi dhidi ya Palestina huku mataifa ya Magharibi kama Uingereza na Ujeurumani yakionya kuwa, kupitishwa kwa sheria hiyo kutawanyima mamilioni ya Wapalestina kupata mahitaji muhimu.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema Israeli itaendelea kutoa ushirikiano wa utoaji misaada ya kibinadamu kwenye ukanda wa Gaza, bila kutishia usalama wa nchi yake.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment