DRC: Kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila yapinga mradi wa kufanyia Katiba marekebisho

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muungano wa Common Front for Congo (FCC) wa Joseph Kabila, rais wa zamani wa DRC kinapinga dhidi ya rasimu ya marekebisho ya Katiba iliyowasilishwa na Rais Félix Tshisekedi wiki iliyopita. 

Rais wa Kongo Félix Tshisekedi (kushoto) na mtangulizi wake Joseph Kabila (kulia) walikuwa washirika mwanzoni mwa muhula wa rais Tshisekedi. Hapa, ilikuwa Januari 24, 2019 jijini Kinshasa.
Rais wa Kongo Félix Tshisekedi (kushoto) na mtangulizi wake Joseph Kabila (kulia) walikuwa washirika mwanzoni mwa muhula wa rais Tshisekedi. Hapa, ilikuwa Januari 24, 2019 jijini Kinshasa. © Jerome Delay / AP

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni ya Jumapili Oktoba 27, muungano wa rais wa zamani umetoa wito wa “kuzuia” mageuzi kupitia “uhamasishaji”. Kambi ya Joseph Kabila pia ilitaka kufanyia marekebisho katiba mwaka 2015, na kuamua kusitisha mradi huo baada ya kupingwa na maandamlano raia na Kanisa.

Nchini DRC, muungano wa Common Front for Congo (FCC) unapinga  mradi wa marekebisho ya Katiba na kutoa “wito wa kuhamasisha raia wa Kongo” ili kuzuia mradi huo. Watu “watasimama” “kutetea haki zao”, “uhuru wao”, muungano wa FCC unasema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumapili jioni.

Wiki iliyopita, akiwa Kisangani, Rais Félix Tshisekedi alithibitisha nia yake ya mageuzi hayo na akataja kuanzishwa mwaka 2025 kwa tume maalum ya wataalam.

Lakini kambi ya mtangulizi wake Joseph Kabila inakataa hoja zilizotolewa na Rais Tshisekedi kuhalalisha mradi wake. Katiba ya 2006 haikuandikwa “nje ya nchi na wageni”, kama mkuu wa nchi alivyosisitiza, lakini na “wazalendo waliowakilisha makabila, dini na majimbo ya taifa la Kongo”.

“Njama ya kisiasa”

Muungano wa FCC unamshutumu rais kwa kujihusisha na “mbinu za kisiasa” ili “kugeuza umakini” kutoka kwa kutokuwa na uwezo wake wa kuhakikisha “usalama.” Muungano huo unabaini kwamba mageuzi yataleta “hatari kwa amani, umoja na utulivu wa nchi”.

Mnamo mwaka wa 2015, kambi ya Joseph Kabila, wakati huo akiwa madarakani, ilijaribu kurekebisha Katiba hii, lakini iliamua kusitisha chini ya shinikizo kutoka kwa Kanisa, maandamano na upinzani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment