Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja
Muhtasari
- Zambia yaomboleza wachezaji soka waliopoteza maisha kwa ajali ya basi
- Wanajeshi wa Korea Kaskazini wamepelekwa Urusi – NATO
- Man Utd yamfuta kazi kocha Ten Hag
- Mwanamke aliyetoweka milimani akutwa na jeraha la nyoka siku sita baadaye
- Uchaguzi wa Marekani 2024: Kwanini kauli kuhusu Puerto Rico inaweza kumponza Trump?
- Hewa chafuzi yaongezeka Delhi huku mazingira yakizidi kuwa mabaya
- Mwanaharakati wa Kenya aachiwa bila kufunguliwa mashtaka
- Hewa chafuzi yaongezeka Delhi huku mazingira yakizidi kuwa mabaya
- Je, kura za Waarabu huko Michigan zitaamua kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Marekani?
- Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran
- Rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales asema gari lake lilipigwa risasi katika jaribio la mauaji
- Trump aahidi sera ya ‘Marekani kwanza’ kuwa kipaumbele
Wanajeshi 40 wauawa katika shambulio nchini Chad

Takriban wanajeshi 40 wa Chad wameuawa baada ya kambi yao kushambuliwa Jumapili jioni, ofisi ya rais inasema.
Rais Mahamat Déby ameamuru tume ya kukabiliana na wahalifu kuwasaka wahalifu, kulingana na taarifa kutoka ofisi yake.
Shambulio hilo limeripotiwa kutokea katika kisiwa kiitwacho Barkaram, katika eneo lenye kinamasi ambalo liliwahi kufunikwa na maji ya Ziwa Chad kabla ya kupungua kwa kiasi kikubwa katika miongo ya hivi karibuni.
Hakuna washukiwa wowote wa shambulio la Jumapili waliotajwa katika taarifa ya ofisi ya rais, lakini eneo hilo liko karibu na maeneo ya mpaka wa Nigeria na Niger ambako wanamgambo wa Kijihadi wamepiga kambi.
Shambulio la Jumapili ni moja ya mashambulizi mabaya zaidi kufanywa dhidi ya wanajeshi wa Chad tangu 2020, wakati wanajeshi 100 walipouawa katika uvamizi ambao ulimfanya Rais wa wakati huo Idriss Déby kuanzisha operesheni dhidi ya wanamgambo wa wenye itikadi kali.
Ni pigo kwa Rais Déby, ambaye pia ni mwanajeshi, na mtoto wa rais wa zamani aliyeuawa miaka mitatu iliyopita katika vita dhidi ya waasi karibu na mpaka wa Libya.
Zambia yaomboleza wachezaji soka waliopoteza maisha kwa ajali ya basi

Shirikisho la Soka Zambia laomboleza baada ya wachezaji saba wa Chavuma Town Council FC kufariki katika ajali ya basi.
Shirikisho hilo limeelezea “kushtushwa” na ajali hiyo, iliyotokea Jumamosi wakati kikosi hicho kilikuwa kinasafiri kuelekea kwenye mechi ya ligi ya daraja la tatu kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
“Tunawasiliana na mamlaka ya soka, kiraia na utekelezaji wa sheria katika jimbo hili ili kutupa maelezo kamili,” rais wa shirikisho la soka Andrew Kamanga alisema.
Watu wengine 12 walijeruhiwa katika ajali hiyo, na watano kati yao wamehamishwa hadi mji mkuu Lusaka kwa matibabu.
Majina ya waliouawa na kujeruhiwa hayajatolewa.
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) Patrice Motsepe alisema yeye na bodi ya shirikisho hilo “tuna matumaini na kuomba” kwamba waliojeruhiwa watapona kabisa hivi karibuni.
“Natuma rambirambi zangu binafsi na za Caf,” Motsepe aliongeza katika taarifa yake.
“Mungu awafariji na kuwafanyia wepesi familia, marafiki, wachezaji wenzao, waliofiwa na Chama cha Soka cha Zambia.
“Nafsi za wachezaji waliopoteza maisha yao zipumzike kwa amani.”
Wanajeshi wa Korea Kaskazini wamepelekwa Urusi – NATO

Wanajeshi wa Korea Kaskazini wametumwa nchini Urusi na wanaendeleza shughuli zao katika eneo la mpaka la Kursk ambako wanajeshi wa Ukraine wana ngome, Nato imesema kwa mara ya kwanza.
Katibu Mkuu wa muungano huo Mark Rutte alisema anaweza kuthibitisha kutumwa kwa wanajeshi hao baada ya wiki kadhaa za uvumi, kufuatia mkutano na maafisa wa kijasusi na ulinzi wa Korea Kusini siku ya Jumatatu.
Mkuu huyo mpya wa Nato alisema kutumwa huko kunachochea “kuongezeka kwa kiasi kikubwa” na “kuhatarisha” vita vya Urusi nchini Ukraine.
Wiki iliyopita Rais Vladmir Putin alikataa kukanusha kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wamewasili nchini Urusi kufuatia ripoti kwamba Pyongyang inajiandaa kutuma maelfu ya wanajeshi wake kusaidia mshirika wake.
Man Utd yamfuta kazi kocha Ten Hag

Manchester United imemfuta kazi kocha Erik ten Hag baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa miaka miwili na nusu.
Mholanzi huyo aliarifiwa kuhusu uamuzi huo na bodi ya klabu hiyo Jumatatu asubuhi.
Manchester United imeanza vibaya msimu huu huku mechi ya mwisho ya Ten Hag ikiwa ya Jumapili ambapo Man Utd ilishindwa mabao 2-1 na West Ham.
United pia wako katika nafasi ya 21 kati ya timu 36 kwenye jedwali la Ligi ya Europa, wakiwa wametoka sare katika mechi zao tatu za ufunguzi.
Ruud van Nistelrooy, ambaye alijiunga na klabu hiyo kama msaidizi wa Ten Hag msimu uliopita wa joto, ametajwa kuwa kocha wa muda hadi kocha mkuu wa kudumu atakapoajiriwa.
Klabu hiyo ilikuwa imeongeza mkataba wa Ten Hag kwa mwaka mmoja kufuatia ushindi wa fainali ya Kombe la FA mwezi Mei dhidi ya Manchester City lakini zaidi ya miezi mitatu baadaye amefutwa kazi baada ya kusimamia mwanzo mbaya zaidi wa United wa pili kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
United sasa wanatafuta kocha wao wa sita wa kudumu tangu Sir Alex Ferguson astaafu mwaka 2013.
Kocha wa zamani wa Ajax Ten Hag, 54, alichukua mikoba msimu wa joto mwaka 2022 na kuiongoza klabu hiyo kushika nafasi ya tatu kwenye Ligi ya Primia katika msimu wake wa kwanza.
Pia aliiongoza United kutwaa taji lao la kwanza katika misimu sita kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle United kwenye fainali ya Kombe la Carabao 2023 na kumaliza washindi wa pili katika fainali ya Kombe la FA, wakifungwa 2-1 na Manchester City.
Msimu wake wa pili kama msimamizi wa klabu hiyo ulianza vibaya, huku United wakimaliza mkiani katika kundi lao la Ligi ya Mabingwa msimu wa vuli lakini wakatwaa kombe, na kuwalaza Manchester City katika fainali ya Kombe la FA.
Kampuni ya Sir Jim Ratcliffe ya Ineos ilinunua asilimia 27.7 ya hisa za klabu hiyo mnamo mwezi Desemba 2023 na bilionea huyo wa Uingereza aliiambia BBC Sport mnamo mwezi Februari matatizo ya klabu hiyo yaliongezeka zaidi ya jukumu la kocha.
“Katika miaka 11 iliyopita, Manchester United imekuwa na makocha wengi na hakuna aliyefanikiwa katika nyanja hiyo,” alisema Ratcliffe. “Hiyo kwangu inamaana kwamba kuna kitu ambacho hakiko sawa kimazingira.”
Lakini mwanzo mbaya wa msimu, ambao umeshuhudia United ikishinda mechi moja tu kati ya nane zilizopita katika mashindano yote, imeilazimu bodi kuchukua hatua.
Mwanamke aliyetoweka milimani akutwa na jeraha la nyoka siku sita baadaye

Mwanamke aliyetoweka kwa siku sita katika Milima ya Snowy nchini Australia amepatikana na huduma za dharura “amechanganyikiwa huku akiwa amejeruhiwa” baada ya operesheni kubwa ya utafutaji na uokoaji.
Polisi wa New South Wales walisema Lovisa Sjoberg alipatikana Jumapili alasiri kwa saa za eneo hilo, akiugua kwa kilichoshukiwa kuwa kuumwa na nyoka, upungufu wa maji mwilini na maumivu makali katika kifundo cha mguu.
Mpiga picha huyo mahiri alitibiwa majeraha yake katika eneo la tukio, kabla ya kukimbizwa hospitalini, ambapo hali yake inaendelea vizuri.
Hofu iliongezeka juu ya usalama wake baada ya kampuni ya magari ya kukodi kuripoti kuwa gari lake halijarudishwa na hakuweza kupatikana.
Baadaye gari lake lilipatikana likiwa limefunguliwa na kutelekezwa.
Polisi wa NSW walitoa ombi tarehe 21 Oktoba kwa umma kusaidia kumpata na walianza msako mkubwa kwa kutumia mbwa wa kunusa, wazima moto, walinzi wa mbuga na helikopta.
Uchaguzi wa Marekani 2024: Kwanini kauli kuhusu Puerto Rico inaweza kumponza Trump?

Suala la Puerto Rico limezua gumzo kali nchini Marekani kuelekea uchaguzi mkuu baada ya mchekeshaji mmoja kutoa matamshi ya matusi na dharau kuhusu eneo hilo la Marekani wakati mkutano wa kampeni- akielezea kama “kisiwa kinachoelea takataka”.
Wakati huo huo nyota wa Puerto-Rica, Bad Bunny ameonekana kumuunga mkono Kamala Harris hadharani, akishiriki moja ya video zake za kampeni kwenye mtandao wake wa kijamii.
Haya yanajiri wakati wagombea urais wa vyama vya Republican na Democratic wameanzisha upya juhudi za kuwashawishi wapiga kura wa Kilatino katika siku za mwisho za kampeni.
Kuna takriban wapiga kura milioni 36 wa Uhispania wanaotarajiwa kupiga kura mwaka huu, kulingana na kituo cha Utafiti cha Pew.
Kwa ujumla wamekuwa kiungo muhimu katika ushindi wa Chama cha Democratic, huku 59% ya Walatino wakimpigia kura Joe Biden mnamo 2020, kulingana Pew.
Lakini Warepublican wamekuwa wakimegua kura zao, haswa miongoni mwa Wamarekani wenye asili ya Cuba – ambao wengi wao walitambuliwa kama wafuasi wa Republican mnamo 2020.
Katika uchaguzi huo, Donald Trump aliongeza mgao wake wa kura kati ya wapiga kura wa Uhispania hadi 38% – kiwango cha juu ukilinganisha na 25% ambayo chama cha Republican kilipata lkatika uchaguzi wa ubunge wa 2018.
Wapiga kura wa Uhispania ni wachache sana katika majimbo kadhaa muhimu ambayo yataamua mshindi wa uchaguzi.
Katika jimbo la Pennsylvania lina takribani Walatino 615,000, kulingana na Pew.
Huko Arizona, ambako Donald Trump anashikilia uongozi mdogo kulingana na kura za maoni, Walatino 855,000 wanatarajiwa kupiga kura.
Ndio maana kauli iliyotolewa kwenye mkutano wa Jumapili yamepewa umuhimu kama mkubwa.
Mbunge wa chama cha Democratic Alexandria Ocasio-Cortez amewataka wapiga kura wa Kihispania huko Pennsylvania kutazama video hizo. Tayari kampeni ya Donald Trump imejitenga na matamshi hayo.
Hewa chafuzi yaongezeka Delhi huku mazingira yakizidi kuwa mabaya

Ubora wa hewa katika mji mkuu wa India Delhi umeshuka hadi viwango vibaya na duni sana katika siku chache zilizopita, data inaonyesha.
Viwango vya uchafuzi wa mazingira vilivuka mara 25-30 kiwango salama kilichopendekezwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) katika maeneo kadhaa jijini wiki iliyopita.
Wataalamu wameonya kuwa hali itazidi kuwa mbaya katika siku zijazo kutokana na hali ya hewa, matumizi ya fataki wakati wa tamasha la Diwali siku ya Alhamisi na uchomaji wa mabaki ya mazao katika majimbo jirani.
Delhi na miji kadhaa ya kaskazini mwa India huripoti viwango vya juu vya uchafuzi wa hewa kati ya Oktoba na Januari kila mwaka, na kusababisha usumbufu kwa biashara, kufungwa kwa shule na ofisi.
Mwanaharakati wa Kenya aachiwa bila kufunguliwa mashtaka

Mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu nchini Kenya Boniface Mwangi ameachiliwa bila kufunguliwa mashtaka baada ya kuzuiliwa na polisi kwa tuhuma za kuchochea ghasia, mkewe ameambia BBC.
Siku ya Jumapili, alielezea jinsi watu sita waliofunika nyuso walimchukua kwa nguvu kutoka nyumbani kwake.
Kuzuiliwa kwake kulitokea baada ya kuitisha maandamano dhidi ya serikali katika mbio za marathon katika mji mkuu, Nairobi, Jumapili.
Polisi walikuwa wamethibitisha kuwa Bw Mwangi alikuwa kizuizini lakini hawakutoa maelezo zaidi.
Kuzuiliwa kwake kulizua hasira miongoni mwa wafuasi wake, waliotaka aachiliwe.
Alikuwa akikusanya watu kwenye mtandao wa X ambao (zamani ulijulikana kama Twitter) kumtaka Rais William Ruto ajiuzulu, akitumia lebo za #RutoMustGo na #OccupyStanChart, ambazo zilirejelea mbio za Standard Chartered marathon, jina rasmi la mbio hizo.
Aliwataka watu kuvalia rangi za bendera ya taifa, kuvaa kanga zenye ujumbe “RutoMustGo” na kushirikisha nyimbo za maandamano mtandaoni.
“Kaa utuliye na amani na ufurahie!” aliongeza.
Bw Mwangi amekamatwa na kuachiliwa mara kadhaa kutokana na kampeni zake.
Iraq yailalamikia Israel kwa kutumia anga yake kuishambulia Iran

Siku ya Jumatatu, serikali ya Iraq ilitangaza katika taarifa yake kuwa imewasilisha malalamiko kwenye Umoja wa Mataifa kupinga kitendo cha Israel kutumia anga yake kuishambulia Iran.
Katika malalamiko yake yaliyoelekezwa kwa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama, Iraq ililaani matumizi ya Israel ya anga yake kuishambulia Iran.
Katika taarifa yake, Iraq ilieleza hatua ya Israel kama “ukiukaji wa wazi wa anga na mamlaka ya Iraq”.
Hapo awali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi alikuwa ameomba kikao cha dharura cha Baraza la Usalama kuhusu shambulio la Israel dhidi ya Iran katika barua aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Amesisitiza kuwa Tehran “inahifadhi” haki ya kujibu mashambulizi ya Israel.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano leo kujadili mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran.
Je, kura za Waarabu huko Michigan zitaamua kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Marekani?

Wamarekani wa asili ya Kiarabu wanajikuta katika nafasi ya kipekee na adimu katika siasa za Marekani siku hizi, huku kampeni za uchaguzi zikipamba moto na kulenga jimbo la Michigan, ambako Waarabu ni asilimia kubwa ya wakazi.
Wakati huu, uchaguzi wa rais wa Marekani ndio wenye ushindani mkubwa katika historia ya kisasa.
Hapo awali uchaguzi haujawahi kuwa karibu sana kati ya wagombea hao wawili.
Kura nyingi zinaonesha mgombea wa Chama cha Kidemokrasia Kamala Harris akiongoza katika jumla ya kura za Marekani nchini Marekani, lakini mfumo wa uchaguzi wa Marekani hautokani na kukokotoa jumla ya kura, bali ni mfumo wa wajumbe.
Mfumo ni kwamba kila jimbo lina sehemu fulani ya kura za wajumbe, ambazo ni jumla ya kura 538, zilizogawanywa kati ya majimbo yote ya Marekani, ambapo idadi ya viti katika jimbo hilo inalingana na idadi ya watu wake.
Michigan ina viti 15 vya wajumbe na ni mojawapo ya majimbo muhimu ambayo ushindani ni mkubwa kati ya Donald Trump na Kamala Harris.
Tulikwenda Michigan kukutana moja kwa moja na wapiga kura Waarabu wa Kimarekani na kufuatilia mwingiliano wao na kampeni za Trump na Harris, na muhimu zaidi, nia zao za kupiga kura, ambazo wakati huu zinaweza kuwa na jukumu kubwa katika kuchagua rais.
Mamia ya maelfu ya Waarabu wanaishi Michigan, lakini tatizo la kuhesabu kura zao na kutambua mielekeo yao si rahisi.
Rima Mroueh, mkurugenzi wa National Arab American Framework alinieleza kwamba ukweli kwamba Waarabu hawachukuliwi kama kabila tofauti, kama vile wazungu, weusi, na Walatino, katika mfumo wa sensa wa Marekani hufanya iwe vigumu kuwahesabu Waarabu, lakini alisema kuwa.
Makadirio yanaonesha kuwa idadi ya wapiga kura wa Kiarabu si chini ya 300,000.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya kikao siku ya Jumatatu kujadili shambulio la Israel dhidi ya Iran, na kuungwa mkono na Algeria, China na Urusi, kwa mujibu wa Uswisi, ambayo inashikilia kiti cha urais wa baraza la Umoja wa Mataifa.
“Vitendo vya utawala wa Israel vinatishia sana amani na usalama wa kimataifa na vinavuruga zaidi eneo ambalo tayari ni tete,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi alisema katika barua yake kwa Baraza la Usalama siku ya Jumamosi.
“Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kuzingatia kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na chini ya sheria za kimataifa, inahifadhi haki yake ya asili ya kujibu mashambulizi hayo ya kihalifu kisheria na kwa wakati ufaao,” aliongeza Araghchi.
Jeshi la Israel limesema makumi ya ndege za kivita zimekamilisha mawimbi matatu ya mashambulizi kwenye vituo vya kutengeneza makombora na maeneo mengine karibu na Tehran na magharibi mwa Iran kabla ya alfajiri ya Jumamosi.
Balozi wa Israel wa Umoja wa Mataifa Danny Danon alikataa malalamiko ya Iran ya Umoja wa Mataifa, akisema katika taarifa yake Jumapili kwamba Tehran “inajaribu kusonga mbele dhidi yetu katika uwanja wa kidiplomasia kwa madai ya kipuuzi kwamba Israel imekiuka sheria za kimataifa.”
“Kama tulivyosisitiza mara kwa mara, tuna haki na wajibu wa kujilinda, na tutatumia njia zote tulizonazo kuwalinda raia wa Israel,” aliongeza.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa “pande zote kusitisha hatua zote za kijeshi, ikiwa ni pamoja na Gaza na Lebanon, kufanya kila wawezalo kuzuia vita kamili vya kikanda, na kurejea kwenye mkondo wa kidiplomasia,” msemaji wake alisema.
Rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales asema gari lake lilipigwa risasi katika jaribio la mauaji

Evo Morales, rais wa zamani wa Bolivia, alisema siku ya Jumapili gari alilokuwa akisafiria lilipigwa risasi katika kile alichosema kama jaribio la kumuua.
Video aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii ilionesha takribani matundu mawili ya risasi kwenye kioo cha mbele cha gari katika siti ya mbele ambayo Morales alikuwa ameketi.
Katika taarifa yake, chama cha Morales, Movement for Socialism (Mas) kilisema wanaume waliovalia nguo nyeusi walifyatua risasi gari hilo lilipopita kando ya kambi ya kijeshi.
Chama hicho kilisema kimetaka serikali ya Rais Luis Arce kuwajibika. Arce alilaani vurugu katika siasa na kuahidi uchunguzi kufanyika.
Wote wawili ni wa chama tawala cha Mas. Lakini wametofautiana na uhusiano wao umekuwa mbaya zaidi tangu wote wawili walipotangaza nia yao ya kuwa wagombea wa chama cha Mas katika uchaguzi wa urais wa 2025.
Morales alidai shambulio hilo lilikuwa “operesheni ya pamoja kati ya jeshi na polisi”. Aliongeza kuwa risasi ilimkosa kwa “sentimita” na kwamba dereva wa gari hilo amejeruhiwa.
Trump aahidi sera ya ‘Marekani kwanza’ kuwa kipaumbele

Donald Trump akitoa hotuba yake katika mkutano wake mkubwa wa New York ameahidi “kurudisha ndoto ya Marekani”.
Anaahidi kufanya miji ya Marekani “salama, mizuri na safi” na “kufundisha watoto daima kuheshimu bendera yetu kuu ya Marekani”.
Trump anauambia umati Marekebisho ya Pili, ambayo yanatoa haki ya kubeba silaha, “yamekuwa yakikosolewa vikali”. Anauuliza umati kama wanataka kuacha bunduki zao na wanajibu kwa sauti kubwa ya “hapana”.
Anaahidi kuwekeza katika mpaka kama sehemu ya mbinu ya “Marekani kwanza”, akisema atafanya hivyo “katika viwango ambavyo hatujawahi kuona hapo awali”.
Trump anasema wafuasi wake wanahitaji kushinda “ajenda ya mrengo wa kushoto” ya Kamala Harris na kutoa ushindi ambao “ni mkubwa sana usiowezekana kuuhujumu”.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.