Iraq yakashifu hatua ya Israeli kutumia anga yake kuishambulia Iran

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Iraq imetuma barua kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na baraza la usalama la UN kulaani hatua ya Israeli kutumia anga yake kuishambulia jirani yake Iran.

Israeli siku ya Jumamosi ilitekeleza mashambulio ya angani dhidi ya maeneo ya kijeshi nchini Iran, hatua ambayo ilizua wasiwasi wa kuzidisha mzozo zaidi.
Israeli siku ya Jumamosi ilitekeleza mashambulio ya angani dhidi ya maeneo ya kijeshi nchini Iran, hatua ambayo ilizua wasiwasi wa kuzidisha mzozo zaidi. AP – HO

Taarifa ya waziri wa mambo ya kigeni wa Iraq Bassim Alawadi inasema hatua hiyo ya Israeli ilikiuka uhuru wa anga yake kwa kuiitumia kutekeleza mashambulio nchini Iran tarehe 26 ya mwezi huu.

Alawadi pia ameeleza kwamba wizara ya mambo ya kigeni ya Iraqi itazungumzia suala hili na Marekani mshirika wa karibu wa Israeli.

Israeli siku ya Jumamosi ilitekeleza mashambulio ya angani dhidi ya maeneo ya kijeshi nchini Iran, hatua ambayo ilizua wasiwasi wa kuzidisha mzozo zaidi.

Soma piaIsraeli yatekeleza mashambuluo dhidi ya maeneo ya kijeshi nchini Iran

Mapigano katika Ukanda wa Gaza yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya mwaka moja sasa, wakati mzozo wa Israel-Hezbollah nchini  Lebanon ukiendelea pia kuripotiwa.

Mashambulio ya Israeli yalikuwa jibu la makombora yaliorushwa nchini mwaka kutokea Iran tarehe moja ya mwezi Oktoba.

Soma piaVideo ya Benjamin Netanyahu wakati wa mashambulio dhidi ya Iran

Msemaji wa mambo ya kigeni wa Iran Esmaeil Baghaei katika taarifa yake ameeleza kwamba Tehran ilikuwa na uhakika kwamba jirani zake hawajatoa idhini kwa Israeli kutimia anga yake.

Baghdad ina uhusiano wa karibu na  Tehran na pia ni mshirika wa kimkakati wa Marekani ambayo wanajeshi wake ni sehemu ya walinda amani wa kimataifa nchini Iraq.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment