Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Marekani, kampeni za uchaguzi wa urais, utakaofanyika Jumanne wiki ijayo, zimeingia siku za mwisho.
Wagombea wakuu, rais wa zamani Donald Trump na Makamu wa rais Kamala Harris, wameendelea kuzua majimbo mbalimbali kuomba kura.
Trump anayepeperusha bendera ya chama cha Republican amekuwa katika uwanja wa Madison Square Garden jijini New York, ambapo amewaambia Wamarekani wamchague ili alete mabadiliko makubwa.
“Changamoto zote tunazopitia zinaweza kutatuliwa. Hatima ya nchi hii sasa iko mikononi mwetu. Jumanne ijayo mjitokeze na kumwambia Kamala Harris kuwa umefanya kazi mbaya sana pamoja na Biden.” Alisema Donald Trump.
Naye Makamu wa rais Kamala Harris kutoka chama cha Democratic ambaye ataingia kwenye vitabu vya historia iwapo atachuuliwa amekuwa katika jimbo la Pennsylvania, ambapo amewaambia wafuasi wake kuwa kumchagua itakuwa ni hatua ya kulinda demokrasia ya Marekani.
“Tunapigania demokrasia na tunaheshimu sauti ya kila mmoja. Tuna siku tisa tu, kupigania demokrasia hiyo. Tuna fursa ya kipekee ya kubadilisha ukurasa wetu na kuachana na siasa na uoga na mgawanyiko ambazo zimekuwa zikienezwa kwa miongo kadhaa na Donald Trump.” Alisema Kamala Harris.
Kuelekea uchaguzi huo wa Novemba tarehe tano, tayari Wamarekani wapatao Milioni 41 wameshapiga kura za mapema kwenye kinyanganyiro hicho kinachotarajiwa kuwa na upinzani mkali kati ya DonaldTrump na Kamala Harris.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.