Kwa WANANDOA Wanaotaka Mafanikio Ya KIFEDHA…
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Kutimiza Mahitaji Muhimu
ii. Kulea Watoto / Parenting tool
iii. Inadhihirisha Tabia
iv. Uimara wa Mwanaume
v. Kuleta Utulivu na Amani
Katika makala hii tutazungumzia nafasi ya nne ya pesa katika ndoa.
– Uimara Wa Mwanaume
Uimara wa mwanaume katika ndoa yake unategemea sana uwezo wake wa kumudu gharama za kipesa ambazo zinatakiwa.
Kunapokuwa na changamoto ya pesa, mara nyingi mwanaume anapoteza hali yake ya kujiamini kama mwanaume kamili (Manhood).
Hii ni kwa sababu kwa asili mwanaume ameumbwa kuwa mtoaji na mtunzaji (Provider), hivyo ni muhimu sana awe na uwezo wa kufanya hivyo.
Ikitokea akashindwa kukamilisha jukumu hili, kinachotokea ni hali ya kupoteza hali yake ya kujiamini.
Kutokana na hili ndio maana wanaume wengine wakikosa pesa huwa wanaamua kupotea nyumbani.
Kukaa mbali na familia au wanakuwa wakali kila wakati.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.