Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mbinu 5 Za Kuondoa Migogoro Inayosababishwa na Pesa Kwenye Ndoa.
i. Kukubaliana Falsafa Yenu Ya Pesa
ii. Kuwa na Maono ya Pamoja Kuhusu Pesa
iii. Kuweka Malengo Ya Pamoja Ya Kifamilia
iv. Kupanga Bajeti Ya Pamoja
v. Utaratibu Wa Msaada Kwa Ndugu
Katika Makala Hii Tutazungumzia Mbinu ya Pili.
– Kuwa na Maono ya Pamoja Kuhusu Pesa
Hapa kama wanandoa mnatakiwa mkae chini na mjiulize, hivi sisi maono yetu kuhusu pesa ni yapi?
Ni hatari sana pale ambapo mmoja wenu anataka kuwa tajiri sana wakati mwingine anasema “Mimi nataka maisha ya kawaida tu”.
Kumbuka hamuwezi kufanya mambo makubwa kwenye maisha kama hamjaoanisha maono yenu.
Maono yenu kuhusu pesa yanahusisha picha yenu kubwa ya Maisha ambayo mnataka kuyaishi huko mbeleni.
Kwa mfano:
• Mngependa kuja kuishi nyumba ya namna gani, ya fahari kubwa au ya kawaida tu?
• Mngependa kuwa mnaenda likizo wapi?
• Mngependa kuwa na uwekezaji wa kiwango gani?
• Mngependa kuendesha gari la aina gani mtakapofanikiwa kifedha?
• Mngependa kuwa mnaingiza kiasi gani katika uzee wenu hata bila kulazimika kuendelea kufanya kazi?
Yapitieni maswali haya kama sehemu muhimu ya kujenga maono yenu ya pamoja kuhusu pesa
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.