Chanzo cha ugomvi katika familia….

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Chanzo kimojawapo cha Ugomvi kwenye familia nyingi ni “ndugu wachonganishi”.

Kuna ile aina ya ndugu ambao kazi yao kubwa ni kuchukua maneno upande mmoja na kupeleka kwingine.

Wengi wa aina hii ya ndugu huwa wanapenda sana kutembelea ndugu mbalimbali, wanahudhuria matukio kwa bidii na huwa wana juhudi ya kupiga simu kusalimia.

Yaani, ukiwatathmini kwa harakaharaka, utaona ni ndugu ambao wanajitoa sana na wanaelewana na kila mtu.

Shida Yao ni moja tu, kuongeaongea hovyo. Yaani kwanza hawa hawana Siri, chochote mtakachoongea, au watakachosikia unaongea au watakachokiona kwako, watakipeleka mahali pengine.

Shida ni kuwa, Mara nyingi wanaongeza chumvi na pia wanabadilisha maana ya ulichoongea.

Waulize sasa: Wataruka mita 100 kukataa kuwa hawajasema kabisa.

Ukiwagundua hawa, wawekee mipaka unachozungumza nao na unachowaonesha kabla hawajakugombanisha na ukoo mzima.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment