Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Niger Hama Amadou amefariki dunia akiwa na miaka 74

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Niger, aliyekuwa Waziri Mkuu Hama Amadou, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74.

Hama Amadou amefariki dunia na kuacha kumkumbuku ya muda mrefu ya utumishi wa umma katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
Hama Amadou amefariki dunia na kuacha kumkumbuku ya muda mrefu ya utumishi wa umma katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Associated Press – SIGI TISCHLER

Kifo cha Amadou, kilitokea siku ya Jumatano jioni baada ya kukimbizwa hospitalini kwenda kupata matibabu dhidi ya maambukizo ya Malaria.

Mwanasiasa huyo mkongwe amefariki dunia na kuacha kumkumbuku ya muda mrefu ya utumishi wa umma katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mwaka 2009, alifungwa jela kwa madai ya wizi za fedha za umma, lakini pia alishtumiwa kwa kupanga kuondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi, kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Mamadou Tandja.

Hama Amadou aliyekuwa Waziri Mkuu wa Niger.
Hama Amadou aliyekuwa Waziri Mkuu wa Niger. AFP – ISSOUF SANOGO

Kati ya mwaka 2011 na 2016, alikuwa mpinzani mkuu wa aliyekuwa rais Mahamadou Issoufou, kabla ya kukimbia nchi kwa sababu za kisiasa baada ya kumaliza wa pili wakati wa uchaguzi wa mwaka 2016.

Mwaka 2021 alifungwa tena jela na kuachiwa huru miezi miwili baadaye kwa sababu za kiafya na kukimbilia nchini Ufaransa na kurejea jijini Niamey baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa madarakani aliyekuwa rais Mohammed Bazom.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment