Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
Mahakama ya kijeshi nchini Uganda, imewahukumu wafuasi 16 wa chama cha upinzani NUP, miaka 5 jela baada ya kuwakuta na ya makosa ya usaliti na kumiliki vilipuzi.

Hata hivyo mahakama hiyo imesema baadhi ya watuhumiwa akiwemo Olivia Lutaaya, watafungwa kwa miezi tatu kutokana na uhalisia kwamba tayari wametumikia miaka tatu jela.
Hili likiafikiwa baada ya washukiwa hao kukubali makosa na wamekuwa wakihudhuria vikao vya mahakama.
Soma piaUganda: Wafuasi wa chama cha Bobi Wine wakutwa na hatia ya kumiliki vilipuzi
Hata hivyo watuhumiwa hao wamesema watakataa rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliotolewa na Brigidia Freeman Mugabe.
Watuhumiwa hao walikamatwa mwaka 2021, wakihusishwa na maandamano ya kupinga matekeo ya uchaguzi wa uarais wa mwaka 2021.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.