Wanawake wengi waliuawa katika maeneo yenye migogoro duniani: UN

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Idadi ya wanawake waliouawa katika maeneo yenye migogoro duniani kote imeongezeka maradufu mwaka jana, ambapo sasa wanachukua asilimia 40 ya watu wote waliouawa katika maeneo ya vita, hii ni kulingana na ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa.

Makaazi ya watu yalioharibiwa katika mashambulio ya Urusi nchini Ukraine, wanawake na watoto wakiwa miongoni mwa waliouawa.
Makaazi ya watu yalioharibiwa katika mashambulio ya Urusi nchini Ukraine, wanawake na watoto wakiwa miongoni mwa waliouawa. © Ukrainian Emergency Service via AP

Ripoti hii iliyochapishwa na shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake, iliangazia hali ya usalama wa wanawake na wasichana walioathiriwa na vita, ikianisha matukio yaliyothibitishwa na Umoja wa Mataifa kuhusu vitendo vya unyanyasaji wa kingono na migogoro viliongezeka kwa asilimia 50 mwaka 2023 ikilinganishwa na 2022.

Umoja wa Mataifa umerekodi angalau vifo vya raia elfu 33 katika maeneo yenye mizozo mwaka uliopita, ambapo zaidi ya elfu 13 kati yao au wanne katika kila watu 10 waliouawa, walikuwa wanawake na watatu kati ya 10 walikuwa watoto.

Watu waliokimbia makazi yao nchini DRC ambao kwa sasa wanaishi katika kambi za wakimbizi mashariki ya nchi hiyo ambapo wanawake na watoto wameathirika pakubwa.
Watu waliokimbia makazi yao nchini DRC ambao kwa sasa wanaishi katika kambi za wakimbizi mashariki ya nchi hiyo ambapo wanawake na watoto wameathirika pakubwa. AP – Moses Sawasawa

Ripoti inasema dunia imenaswa “katika wimbi la kutisha la migogoro, ukosefu wa utulivu na ghasia” na migogoro ya silaha 170 ilinakiliwa mwaka wa 2023, watafiti wakionesha picha ya kutisha ya kuongezeka kwa madhara ya vita kwa wanawake na wasichana duniani kote.

Nchini Sudan, ambako kumekuwa na ripoti nyingi za unyanyasaji wa kijinsia, UN ikisema waathiriwa wengi hawakuweza kupata huduma za matibabu katika muda wa saa 72 baada ya kubakwa, baadhi wakikataliwa kutoa mimba kwa sababu ilikuwa nje ya muda uliowekwa kisheria.

Nchini Sudan wanawake pia wameripotiwa kukabiliwa na vitendo vya ubakaji kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF.
Nchini Sudan wanawake pia wameripotiwa kukabiliwa na vitendo vya ubakaji kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF. © AP

Ripoti hii inakuja miaka 24 baada ya kupitishwa kwa azimio nambari 1325 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo linatoa wito kwa pande zote kwenye migogoro kuhakikisha usalama wa wanawake na wasichana, na ushiriki kamili wa wanawake katika michakato ya amani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment