Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja ya changamoto kubwa ambayo iko kwa sasa duniani ni “Bullying” (Kufanyiwa mambo endelevu yanayokusababishia maumivu, kukuondolea kujiamini n.k).
Wapo ambao wanaipata kutoka kwa mwezi, Mzazi au hata Bosi wake Ofisini.
Kuna watu wananyanyasa watu kupitia mitandao (Cyber Bullying), yaani mtu anaanza kumtukana, kumsema hovyo, kumdhalilisha na kumuabisha mwingine waziwazi.
Wapo ambao wanafanya “Leadership Bullying”, yaani anatumia nafasi yake ya Uongozi kunyanyasa wengine, kuwaadhibu bila kosa, kuwasemea maneno ya kuwadhalilisha n.k
Kwa mujibu wa tafiti nyingi za kisaikolojia, watu wengi wanaofanya hivi ni kwa sababu wamepoteza Uwezo na Hali Yao ya Kujiamini.
Kwa mujibu wa Shay Mitchell anasema “ ..Bullying never has to do with you. It’s bully who is insecure”.
Yaani, ukimuona mtu anatumia mbinu hii kwako, tatizo haliko kwako bali ni yeye ndiye amepoteza hali ya kujiamini.
Kitu Unachotakiwa kukumbuka ni kuwa, ukimruhusu akupelekeshe na tabia hiyo kila siku ataongeza nguvu ya manyanyaso dhidi yako.
Jitetee!
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.