Waimbaji wanaoi bukia katika,huduma[Limbukeni]

Mungu amekupa huduma nzuri sana lakini inahitaji unyenyekevu sana maana aliyepewa wa kwanza (rucifer) ilimshinda kwa sababu ya kiburi.

Ufuatao ni ushauri wangu, ili ufike mbali.
1. Ukiitwa kuimba na ukanyimwa nauli usitangaze wala kunung’unika.

2. Ukipewa kuimba wa kwanza usijione hujaheshimiwa, maana kuimba mwisho baada ya wengine kuimba haimaanishi wewe ni mwimbaji mkubwa kuliko wengine.

3. Ukiitwa kuimba wakati wa kutoa sadaka usijisikie vibaya na kudhani wamekudharau, sadaka ni sehemu ya ibada hivyo imba kwa furaha, usitishwe na movement za watu, UKIHISI HAWAKUSIKILIZI JIFUNZE KUJISIKILIZA MWENYEWE.

4. Ukiitwa kuimba watu wanapotoka usikasirike, imba kwa furaha maana ibada yako ya sifa inamuhusu Mungu ambaye wakati huo anakuwepo wala hatoki, HIVYO MUHESHIMU HUYO.

5. Ukisahauliwa kupewa nafasi ya kuimba usihangaike kukumbusha kuwa upo. KAMWE USING’ANG’ANIZE MAANA ALIYEKUPA HUDUMA ANAJUA UPO, HIVYO USIMCHUKIE MWONGOZA IBADA KWA KUKUSAHAU, RATIBA ZA KUIMBA ANAZO MUNGU HUYO UNAMUONEA TU.

6. Ukiambiwa ratiba jumapili zimebana uje kuimba ibada za katikati ya wiki, usiseme hawajakuheshimu MAANA SIKU ZOTE NI ZA MUNGU KAMA ILIVYO JUMAPILI NENDA KAIMBE TENA USIKOSE.

7. Ukialikwa na kukuta watu wachache kuliko ulivyodhani USIPUNGUZE KIWANGO NA MORALI YAKO YA KUHUDUMU. JIWEKEE MALENGO YA KUKUTANA NA MTU MMOJA NA HUYO MTU UWE WEWE, ILI HATA UKIKOSA MTU UJIIMBIE WEWE NA UMUIMBIE MUNGU WAKO KWA SIRI. Ukifanya hivyo hata ukimkuta mmoja utakuwa na amani maana utaona mko wengi kuliko ulivyopanga.

8. Ukikuta vyombo vibovu usilaumu maana hujachangia gharama za vyombo, Fanya kilichokuleta, KUMBUKA WAO WAMEVIZOEA NA WANAKUSIKIA NA UBOVU WA VYOMBO VYAO HIVYO KAMA UNAJISIKIA WEWE INATOSHA, TIMIZA WAJIBU WAKO.

9. Ukilazwa sehemu duni, ukapewa chakula duni, usihame wala usiombe chakula bora zaidi, labda kama utafanya hivyo kwa gharama zako, ila pia tumia hekima ili wenyeji wako wasijisikie vibaya wakakwazika. MAANA UWEZO WAO HUENDA UMEISHIA HAPO NA WALICHOKUANDALIA NDIO CHA KIWANGO CHA JUU NA MWISHO WA UWEZO WAO, USIENDE ZAIDI YAO BALI TUMIA HEKIMA, MAANA HUTAKONDA WALA KUFA UKICHUKULIANA NAO.

10. Ukiombwa wimbo usikatae ila kama una sababu basi tumia hekima kuwaelewesha, maana wanaweza kuomba wimbo nawe ndani yako ukasikia Roho anakuongoza kuimba wimbo mwingine, BILA SHAKA ROHO WA MUNGU ATAKUPA AMANI NA HEKIMA YA KUAMUA NA WOTE WAKABAKI NA AMANI.

11. Kama itatokea mwenzio kafanya vizuri na kashangiliwa kuliko WEWE usione wivu, na kama roho itakuuma basi pambana nayo kwa kumuombea ili akisimama tena wamshangie zaidi ya vile roho ilivyokuuma.

12. Usiposhangiliwa usijisikie vibaya ukahisi umekosea, kushangiliwa ama kutoshangiliwa sio ishara ya kufanya vizuri ama vibaya.

13.Uwapo ugenini jiepushe kukaribisha watu hasa wa jinsia tofauti mahali unapolala hata kama ndugu ni zako onana nao kanisani, MAANA HAKUNA ATAKAYEJUA NI NDUGU YAKO. NA IKITOKEA WAMEKUJA BASI ZINGATIA USHUHUDA NA USALAMA ILI KUMPONYA MWENYE MASHAKA.

14. Ukiimba kaa mahali ulipoandaliwa, usitoke mpaka ibada iishe, hata kama unabanwa na haja,, kama unauwezo wa kuvumilia kaa maana hautakufa. USIENDE NJE NA KUANZA KUPIGA STORY NI UTOTO NA UTOVU WA NIDHAMU KWA MUNGU NA KWA WENYEJI WAKO.

15. Usilazimishe vitu, usilazimishe na kushawishi nguvu ya Mungu, wakati ndani ya moyo wako unajua haipo, usinene lugha ambayo chanzo sio Roho wa Mungu, ili kuwahadaa watu uko rohoni, kwanza umeitwa kuimba fanya kazi yako. BALI KILA JAMBO LIFANYIKE KWA DALILI YA ROHO MTAKATIFU.

MWISHO UWE NA KIASI KWA KILA JAMBO.
Nawatakiwa mwaka mpya mwema naamini Mungu kakupa kazi njema sana, ila vitu hivi vinaweza kuiharibu huduma yako na kusababisha usidumu kama ilivyokusudiwa.

CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!

Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment