Usijipe umuhimu mahala hapatakikani.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja ya kitu ambacho lazima uamue kukiacha kama unataka kufanikiwa, ni hiki:

Acha kujipa umuhimu mahali usipokuwa na umuhimu.

Watu wengi wanaumia sana kwa sababu hii.

Si unajua kuwa, kuna watu ambao ndani ya moyo wako umewapa “grade one” Tena VIP.

Ila wao ndani ya mioyo yao wewe ni nyongeza.

Au haujui kuwa, kuna watu ambao umewapa kipaumbele kwa kuacha mambo muhimu ili uwape nafasi.

Ila wao wanakupa nafasi wakiona wamemaliza yote muhimu.

Jifunze kusoma watu kwa Matendo Yao sio maneno Yao.

Usijiweke ambapo haujawekwa.

Hii itakupunguzia kulaumu na kuumia.

Usilazimishe kuwa muhimu kwa anayekuona wa kawaida.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment