Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wakili wa mgombea mkuu wa upinzani nchini Msumbiji Venancio Mondlane, aliyewania uchaguzi mkuu wa urais wa tarehe 9 ya mwezi Oktoba ameuawa mjini Maputo.
Wakili huyo Elvino Dias, ameuawa pamoja na mgombea mwengine, Paulo Guambe, wa chama cha Podemos kilichokuwa kinamuunga mkono Mondlane.
Wawili hao walipigiwa risasi wakiwa kwenye gari lao ambalo lilikuwa limeegeshwa katika mji mkuu kwa mujibu wa walioshuhudia.
Kiongozi wa chama cha Podemos, Albino Forquilha amethibitisha kuuawa kwa wawili hao wakati chama cha mawakili kikieleza kushangazwa na mauaji ya Dias.
Mashirika ya kiraia kwenye taifa hilo yametaja mauaji hao kama njia moja ya kuwatishia wapinzani pamoja na kuminya demokrasia. Polisi wanasema wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo licha ya kutotoa taarifa kamili kuhusiana na waliouawa.
Raia wa Msumbiji wanasubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu ambayo yanatarajiwa kuchapishwa tarehe 24 ya mwezi huu.
Mondlane, ambaye alitoa upinzani mkubwa kwa chama tawala cha Frelimo ambacho kimekuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 49 amedai kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
Amedai kuwepo kwa udaganyifu, chama cha Frelimo kikidai kwamba kinaoongoza katika zoezi la kuhesabu kura na tayari ameitisha maandamano siku ya Jumatatu.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.