Afrika Leo Jioni-18-10-2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Karibu katika Matangazo yetu ya Afrika Leo Jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja

MUHTASARI

  • Kiongozi mkuu wa Hamas athibitisha kifo cha Yahya Sinwar
  • Mahakama yasitisha kuondolewa kwa Gachagua ofisini
  • Lebanon yaishutumu Iran kwa kuingilia masuala yake ya ndani
  • IDF yasema imewaua wapiganaji walioingia Israel kutoka Jordan
  • Gachagua yuko katika hali nzuri kiafya – Daktari
  • Serikali yachapisha kwenye gazeti lake kuondolewa mamlakani kwa Gachagua, huku Rais Ruto akipanga kumteua Naibu Rais mpya
  • Jaji azuia dakika za mwisho kunyongwa kwa mwanaume aliyedaiwa kumuua mwanaye Texas
  • Hezbollah yasema itazidisha vita na Israel baada ya kiongozi wa Hamas kuuawa
  • Idara ya huduma za usalama ya Marekani ina ‘dosari kubwa’ na lazima ibadilishe uongozi, ripoti yanasema
  • Kiongozi wa Hamas Yahya Al-Sinwar ameuawa na kifaru cha kijeshi baada ya kufanya makosa, IDF yaiambia

Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Jioni  moja kwa moja ikiwa ni tarehe 18/10/2024 Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.

Hezbollah kuzidisha mzozo na Israeli kufuatia kifo cha kiongozi wa Hamas

Wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon wameapa kuzidisha mapambano dhidi ya Israeli wakati Iran nayo ikisisitiza kwamba roho ua uasi itatiwa nguvu zaidi kufuatia kifo cha kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar.

Kundi la Hamas halijazungumzia ripoti ya kuuawa kwa kiongozi wake Yahya Sinouar katika Ukanda wa Gaza.
Kundi la Hamas halijazungumzia ripoti ya kuuawa kwa kiongozi wake Yahya Sinouar katika Ukanda wa Gaza. AP – Adel Hana

Sinwar, aliyepanga shambulio la tarehe 7 ya mwezi Oktoba na ambalo lilisababisha kuzuka kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza, aliuuawa katika oparesheni ya wanajeshi wa Israeli huko Gaza.

Viongozi wa mataifa ya Magharibi wanasema kifo chake kinatoa nafasi ya kumalizika kwa mzozo unaoendelea lakini Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameahidi kuendelea na vita hadi pale ambapo mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas wataachiwa huru.

Raia wa Israeli baada ya kupata taarifa ya kuuawa kwa kiongozi wa Hamas
Raia wa Israeli baada ya kupata taarifa ya kuuawa kwa kiongozi wa Hamas REUTERS – Amir Cohen

Sinwar, ambaye aliteuliwa kuhudumu katika wadhifa wa kiongozi Hamas baada ya mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo Ismail Haniyeh mjini Tehran mwezi Julai, alidaiwa kujificha katika mahandaki yaliojengwa katika ukanda wa Gaza.

Aliuawa katika makabiliano ya risasi kusini mwa Gaza siku ya Jumatano na wanajeshi wa Israeli ambao hata hivyo wanasema hawakujua wamefanikiwa kumpata adui namba moja wa taifa lake.

Israeli inasema kiongozi huyo wa Hamas alikuwa amejificha kwenye handaki
Israeli inasema kiongozi huyo wa Hamas alikuwa amejificha kwenye handaki REUTERS – Mohammed Salem

Jeshi la Israeli limechapisha video iliyonaswa na ndege isio na rubani kuonyesha kile linasema ni ya Sinwar, akiwa ameuawa katika jengo ambalo waliharibu.

Hamas haijazungumzia rasmi suala hili japokuwa taarifa za ndani kutoka kwenye kundi hilo zinasema kiongozi wao aliuuawa na wanajeshi wa Israeli.

Korea Kaskazini kutuma wanajeshi nchini Ukraine kuisaidia Urusi: Korea Kusini

Korea Kaskazini imeamua kutuma idadi kubwa ya wanajeshi kusaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la nchini Korea Kusini Yonhap likinuku idara ya ujasusi ya Seoul.

Imechapishwa: 18/10/2024 – 12:28Imehaririwa: 18/10/2024 – 13:12

Dakika 2

Korea kusini inasema Korea ya Kaskazini inawatuma wanajeshi wake kwenda kuisaidia Urusi kupigana dhidi ya Ukraine.
Korea kusini inasema Korea ya Kaskazini inawatuma wanajeshi wake kwenda kuisaidia Urusi kupigana dhidi ya Ukraine. via REUTERS – Gavriil Grigorov

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Korea Kaskazini imeamua kuwatuma karibia wanajeshi wake 12,000 wakiwemo wale wa kitengo maalum kupigana nchini Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika taarifa siku ya Alhamis, alidai kuwa na ripoti za kijasusi kwamba Korea Kaskazini ilikuwa inatoa mafunzo kwa wanajeshi Elfu 10 kwenda kuisaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Kyiv.

Zelensky alidokeza kwamba Urusi ilikuwa inategemea pakubwa wanajeshi wa Korea Kaskazini kujaza nafasi ya maofisa wake waliofariki katika mapambano.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. REUTERS – Johanna Geron

Rais wa Korea ya Kusini Yoon Suk Yeol amekuwa na kikao cha dharura cha usalama kuhusiana na hatua hiyo ya Pyongyang.

Katika kikao hicho imejadiliwa kwamba uhusiano wa karibu wa kijeshi kati ya Urusi na Korea Kaskazini ulikuwa umeenda zaidi ya uhamishaji wa silaha hadi usafirishaji wa wanajeshi kwenda nchini Urusi.

Pyongyang na Moscow zimekuwa na uhusiano tangu kuasisiwa kwa nchi ya Korea Kaskazini baada ya vita vya pili vya dunia, ushirikiano ambao hata hivyo umeonekana kuongezeka tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwaka wa 2022.

Uhusiano kati ya Urusi na Korea kaskazini umekuwa ukiendelea kuimarika tangu kutokea kwa uvamizi wa Moscow nchini Ukraine.
Uhusiano kati ya Urusi na Korea kaskazini umekuwa ukiendelea kuimarika tangu kutokea kwa uvamizi wa Moscow nchini Ukraine. © Vladimir Smirnov / AFP

Marekani na Korea Kusini zimekuwa zikisisitiza kwamba Rais Kim Jong Un alikuwa anatuma silaha kwenda nchini Ukraine.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alifanya ziara jijini Pyongyang mwezi Juni, mataifa hayo mawili yakitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi.

Mapema mwezi huu, vyombo vya habari nchini Ukraine viliripoti kwamba wanajeshi sita wa Korea Kaskazini waliuawa katika shambulio la Ukraine karibu na mji wa Donetsk tarehe  3 ya mwezi Oktoba.

Korea Kaskazini kutuma wanajeshi kuisadia Urusi: SeoulthChanzo cha picha,ReutersKorea Kaskazini imeanza kutuma wanajeshi kupigana pamoja na wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine, shirika la kijasusi la Korea Kusini limesema huku Seoul ikionya kuhusu “tishio kubwa la usalama”.Madai hayo yanakuja siku moja baada ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kusema anaamini kuwa wanajeshi 10,000 wa Korea Kaskazini wanaweza kujiunga na vita hivyo kutokana na taarifa za kijasusi.Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol aliitisha mkutano wa usalama siku ya Ijumaa na kusema jumuiya ya kimataifa lazima ijibu kwa “njia zote zilizopo”.Kulingana na shirika hilo la kijasusi, wanajeshi 1,500 tayari wamewasili nchini Urusi – huku duru zisizojulikana zikiambia vyombo vya habari vya Korea Kusini kwamba huenda idadi ya mwisho inaweza kuwa karibu 12,000.Haya yanajiri huku ushahidi ukiongezeka kuwa Korea Kaskazini inaipatia Urusi risasi, kama ilivyodhihirishwa hivi karibuni na kupatikana kwa kombora katika eneo la Poltava nchini Ukraine.Moscow na Pyongyang pia zimekuwa zikiimarisha ushirikiano wao katika miezi ya hivi karibuni. Wiki iliyopita, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alimsalimia Rais wa Urusi Vladimir Putin katika siku yake ya kuzaliwa, akimwita “rafiki wake wa karibu” .Mkutano wa usalama wa Ijumaa ulihudhuriwa na maafisa wakuu kutoka Ofisi ya Usalama wa Kitaifa ya Korea Kusini, Wizara ya Ulinzi wa Kitaifa, na Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi, ofisi ya Yoon ilisema.”[Washiriki] waliamua kutopuuza hali hiyo na kuijibu kwa pamoja na jumuiya ya kimataifa kwa kutumia njia zote zilizopo,” ilisema.Madai hayo ya Idara ya Kitaifa ya Ujasusi yanakuja siku chache baada ya vyanzo vya kijasusi vya jeshi la Ukraine kusema kuwa jeshi la Urusi linaunda kikosi cha Wakorea Kaskazini.

Biden na Scholz wanachukulia kifo cha Sinwar kama fursa ya amani Mashariki ya Kati

Joe Biden yuko katika ziara yake ya kwanza Berlin tangu awe rais
Maelezo ya picha,Joe Biden yuko katika ziara yake ya kwanza Berlin tangu awe rais

Kifo cha kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar kinawakilisha “wakati wa haki”, anasema Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye anafanya mazungumzo mjini Berlin na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani.

Biden alisema Sinwar ilikuwa na damu ya Wamarekani, Waisraeli, Wapalestina, Wajerumani na wengine wengi mikononi mwake, viongozi hao wawili walikubaliana kwamba kifo chake ni ahueni kwa waathirika.

Scholz alisema kifo cha Sinwar kinatoa furasa ya kfikiwa kwa “matarajio halisi ya kusitishwa kwa mapigano huko Gaza na makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka wa Hamas”.

Biden alisema alimwambia waziri mkuu wa Israel: “Naomba tutumie hii fursa ya kutafuta mpango wa amani – mustakabali bora wa Gaza bila Hamas.”

Biden pia atakutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Emmanuel Macron wa Ufaransa wakati wa ziara yake mjini Berlin.

Pamoja na matukio ya Mashariki ya Kati, wanatarajiwa pia kujadili vita vya Urusi nchini Ukraine.

Biden aliwaambia waandishi wa habari kwamba nchi za Magharibi zilipaswa kudumisha uungaji mkono kwa Ukraine katika mapambano yake dhidi ya Urusi.

Kiongozi mkuu wa Hamas athibitisha kifo cha Yahya Sinwar

Al-Hayya, kwenye picha iliyopigwa mapema mwaka huu, ndiye mtu mkuu zaidi katika Hamas baada ya kiongozi wake aliyeuawa Yahya Sinwar.
Maelezo ya picha,Al-Hayya, kwenye picha iliyopigwa mapema mwaka huu, ndiye mtu mkuu zaidi katika Hamas baada ya kiongozi wake aliyeuawa Yahya Sinwar.

Afisa mkuu wa Hamas amethibitisha kifo cha kiongozi wa kundi hilo, Yahya Sinwar.

Katika taarifa ya video, Khalil al-Hayya anaendelea kusema kwamba Sinwar alikufa katika mapigano.

Khalil al-Hayya anasema kuwa kundi hilo litaendelea na juhudi zake ili kufikia malengo ya wananchi wa Palestina na kuongeza kuwa, kifo cha Sinwar kitazidi kuimarisha kundi hilo.

Anaongeza kuwa mateka wa Israel hawatarejeshwa hadi uvamizi wa Gaza utakapomalizika na majeshi ya Israel kuondolewa katika Ukanda huo.

Al-Hayya ndiye mkuu zaidi katika kundi la Hamas baada ya Sinwar, ambaye aliuawa wakati wa msako wa kawaida wa wanachama wa Hamas huko Rafah siku ya Alhamisi.

Mahakama yasitisha kuondolewa kwa Gachagua ofisini

Gachagua
Maelezo ya picha,Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua

Mahakama kuu imesitisha utekelezwaji wa azimio la Seneti la kuidhinisha mashtaka ya kumuondoa madarakani Rigathi Gachagua.

Uamuzi huo umetolewa muda mfupi tu baada ya Bunge la Kitaifa kuafiki uteuzi wa Kithure Kindiki kuwa Naibu wa Rais baada ya Rais William Ruto kuwasilisha jina lake kwenye bunge hilo.

Hapo jana Maseneta nchini humo waliidhinisha mashtaka 5 kati ya 11 dhidi ya Gachagua na kumuondoa ofisini.

Gachagua alikosa kufika mbele ya maseneta kujitetea baada ya mawakili wake kusema alipatwa na ”maumivu makali ya kifua” na kulazimika kulazwa hospitalini.

Uamuzi uliotolewa na Jaji E.C. Mwita umezuia kutekelezwa kwa azimio hilo la seneti na pia kuzuia rais kumteua mtu kuichukua nafasi hiyo hadi tarehe 24 mwezi huu hadi kesi hiyo sikilizwe na jopo la majaji watakaoteuliwa na Jaji Mkuu Martha Koome.

Hata hivyo tayari rais amependekeza jina la Kithure Kindiki kuichukua nafasi ya Gachagua na bunge la taifa kuafiki uteuzi wake.

Bunge la Kenya lamuidhinisha Profesa Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais

Kindiki

Wabunge nchini Kenya muda mfupi uliopita wamepiga kura kwa kauli moja kuafiki uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais mpya.

Wabunge wote 236 waliokuwa bungeni wamepiga kura kuunga mkono uteuzi wa Rais

Hii ni baada ya Rais William Ruto kuwasilisha jina la Profesa Kindiki kwa Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula kupendekeza achukuwe wadhifa huo.

Nafasi ya Naibu Rais iliachwa wazi baada ya Rigathi Gachagua kuondolewa madarakani kupitia mchakato wa kikatiba.

Kilichosalia sasa ni Spika wa Bunge kuchapisha hatua hiyo katika Gazeti rasmi la serikali.

Lebanon yaishutumu Iran kwa kuingilia masuala yake ya ndani

xx

Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati ameelezea kughadhabishwa kwake na kauli iliyotolewa na spika wa bunge la Iran juu ya mustakabali wa kusini mwa Lebanon.

Spika wa Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amejitolea kufanya mazungumzo na Ufaransa kuhusu azimio nambari 1701 la Umoja wa Mataifa, ambalo lilimaliza mzozo mkubwa wa mwisho kati ya Israel na Hezbollah mwaka 2006 na kuupa Umoja wa Mataifa mamlaka ya kulisaidia jeshi la Lebanon kudumisha amani.

Mikati alielezea kauli ya Iran kama “uingiliaji wa wazi katika masuala ya Lebanon na jaribio la kuanzisha ulezi usiokubalika dhidi ya Lebanon”.

Hezbollah inachukuliwa kuwa wakala wa Iran – ambayo hutoa ufadhili wake mwingi na silaha – na kwa kambi yake kubwa ya wabunge bungeni, ina ushawishi mkubwa kwa serikali ya Lebanon.

Qalibaf alikuwa Lebanon wikendi iliyopita tu, alipokutana na waziri mkuu.

Mikati anasema ameomba baraza la mawaziri la Iran kutoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa hiyo – akiongeza kwamba mazungumzo yoyote kuhusu Azimio nambari 1701 yanapaswa kufanywa na serikali ya Lebanon.

IDF yasema imewaua wapiganaji walioingia Israel kutoka Jordan

Jeshi la Israel (IDF) linasema kuwa limewaua watu wawili wenye silaha waliovuka na kuingia nchini humo kutoka Jordan.

Katika taarifa fupi iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X , IDF inasema “ilitambua idadi kubwa ya magaidi” kusini mwa Bahari ya Chumvi.

Wanajeshi wa Israel walitumwa katika eneo hilo “kuwakabili” wapiganaji, inasema.

IDF inaendelea kufanya msako zaidi katika eneo hilo, taarifa hiyo ilisema.

Wakati huo huo vyombo vya habari vya Israel vinaripoti kuwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anatarajiwa kuongoza mkutano wa usalama baadaye leo, kufuatia mauaji ya kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar.

Mkutano uunasemekana utafanyika saa saba kwa saa za ndani (11:00 BST) katika makao makuu ya kijeshi ya Kirya mjini Tel Aviv.

Mawaziri wa serikali na maafisa wa usalama watazingatia mpango utakaosaidia kufikia makubaliano ya kuwarejesha nyumbani mateka, ropoti zaidi zinasema.

Gachagua kupambana tena mahakamani saa chache baada ya kuondolewa mamlakani

g

Katika juhudi za dakika za mwisho za kurejesha tena wadhifa wake, Rigathi Gachagua amekwenda mahakamani kumzuia Rais William Ruto kumteua mtu wa kuchukua wadhifa wa Naibu Rais.

Chini ya cheti cha dharura, Rigathi kupitia wakili wake mwandamizi Paul Muite anasisitiza kuwa mashtaka yaliyomkabili mbele ya Bunge la taifa na hatimaye Seneti hayana maana.

Anasema Seneti ilitakiwa na kisheria kufanya kazi kama msuluhishi asiye na upendeleo kwa kuzingatia ikiwa mashtaka kabla ya kuthibitishwa au la.

Asisitiza kuwa ushahidi uliotegemewa kuunda msingi wa mashtaka yake haukuwa wa kutosha kutekeleza mchakato huo na hivyo ulikuwa na kasoro.

Anasema hii ilikwenda kinyume na kiwango kilichowekwa na mahakama ya rufaa katika kesi ya Martin Wambora ambapo iliamuliwa kwamba katika mashtaka ya aina hiyo, madai lazima yawe makubwa na yenye uzito na kwamba mashtaka kama yalivyopangwa lazima yafichue ukiukaji mkubwa wa sheria, mashtraka ambayo Naibu Rais anasema hayakuwepo.

“Madai yasiyo na msingi na ya uongo yametolewa dhidi yangu katika hoja ya mashtaka mbele ya mabunge yote mawili. Itakuwa ni kwa maslahi ya haki kwamba taarifa hizo za uongo zirekebishwe kulingana na masharti ya ibara ya 35 ya katiba,” sehemu ya nyaraka zake ilieleza.

Takriban maseneta 53 kati ya 66 walipiga kura ya kuunga mkono mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake na bunge la kitaifa wiki iliyopita.

Hoja hiyo ya kumng’oa mamlakani iliwasilishwa na Mbunge wa Kibwezi Mwengi Mutuse ambayo baadaye iliishia katika Seneti.

Gachagua ambaye bado yuko hospitalini sasa anataka amri ya kuzuia Seneti kutoangalia azimio lake ambalo liliidhinisha mashtaka yake ya kumuondoa madarakani.

Pia kilichotafutwa ni agizo la kuzuia bunge la taifa kufanya uchunguzi na kuidhinisha uteuzi wa mtu aliyewasilishwa na rais kujaza nafasi hiyo katika ofisi ya Naibu Rais.

Hatahivyo tayari Rais Ruto amemteua Profesa Abraham Kindiki Kithure kuchukua wadhifa wa Naibu Rais.

Gachagua yuko katika hali nzuri kiafya – Daktari

h

Naibu Rais Rigathi Gachagua yuko katika hali nzuri baada ya kulazwa katika hospitali ya Karen Alhamisi alasiri, wakati Bunge la Seneti lilipokuwa likisikiliza kesi ya kumg’oa madarakani.

Akihutubia wanahabari nje ya Hospitali ya Karen, Dan Gikonyo Mkuu wa magonjwa ya moyo, aliripoti kuwa Gachagua alilazwa mwendo wa saa 3 usiku baada ya kupata maumivu makali ya kifua.

“Naibu rais alilazwa hapa mchana wa leo, aliingia saa tatu hivi, aliingia akiwa na maumivu makali ya kifua, anafanyiwa uchunguzi mbalimbali, vipimo vya damu, ECG, mambo yote tunayofanya ili kujua kama kuna hatari yoyote,” alisema Dkt. Gikonyo jana jioni.

Aliongeza, “Kwa sasa yuko imara. Maumivu yanapungua. Msukomo wa damu uko sawa, na bado tunaendelea na uchunguzi.”

Dkt Gikonyo alibainisha kuwa Gachagua atahitaji ufuatiliaji wa karibu kwa saa 48 hadi 72 ili kuhakikisha usalama wake. “Tunalazimika kumuweka ndani kwa takriban masaa 48 hadi 72 ili kuhakikisha kuwa yuko salama,” alisema.

Naibu Rais aliugua muda mchache tu kabla ya kujibu mashahidi katika kesi yake ya kuondolewa madarakani katika Seneti.

Mahakama Kenya yasitisha mchakato wa kuteuliwa Naibu Rais mpya

Maseneta walipiga kura 17 Oktoba 2024 kumuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua baada ya kura ya kumuondoa kupigwa na Bunge la Taifa awali.

Rais William Ruto alikuwa tayari amemteua Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki kuchukua nafasi ya Rigathi Gcahagua kama Naibu Rais/ Picha: Wengine 

Mahakama Kuu nchini Kenya imetoa maagizo ya kusimamisha utekelezwaji wa azimio la Seneti la kuunga mkono kutimuliwa kwa Rigathi Gachagua kama Naibu Rais.

Maseneta walipiga kura Oktoba 17, 2024 kumuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua baada ya Bunge la Taifa kupiga kura ya kumuondoa.

Mahakama Kuu pia imeamrisha kutishwa kwa mchakato wa kuteuliwa kwa mrithi wake hadi Oktoba 24, 2024, wakati kesi hiyo itakapofika mbele ya benchi la majaji watatu walioteuliwa na jaji mkuu Martha Koome.

“Kulingana na uzito ya masuala yaliyoibuka katika ombi lililoletwa nimedhihirisha kuwa suala hili linaibua masuala muhimu ya sheria na umma,” Jaji Chacha Mwita wa Mahakama ya Kilimani alisema.

Ijumaa Oktoba 18, 2024, Bunge la Taifa lilipiga jumla ya kura 236 kumpitisha Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais wa Kenya, baada ya kuteuliwa na Rais William Ruto.

Licha ya amri ya mahakama kusimamisha uteuzi wa Kindiki tayari uteuzi huo umeingia katika Gazeti la Serikali na kuonyesha kuwa amepitishwa na Bunge la Taifa kama Naibu Rais wa Kenya.

Sinwar alipatikana na bunduki na pesa, msemaji wa IDF anasema

g

Haya ndiyo tunayojua kufikia sasa kuhusu kile kilichotokea muda mfupi kuelekea kifo cha kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Daniel Hagari amesema Sinwar aliuawa baada ya vikosi vya Israel kubaini “magaidi” watatu waliokuwa wakikimbia nyumba hadi nyumba katika eneo la Tal El Sultan huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Hagari amewasilisha video ambayo anasema inamuonyesha Sinwar akifikiwa na ndege isiyo na rubani ya IDF, akiwa amejifunika uso na akiwa na jeraha kwenye mkono wake.

Mwanamume huyo, ambaye ameketi kwenye kiti kwenye ghorofa ya pili ya nyumba iliyoharibiwa zaidi kwenye picha, kisha anarusha kile kinachoonekana kuwa fimbo kwenye droni na video inaisha.

Sinwar alipatikana akiwa na bunduki na fedha shekeli 40,000 (£7,700), Hagari anasema.

“Alikuwa akikimbia na tulimuua,” anaongeza.

Jaji azuia dakika za mwisho kunyongwa kwa mwanaume aliyedaiwa kumuua mwanaye Texas

h
Maelezo ya picha,Ombi la dakika za mwisho la Robert Robertson la kuomba msamaha halikufaulu

Jaji wa Texas amezuia kunyongwa kwa mwanaume wa kwanza kuhukumiwa kifo nchini Marekani kwa mashtaka ya mauaji yanayohusiana na maradhi ya majeraha ya ubongo ya mtoto “shaken baby syndrome”, chini ya saa mbili kabla ya hukumu ya kifo kutekelezwa.

Robert Roberson mwenye umri wa miaka 57, alihukumiwa kifo mwaka 2003 kutokana na kifo cha binti yake wa miaka miwili, Nikki Curtis, baada ya uchunguzi wa maiti kuhitimisha kuwa alifariki kwa majeraha kutokana na unyanyasaji.

Roberson, mawakili wake na wafuasi kwa muda mrefu wamekuwa wakisisitiza kuwa mtoto huyo alikufa kutokana na matatizo ya homa ya mapafu.

Waendesha mashtaka, hata hivyo, wamesisitiza kuwa ushahidi mpya haukanushi hoja yao kwamba mtoto huyo alifariki kutokana na majeraha aliyopata kutoka kwa baba yake.

Roberson alipaswa kuuawa saa 12:00 jioni kwa saa za eneo (23:00 GMT) siku ya Alhamisi.

Lakini dakika 90 tu kabla, jaji wa Kaunti ya Travis alitoa amri ya zuio la muda kusimamisha kuendelea, ili Roberson aweze kutoa ushahidi katika kesi katika bunge la jimbo wiki ijayo.

Uamuzi huo ulikuja baada ya jopo la Bunge la Texas kutoa wito usio wa kawaida sana kwa Roberson mwishoni mwa Jumatano, wakitumai kwamba mamlaka ingemlazimu kumpeleka kwenye kikao cha kusikilizwa mnamo tarehe 21 Oktoba.

Idara ya huduma za usalama ya Marekani ina ‘dosari kubwa’ na lazima ibadilishe uongozi, ripoti yanasema

g
Maelezo ya picha,Jopo huru lilipewa jukumu la kuchunguza shambulio la Julai 13 katika mkutano wa hadhara wa Donald Trump

Idara ya huduma za usalama ya Marekani (Secret services) ina “dosari kubwa” ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa haraka au majaribio zaidi ya mauaji kama yale yaliyofanyika mkutano wa hadhara wa Donald Trump yatatokea tena, ripoti iliyofichua kasoro yasema.

Jopo huru lililopewa jukumu la kuchunguza tukio la ufyatuaji risasi wa Julai 13 huko Butler, Pennsylvania, lilitoa matokeo yake siku ya Alhamisi, na kusema shirika hilo limekuwa “la urasimu, lenye kuridhika na halichukui maamuzi”.

Katika ripoti hiyo ya kurasa 52 , ripoti hiyo ilitoa wito wa kufanyiwa marekebisho uongozi wake, na kusema ” kushindwa kwa utekelezaji kazi wake ” kuliwezesha kufanyika kwa mashambulizi dhidi ya mgombea urais wa Republican.

Tayari Idara ya huduma za usalama imekubali kushindwa kwa upande wake, na mkurugenzi wake alijiuzulu wiki chache baada ya kshambulio la risasi dhidi ya Trump.

Katika taarifa siku ya Alhamisi, kaimu mkurugenzi wake Ronald Rowe alisema shirika hilo litachunguza kwa makini ripoti hiyo mpya

MKUSANYIKO WA HABARI DUNIANI.

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, amekariri tena kujitolea kwa nchi yake kwa NATO na kuunga mkono Ukraine katika mkutano wa pamoja na Rais wa Marekani, Joe Biden, uliofanyika Berlin siku ya Ijumaa. Scholz amempongeza Biden kwa kuwaleta pamoja washirika na kutoa msaada muhimu katika wiki za mwanzo baada ya Urusi kuanzisha uvamizi wake kamili dhidi ya Ukraine mwaka 2022.

Kundi la wanamgambo wa Kipalestina, Hamas, limethibitisha kuuawa kwa kiongozi wake Yahya Sinwar, siku moja baada ya Israel kutangaza kifo chake huko Gaza. Sinwar alikuwa mtu anayetafutwa sana na Israel baada ya shambulio la Oktoba 7, 2023, ambalo lilikuwa baya zaidi katika historia ya Israel. Israel ilitangaza kifo cha Sinwar siku ya Alhamisi, ambapo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alielezea kuwa ni “pigo kubwa” kwa kundi hilo ambalo wanajeshi wa Israeli wamekuwa wakipambana nalo Gaza kwa zaidi ya mwaka mmoja. Shambulio la Hamas la Oktoba 7 lilipelekea vifo vya watu 1,206, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya AFP ya takwimu rasmi za Israel ambazo zinajumuisha mateka waliouawa wakiwa kifungoni. Kampeni ya Israel ya kulimaliza Hamas na kuwarejesha mateka waliotekwa na wanamgambo hao imesababisha vifo vya watu 42,500 huko Gaza, wengi wao wakiwa raia, kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya ya eneo linalosimamiwa na Hamas, ambazo Umoja wa Mataifa huziona kuwa ni za kuaminika.

Kalonzo aruhusiwa kuona Gachagua hospitalini, akosoa seneti

    Kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka na wanasiasa wenza nje ya Hospitali ya Karen, Nairobi ambapo walikuwa wameenda kumuona aliyekuwa naibu rais, Rigathi Gachagua.

    KIONGOZI wa Wiper Kalonzo Musyoka amesema ameruhusiwa kumuona Naibu Rais aliyetimuliwa mamlakani Rigathi Gachagua katika hospitali ya Karen.

    Akizungumza muda mfupi baada ya kukutana na kiongozi huyo aliyetimuliwa, Bw Musyoka alisema Gachagua anaendelea kupata nafuu.

    Yeye, kiongozi wa chama cha DAP – Kenya Eugene Wamalwa na Seneta Joe Nyutu walikuwa wanasiasa wa kwanza kumuona Gachagua tangu Almisi usiku, Oktoba 17, 2024.

    “Tuna bahati kwamba baadhi yetu tumeweza kuruhusiwa kumuona. Mimi mwenyewe, Wamalwa na Nyutu tumemwona,” Bw Musyoka alieleza.

    Mungu kuokoa maisha yake

    “Tunamtakia Gachagua afueni ya haraka sana. Tunamshukuru Mungu kwamba ameyaokoa maisha yake.”

    Bw Gachagua aliugua hoja ya kumtimua ikisikilizwa katika Seneti jana usiku (Alhamis).

    Alitarajiwa kujitetea mbele ya maseneta, afya yake ilipodhoofika.

    Maseneta hao walimtimua alipokuwa hospitalini.

    Lakini Bw Kalonzo alikosoa hatua hiyo, haswa baada ya Bw Gachagua kulazwa hospitalini.

    “Sheria ya haki inadai kwamba hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa. Mawakili wa Gachagua watapinga hilo,” alisema Musyoka.

    “Haki itawale katika mahakama zetu,” alisema.

    Bw Wamalwa, kwa upande wake, alitaja Alhamisi usiku seneti ilipoidhinisha kuondolewa kwa Bw Gachagua, kama siku ya huzuni kwa nchi.

    Kiongozi huyo wa DAP-K alimsifu Bw Gachagua kwa kuchagua “kuwakabili wanaomshtaki badala ya kusalimu amri.”

    “Iwapo tulitilia shaka kuwa bunge limetekwa na serikali, jana usiku ulikuwa ushahidi,” Bw Wamalwa alisema.

    All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


    Discover more from cantonadigital

    Subscribe to get the latest posts sent to your email.

    Leave a comment