Israeli kujibu shambulio la Iran kulingana na masilahi yake: Benjamin Netanyahu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu katika taarifa yake imesema itaangazia ushauri wa Marekani lakini itajibu shambulio la kombora la Iran kulingana na masilahi ya taifa lake.

Israel imeapa kujibu mashambulio ya Iran kwa mujibu wa masilahi ya nchi japokuwa itazingatia mapendekezo ya Marekani.
Israel imeapa kujibu mashambulio ya Iran kwa mujibu wa masilahi ya nchi japokuwa itazingatia mapendekezo ya Marekani. © Eduardo Munoz / Reuters

Rais wa Marekani Joe Biden ameionya Israeli dhidi ya kushambulia vinuu vya nyukilia vya Iran au hata vituo vyake vya mafuta kama njia moja ya kuzuia kuongezeka kwa mzozo katika eneo la mashariki ya kati.

Wataalam wa masuala ya kuichumi wameonya kwamba wasiwasi iliopo kati ya Iran na Israeli huenda ikichangia kuongezeka kwa bei ya mafuta duniani iwapo Israeli itashambulia vituo vya mafuta ya Iran.

“Tunasikiliza mapendekezo ya Marekani ila tutafanya uamuzi wetu wa mwisho wenyewe kwa mujibu wa masilahi ya taifa letu,” imesema ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli.

Rais Joe Biden wa Marekani amekuwa akishinikiza Israeli kuepuka mzozo wa moja kwa moja na Iran haswa kwa kushambulia vinuu vyake vya nyukilia.
Rais Joe Biden wa Marekani amekuwa akishinikiza Israeli kuepuka mzozo wa moja kwa moja na Iran haswa kwa kushambulia vinuu vyake vya nyukilia. AP – Manuel Balce Ceneta

Taarifa hiyo imekuja baada ya ripoti ya jarida la The Washington Post la nchini Marekani, ilioeleza kwamba Netanyahu alikuwa ameihakikishia White House kwamba mashambulio yoyote ya kulipiza kisasi yatalenga tu maeneo ya kijeshi peke.

Ripoti ya The Wall Street Journal, nayo pia ikiwanuku maofisa kutoka nchini Marekani ilisema kwamba hakikisho hilo liliafikiwa kwa njia ya simu wiki iliopita kati ya Netanyahu na Biden.

Aidha inaripotiwa kwamba hakikisho hilo la Israeli pia liliafikiwa katika mazungumzo kati ya Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na mwenzake wa Israeli, Yoav Gallant.

Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israeli na waziri wake wa mambo ya usalama Yoav Gallant.
Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israeli na waziri wake wa mambo ya usalama Yoav Gallant. via REUTERS – Pool

Iran ilitekeleza karibia mashambulio 200 ya roketi kuekekea nchini Israeli tarehe moja ya mwezi Oktoba kujibu shambulio la Israeli katika mji wa Beirut ambalo lilisababisha kifo cha kiongozi wa wapiganaji wa Hezbollah Hassan Nasrallah na afisa mwengine wa usalama wa Iran Jenerali Abbas Nilforoushan.

Israel kwa upande wake imeapa kujibu mashambulio ya Iran, Waziri wa ulinzi wa Israeli Yoav Gallant akisema kwamba jibu la nchi yake litakuwa baya na la kushtukiza.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment