Mataifa ya India na Canada yawafukuza wanadiplomasia wake

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mataifa ya India na Canada yamewafukuza wanadiplomasia wao, kutokana mzozo unaoendelea ambapo canada inatuhumu India kwa kutekelza mauwaji ya Hardeep Singh Nijjar, kiongozi wa vuguvugu linaloshinikiza kujetenga kwa Sikh, katika ardhi ya canada.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na mwenzake wa Canada Justin Trudeau.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na mwenzake wa Canada Justin Trudeau. AP – Sean Kilpatrick

Waziri mkuu wa CanadaJustin Trudeau amesema canada imelazimika kuwatimua wanadiplomasia wa India nchini mwake baada ya taarifa kuonesha kuwa mawakala wa India walihusika moja kwa moja na kifo cha Hardeep Singh Nijjar.

Polisi wa Canada pia wanawatuhumu mawakala wa India kwa kuhusika na visa vya utekaji wa wanachama wa vuguvugu la Sikh, wanaoishi nchini Canada.

Hata hivyo India imekanusha madai hayo ya Canada na Kusema waziri mkuu Justin Trudeu anatafuta ushawishi wa kisiasa kupitia vuguvugu la Sikh.

India imekuwa ikituhumu kundi la Sekh kwa kujihusisha na visa vya kihalifu na kulitaja kuwa kundi la kigaidi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment