“The Price of Being At The Top is to always Become The Topic”

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja ya kitu kinachoweza kukuchelewesha kwenye mafanikio yako ni pale unapochelewa kujikubali.

Kuna watu wengi sana ambao wamepoteza ukubwa wao kwa sababu ya kusubiria kukubaliwa.

Ngoja nikukumbushe, bila kujali wewe ni Nani na unafanya nini, lazima kuna watu watakuwa kinyume nawe.

Elbert Hubbard aliwahi kusema “There is only one way to avoid criticism: do nothing, say nothing, and be nothing.”

Yaani, Kama hautaki kukosolewa basi usifanye chochote, usiseme chochote wala usiwe chochote.

Mentor wangu aliniambia, “The Price of Being At The Top is to always Become The Topic”,. Yaani, moja ya gharama ya kuwa juu ni kujikuta ukijadiliwa kila siku, aidha kwa namna unayopenda au la.

Mbaya zaidi ni kuwa, wengi watakaokuongela vibaya ni wale ambao hawakujui na hauna ugomvi nao.

Ndio maisha yalivyo, jifunze kufanya bila kuogopa watakachosema. Una hatima kubwa, usiruhusu izuiliwe na maneno ya watu. Leo dhamiria kufanya unachokiamini bila kujali wanaosema kinyume nawe.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment