Nigeria kutocheza mechi yao ya kufuzu kwa mashindano ya Afcon dhidi ya Libya

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirikisho la mpira wa miguu nchini Nigeria (NFF) limesema litawarejesha nchini humo wachezaji wa timu ya taifa kutokana na madai ya kushugulikiwa vibaya wakati wakiwa nchini Libya kuelekea mechi ya kufuzu kwa michuano ya Afcon 2025.

Mashabiki wa Nigeria baada ya timu yao kuishinda Cameroon 2-0 na kutinga hatua ya nane bora katika mechi za  Afcon 2023.
Mashabiki wa Nigeria baada ya timu yao kuishinda Cameroon 2-0 na kutinga hatua ya nane bora katika mechi za Afcon 2023. REUTERS – LUC GNAGO

Kwa mujibu wa afisa wa mawasiliano wa shirikisho hilo Ademola Olajire, wachezaji wameamua kwamba hawatacheza tena mechi yao dhidi ya Libya na kwamba mipango ya kuwarejesha nyumbani inaendelea.

Tayari Nigeria imeandikia CAF kulalamikia tuhuma za wachezaji wake kupewa mapokezi mabaya nchini Libya.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria walishikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa Libya kwa zaidi ya saa 15 tangu kutua kwa ndege yao siku ya Jumapili.

Ubalozi wa Nigeria nchini Libya umeripotiwa kushindwa kuingilia kati suala hilo kwa sababu wanahitaji kupata idhini ya kufanya hivyo kutoka kwa serikali ya Libya.

4pm | Kenya vs Cameroon

5pm | Gambia vs Madagascar

7pm | Zimbabwe vs Namibia

7pm | Liberia vs Equatorial Guinea

7pm | Togo vs Algeria

10pm | Eswatini vs Mozambique

Ratiba ya mechi za leo Jumatatu kufuzu kwa Afcon 2025.
Ratiba ya mechi za leo Jumatatu kufuzu kwa Afcon 2025.
Ratiba ya mechi za leo Jumatatu kufuzu kwa Afcon 2025. © CAF

Nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria William Troost-Ekong amethibitisha kwamba hawatacheza mechi hiyo na kwamba hawatakubali usafiri wa basi wa saa tatu kutoka katika eneo la Al-Abraq hadi Benina, eneo ambapo mechi hiyo ilikuwa imeratibiwa kuchezwa siku ya Jumanne kutokana na masuala ya kiusalama.

Siku ya Ijumaa, Nigeria ilipata ushindi wa bao moja bila ya jibu dhidi ya Libya kusini mwa mji wa Uyo nchini Nigeria.

Wanaoongoza kundi D wakiwa na alama saba baada ya kucheza mechi tatu wakati Libya wakiwa wa mwisho na alama moja.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment