UN yataka kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza na nchini Lebanon

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Umoja wa Mataifa umesisitizia wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon na katika Ukanda wa Gaza kama njia moja ya kuzuia kutokea kwa mzozo zaidi mashariki ya kati, hatua ambayo UN inasema itaadhiri dunia nzima.

Mkuu wa shirika UNHCR  Filippo Grandi
Mkuu wa shirika UNHCR Filippo Grandi AFP – BRYAN R. SMITH

Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa shirika la wakimbizi UNHCR unaofanyika mjini Geneva, Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi ameeleza kwamba mapigano yanatakiwa kusitishwa mara moja.

Wito wake umekuja wakati huu Israeli ikiripotiwa kuendelea kutekeleza mashambulio inayosema yanawalenga wapiganaji wa Hezbollah.

Israeli inasema itaendelea kuwatafuta wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon
Israeli inasema itaendelea kuwatafuta wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon © Mohammad Zaatari / AP

Zaidi ya watu 1,300 wameripotiwa kuuawa na mamilioni ya wengine wakiwa wamepoteza makazi yao tangu mwezi Septemba kwa mujibu wa maofisa wa afya kutoka nchini Lebanon.

Hezbollah ilianza kutekeleza mashambulio kaskazini mwa Israeli mwaka mmoja uliopita katika kile ilisema inawaunga mkono wapiganaji wa Hamas kufuatia shambulio la tarehe 7 ya mwezi Oktoba, shambulio ambalo hata hivyo limesababisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Pande hasimu katika mzozo wa Gaza na Lebanon zimekuwa zikitakiwa kusitisha mapigano.
Pande hasimu katika mzozo wa Gaza na Lebanon zimekuwa zikitakiwa kusitisha mapigano. © Mahmud HAMS / AFP

Makabiliano ya karibia kila siku yamesababisha makumi kwa maelfu ya watu kupoteza makazi yao kutoka pande zote mbili za mpaka hata kabla ya mapigano kuongezeka mwezi uliopita.

Mwezi uliopita, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliapa kulitokomeza kundi la Hezbollah ilikuwaruhusu raia wa Israeli waliopoteza makazi yao kurejea nyumbani.

Mkuu huyo UNHCR ambaye alizuru nchi ya Lebanon na Syria amelaani pia mashambulio dhidi ya wafanyikazi wa mashirika ya misaada.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment