Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mapigano kati ya jamii kusini mashariki mwa Kenya yamesababisha vifo vya takriban watu 18 katika muda wa wiki mbili zilizopita, polisi imetangaza siku ya Jumamosi, huku ikiongeza idadi ya maafisa wa polisi katika maeneo husika.

Siku ya Ijumaa, Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki alitangaza maeneo 12 katika Kaunti ya Tana River kuwa “hatari na yenye matatizo”, ukiwemo mji wa Bura ambako mapigano yalikuwa makali zaidi.
Mkuu wa polisi nchini Kenya Douglas Kanja amewataka wakaazi kusalimisha silaha zao ili kuepusha kuongezeka kwa ghasia.
Matatizo yalianza pale serikali ya kaunti ilipotoa ardhi kwa ajili ya kuwahifadhi watu waliokimbia makazi yao kutokana na mafuriko pembezoi mwa Mto Tana, mto mrefu zaidi nchini Kenya.
Wafugaji wa eneo hilo waliandamana, wakisisitiza kwamba malisho yao yatakaliwa na waliohamishwa.
“Tumepoteza watu 18 tangu mwezi uliopita na usalama umeimarishwa ili kuzuia vifo zaidi,” amesema afisa mkuu wa polisi katika Kaunti ya Tana River, akizungumza kwa sharti la kutotajwa. “Lakini kwa sasa hali ni ya wasiwasi kwa sababu watu hawataki kusalimisha silaha zao.”
Siku ya Jumamosi, mkurugenzi wa uchunguzi wa jinai Mohamed Amin ametangaza kukamatwa kwa viongozi wawili wa eneo hilo, gavana wa kaunti Dhadho Godhana na mbunge Said Hiribae, kwa kutojibu wito wa polisi kuhusu ghasia hizo.
Nyumba kadhaa zimeharibiwa na idadi isiyojulikana ya watu walikimbia eneo hilo.
“Hatujisikii salama tena hapa, mashambulizi mengine yamefanyika wakati wa mchana Serikali inapaswa kutafuta suluhu la kudumu la mgogoro huu,” amesema Mohamed Ibrahim, mkazi wa Bura, Mohamed Ibrahim.
“Yote ni kwa sababu ya ardhi. Wafugaji hawataki watu hawa ambao wamehamishiwa hapa, na hilo ndilo lililozua mapigano,” ameongeza mkazi mwingine.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.