Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
China imeanzisha mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa cha Tiawan, wizara ya ulinzi ya China ikisema ni onya kwa vikosi vya Taiwan.

Mazoezi hayo ya kijishi yaliopewa jina Sword-2024B, yanafanyia majaribio uwezo wa vikosi vya ndani vya China, Beijing ikisema mazoezi hayo yatafanyika eneo la Kaskazini na mashariki mwa kisiwa cha Taiwan bila kutoa taarifa ni lini mazoezi hayo yatakamilika.
Taiwan kwa upande mwingine imesema imetuma vikosi vyake kukabiliana na uvamizi wowote wa China.
China imekuwa ikifanya mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa hicho huru cha Taiwan, ambacho imesisitiza kuwa ni sehemu ya himaya yake, kwa kutuma ndege za kijeshi pamoja na meli.
Hata hivyo China haijawahi weka wazi iwapo inaweza au la kutumia nguvu kuchukuwa udhibiti wa kisiwa cha Taiwan.
Marekani mshirika wa karibu wa Taiwan, ameonya China dhidi ya kuvamia Taiwan
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.