Zaidi ya wanawake milioni 79 waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia Kusini mwa Jangwa la Sahara

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Zaidi ya wanawake na wasichana milioni 79 wmekuwa waathiriwa wa ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia Kusini mwa Jangwa la Sahara, moja ya kanda za ulimwengu zilizoathiriwa zaidi na ukatili huu, kulingana na data mpya iliyochapishwa siku ya Alhamisi na UNICEF.

Watu waliokimbia makazi yao wanasubiri UNICEF kuwapa chakula huko Munigi, DRC, Desemba 5, 2022.
Watu waliokimbia makazi yao wanasubiri UNICEF kuwapa chakula huko Munigi, DRC, Desemba 5, 2022. © AFP

ulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, mwanamke mmoja kati ya watano amekuwa mwathirika wa unyanyasaji wa kijinsia au ubakaji kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 katika eneo hili la dunia.

Duniani, jumla ya wasichana na wanawake milioni 370 wamefanyiwa ukatili wa kijinsia, UNICEF inabainisha.

“Unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto ni doa kwenye dhamiri zetu za maadili,” Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Catherine Russell amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Hii ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuchapisha takwimu kama hizo, ambazo hukusanya data za kitaifa na programu za uchunguzi wa kimataifa kati ya mwaka 2010 na 2022, Claudia Cappa, mtakwimu mkuu wa masuala ya idadi katika shirika hilo, anmeliambia shirika lahabari la AFP, hata kama kunabaki mapungufu ya data, na vile vile makadirio katika baadhi ya nchi.

“Tunajua mipaka, lakini pia tulitaka hatimaye kutoa uonekano wa tatizo hili kupitia takwimu,” anasema.

“Inatisha,” anasema Nankali Maksud, mtaalamu wa ukatili dhidi ya watoto katika shirika la UNICEF, aliyeko Nairobi.

“Tunashuhudia unyanyasaji wa kutisha wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro, ambapo ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia mara nyingi hutumiwa kama silaha za vita,” anaongeza Russell.

Mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini Sudan yametahadharisha haswa juu ya hatari ambazo mzozo unaoendelea kwa wasichana na wanawake.

Kulingana na shirika la Human Rights Watch (HRW), ni vigumu pia kutathmini ukubwa wa unyanyasaji wa kijinsia, kutokana na waathiriwa kusita kutoa ushahidi, kwa hofu ya kunyanyapaliwa

Kusambaza :

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment