Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekutana na Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, siku ya Ijumaa Oktoba 11, 2024 katika hadhara yake ya pili ya faragha huko Vatican tangu mashambulizi ya Urusi.

Baada ya mkutano wa kwanza mwezi Juni mwaka jana, wakati wa mkutano wa kilele wa G7 nchini Italia, ambapo walialikwa na Italia iliyokuwa ikishikilia zamu ya urais wa kundi hilo, hadhira hii mpya ilikuwa fursa ya kuhutubia ujumbe wa upatanishi wa Vatican ndani ya mfumo wa vita vya Ukraine. Ujumbe wakati mwingine umeonekana na Ukraine kama utata.
Ujumbe tata kwa Papa Francis na makao makuu ya Kanisa katoliki duniani katika toleo hili la Ukraine. Wakati mazungumzo na viongozi wa Urusi yamekatizwa, Vatican inahamasishwa zaidi juu ya upatanishi kuhusu kubadilishana wafungwa kati ya Urusi na Ukraine na kuwarejesha makwao watoto wa Ukraine wanaozuiliwa na Urusi tangu kuanza kwa vita.
“Swali la kurejea nyumbani kwa wenzetu lilikuwa kiini cha mkutano wangu na Papa Francis @Pontifex. Tunategemea msaada wa Vatican kusaidia kuwarejesha makwao Waukraine waliotekwa na Urusi,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameandika saa sita mchana mnamo kwenye mtandao wa X.
Juhudi za kidiplomasia kutoka Vatican
Tangu mashambulizi ya Urusi yaanze mnamo mwaka 2022, Vatican imeongeza juhudi za kidiplomasia kufikia usitishaji wa mapigano na kuharakisha mchakato wa kuwaachilia wafungwa, pamoja na watoto. Mnamo Mei 12, Papa Francis alisihi “mabadilishano ya jumla ya wafungwa wote kati ya Urusi na Ukraine,” akibainisha uwepo wa Vaticani kuunga mkono juhudi hizi. Papa pia alitangaza kuwa na jukumu la upatanishi, na hivyo kuwezesha kuachiliwa kwa wafungwa 300 wa Ukraine mnamo wezi wa Septemba 2022.
“Amani ya haki na utulivu nchini”
Mkutano huu wa faragha wa dakika 35 ni hadhira ya pili iliyotolewa na papa kwa Zelensky huko Vatican tangu kuanza kwa vita. Wakati wa mazungumeo yao ya ana kwa ana, Zelensky na papa walijadili hasa masuala ya kibinadamu, wakati Vatican imesema katika taarifa kwamba majadiliano pia yalilenga “njia za kukomesha, na kurejesha amani na utulivu nchini. . » Dhana, ambayo mara nyingi imekuwa ikieleweka vibaya na Vatican, kulingana na Kyiv.
Mwezi Machi mwaka huu, Francis alizua mzozo wa kidiplomasia na Kyiv baada ya kuwaalika Waukraine “kuinua bendera nyeupe na kujadili”. Mwishoni mwa mwezi wa Agosti, pia alionyesha wasiwasi wake kwa uhuru wa kuabudu nchini Ukraine, baada ya Kyiv kupiga marufuku Kanisa la Othodox la Ukraine lenye uhusiano na Moscow.
Kubadilishana kwa zawadi za kiishara kati ya Zelensky na Papa
Mkutano umemalizika kwa kubadilishana zawadi za kiishara. Papa Francis amempa Zelensky sanamu ya shaba, ikiambatana na maneno: “Amani ni ua dhaifu.” Kwa upande wake, rais wa Ukraine ametoa mchoro unaoonyesha mauaji ya Boucha, tukio la kutisha la vita vya Ukraine.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.