Mkutano wa ASEAN: Vita vya maneneo vyaibuka kati ya Urusi na Marekani.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mkutano wa kilele wa ASEAN, unaoleta pamoja nchi za Kusini-mashariki mwa Asia, umehitimishwa leo Ijumaa, Oktoba 11 huko Laos, huko Vientiane. Kama kawaida, kambi hii ya nchi kumi ilialika washirika wake wakuu: Marekani, China, India, Japani na Urusi. Ilikuwa ni fursa adimu ya kuleta pamoja mamlaka zenye maslahi tofauti katika chumba kimoja, katika muktadha wa mvutano kati ya Washington, Moscow na Beijing.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa 44 na 45 wa Umoja wa Mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia (ASEAN) mjini Vientiane, Laos, Oktoba 11 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa 44 na 45 wa Umoja wa Mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia (ASEAN) mjini Vientiane, Laos, Oktoba 11 2024. © TANG CHHIN SOTHY / REUTERS

Vita vya maneno kati ya Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, na Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, vilikuwa vikisubiriwa kwa hamu. Kwa hakika, wawili hao hawadumii mawasiliano ya moja kwa moja, ikimaanisha kwamba ni kupitia hotuba za kutupiana maneno ndipo huelewana kati yao.

Antony Blinkenamehusisha uhusiano kati ya mashambulizi ya Urusi kwa Ukraine na malengo ya China kwa Taiwan, ambapo luteka za majini za hivi karibuni zinawatia wasiwasi majirani zake wa Asia. “Nchi zote zilizoitikiwa mkutano huu” Blinken amesema, “zimeweka wazi kwamba uchokozi wa Ukraine lazima ukome … pia kwa sababu wanajua kwamba ikiwa nchi itaruhusiwa kuchukua hatua bila kuadhibiwa, ni ishara kwa washambuliaji wanaowezekana ulimwenguni kote. “

Lavrov ajibu tuhuma

Kwa upande wake, Sergei Lavrov amebainisha kwamba hatua ya Marekani katika Asia ya Kusini-Mashariki imekuwa “ya uharibifu”, akiishutumu Washington hasa kwa kushinikiza Japani kuelekea “kijeshi” kwa mantiki ya makundi ambayo hubeba, “hatari za mapambano”. Hii inarejelea wazo la Waziri Mkuu mpya wa Japani, Shigeru Ishiba, kuunda muungano wa kijeshi wa kikanda unaozingatia NATO.

Kumbuka kwamba kando ya mkutano huu wa ASEAN, Japani na Korea Kusini zimeimarisha ushirikiano wao wa ulinzi, kwa kuzingatia maelewano ya kijeshi kati ya Korea Kaskazini na Urusi.

Uhusiano kati ya Tokyo na Seoul umekuwa ukidhoofishwa kwa muda mrefu na mizozo ya kihistoria tangu mwaka 2023 na kuongezeka kwa vitisho vya nyuklia vya China na Korea Kaskazini.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment