Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Baada ya gereza la Makala huko Kinshasa, wafungwa 270 kutoka gereza la Kasapa huko Lubumbashi wameachiliwa kwa dhamana tangu siku ya Jumatatu Oktoba 7, 2024. Waziri wa Sheria wa Kongo, Constant Mutamba, akiwa katika zira ya kikazi huko Haut Katanga, yeye mwenyewe aliendesha operesheni hii ambayo inalenga kupunguza msongamano katika magereza nchini. Gereza la Kasapa lililojengwa wakati wa ukoloni likiwa na uwezo wa kuchukua wafungwa 680, lina wafungwa 2,790.

Samy Kapanga amefanya miaka mitatu tu katika gereza kuu la Kasapa huko Lubumbashi bila kuhukumiwa. Yeye ni mmoja wa wafungwa 40 wagonjwa ambao wote waliachiliwa siku ya Jumatatu, Oktoba 7. Kwa akizungumza kwa uoga, Samy anarejelea mazingira ya kukamatwa kwake: “Nilikamatwa saa kumi na mbili jioni kwa sababu nilikuwa nikitembea bila hati za utambulisho. Nilipelekwa jela na huko waliniomba dola 300. Kwa vile sikuwa nazo waliniingiza gerezani. “
Wafungwa wengine 230 pia waliachiliwa. Wengine walizuiliwa kwa makosa madogo, wengine tayari walikuwa wametumikia zaidi ya nusu ya kifungo chao. Akiwa na tikiti yake ya mkononi ya kumruhusu kuondoka jela, Moïse Ngandu, dereva, hakutarajia hali hiyo. “Nilihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa sababu niligonga watu wawili ambao walijeruhiwa. Kisha waliniongeza mwaka mmoja. Huko, nilikuwa nimebakiza miezi tisa. Namshukuru Mungu Mwema. Hatukuweza kufikiria kwamba waziri angekuja yeye mwenyewe kutekeleza kuachiliwa kwetu. “
Waziri wa Sheria, Constant Mutamba, aliwataka viongozi wa ofisi za mashitaka za kiraia na kijeshi kutembelea magereza mara kwa mara ili kufuatilia mafaili ya wafungwa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.