Afrika Leo Jioni-04 Oktoba 2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja …………

Muhtasari

  • Waziri wa mambo ya nje wa Iran azuru Beirut huku mashambulizi yakiendelea
  • WHO yaidhinisha kipimo cha kwanza cha mpox kwa utambuzi wa haraka
  • Kiongozi mkuu wa Iran atetea shambulio dhidi ya Israel katika hotuba adimu ya umma
  • Mwanamume apatikana na hatia ya unyanyasaji dhidi ya watoto
  • India yasema kuharamisha ubakaji ndani ya ndoa ni ‘adhabu kali zaidi’
  • Shambulio la genge la Haiti lasababisha vifo vya takriban watu 20
  • Tazama: Milipuko ilipotokea karibu na uwanja wa ndege wa Beirut
  • Melania Trump awa mke wa rais wa hivi karibuni zaidi kutoka Republican kuunga mkono utoaji mimba
  • Zelensky amfuta kazi mkuu wa jeshi la anga la Ukraine
  • Takriban watu 78 wafariki baada ya feri kuzama katika ziwa DRC
  • Biden asema Marekani inajadili uwezekano wa mashambulizi ya Israel dhidi ya vituo vya mafuta vya Iran
  • Milipuko mikubwa yashuhudiwa Beirut baada ya mashambulizi mapya ya anga ya Israel

Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili hujambo na karibu katika Afrika Leo Jioni Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran azuru Beirut huku mashambulizi yakiendelea

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi ametua Beirut – saa chache tu baada ya mfululizo wa mashambulizi makubwa ya anga kusini mwa mji huo.

Hii ni ziara ya kwanza rasmi na iliyofanywa na mwanasiasa wa ngazi ya juu wa Iran tangu Israel kumuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah.

Baada ya kuwasili mjini humo alisema Iran inaunga mkono juhudi za kusitisha mapigano nchini Lebanon ikiwa Hezbollah itaiunga mkono – na ikiwa itaambatana na usitishaji mapigano huko Gaza.

Araghchi yuko Beirut wakati ambapo hakuna kinachoonekana kupendelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wengine hapa wanailaumu Iran kwa “kuweka Hezbollah chini ya shinikizo” kushiriki katika vita vya Hamas na Israel baada ya Oktoba 7, lakini haikutoa msaada ambao kundi hilo lilihitaji.

Ingawa shambulio la hivi majuzi la Iran liliibua msisimko mingoni mwa wafuasi wa Tehran na Hezbollah, hali hiyo ilikuwa ya muda na sasa tena kuna ukosoaji katika vyombo vya habari na mitaani.

Kwa upande mwingine, vyama vinavyopinga Hizbullah vinaona hii kama vita ambayo Iran ilileta kwao.

Wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati, Araghchi anasema: “Iran itaanzisha kampeni ya kidiplomasia kusaidia Lebanon”, vyombo vya habari vya Lebanon vinaripoti.

Lakini kwa kampeni kama hiyo, mtu anapaswa kuwa na kadi mkononi za kucheza. Kwa miaka kadhaa kadi za Irani zilikuwa vikundi vya kijeshi vya washirika kama Hezbollah.

Kwa sasa, ni vigumu kubaini jinsi kampeni hiyo itakavyofanywa wakati Iran yenyewe inakabiliwa na tishio la kuwa shabaha katika vita hivi.

Hotuba adimu kutoka kwa kiongozi mkuu wa Iran – na matukio mengine

xx

Tumekuwa tukifuatilia matukio tofauti katika eneo la Mashariki ya Kati nakukufahamisha moja kwa moja mambo yanayojiri – haya hapa ni baadhi ya matukio hayo kwa ufupi,

Barabara kuu kati ya Lebanon na Syria imekumbwa na shambulizi la anga la Israel. Kivuko cha Masnaa kilitumiwa na watu waliokimbia Lebanon – baadhi yao wamepigwa picha wakitembea karibi na kivuko hicho asubuhi ya leo, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limethibitisha kushambulia handaki la chini la ardhi lililokuwa likitumiwa na Hezbollah kuhifadhi na kuhamisha silaha.

Mashambulizi ya anga yaliendelea usiku kucha nchini Lebanon, ikiwa ni pamoja na karibu na uwanja wa ndege wa Beirut. Takriban watu 37 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita, Lebanon ilisema asubuhi ya leo. Kando, waziri wa mambo ya nje wa Iran alitua katika uwanja wa ndege leo asubuhi kwa ziara, kulingana na vyombo vya habari vya Lebanon

Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Marekani vimewanukuu maafisa wa Israel wakisema kuwa binamu wa kiongozi wa zamani wa Hezbollah Hassan Nasrallah, Hashem Safieddine, anasadikiwa kuwa lengo la shambulio la jana usiku. Safieddine anatarajiwa kuwa mrithi Nasrallah. Hezbollah bado haijatoa taarifa yoyote kuhusiana na hilo,

Roketi zimeendelea kurushwa nchini Israel kutoka Lebanon, Israel inasema – huku IDF ikisema kundi hilo lilirusha roketi 20 leo asubuhi. Nyingi zilizuiliwa, linasema, na zingine walianguka katika eneo wazi.

Ving’ora vilisikika kusini mwa Israeli kwa mara ya kwanza ndani ya miezi miwili, IDF pia ilisema.

WHO yaidhinisha kipimo cha kwanza cha mpox kwa utambuzi wa haraka

XX

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeidhinisha kipimo cha kwanza cha uchunguzi wa ugonjwa wa mpox ambapo matokeo yake yanaweza kujulikana mara moja, likisema kuwa hatua hiyo muhimu itasaidia kudhibiti ongezeko la maambukizi ya virusi hivyo hatari duniani.

Kipimo kipya cha PCR huwezesha ugunduzi wa DNA ya mpox iliyochukuliwa kutoka kwenye swabs za vidonda vya ngozi.

Kwa sasa, sampuli zinapaswa kutumwa kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi na mgonjwa na madaktari wanapaswa kusubiri siku kwa matokeo.

Uwezo mdogo wa kupima na ucheleweshaji wa kuthibitisha kesi unaendelea kuwa changamoto barani Afrika – na kuzidisha kuenea kwa mpox ambayo hapo awali ilijulikana kama monkeypox.

Kati ya zaidi watu 30,000 wanaoshukiwa kuwa na maambukizi ya Mpox barani Afrika mwaka huu, ni takriban 40% wamethibitishwa kufanyiwa uchunguzi, WHO ilisema.

Khamenei asema shambulio dhidi ya Israel lilikuwa ‘adhabu ndogo’

Ayatollah Ali Khamenei
Maelezo ya picha,Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei

Khamenei amesifia shambulio la siku ya Jumanne la nchi hiyo dhidi Israel, na kulitaja kuwa “halali” kabisa.

Anasema walichokifanya ni “adhabu ndogo” kwa Israel kupinga “uhalifu wao wa kustaajabisha”.

Anaita Israel kuwa utawala wa “kinyama” na Marekani “mbwa kichaa” katika eneo hilo.

Anasema Jamhuri ya Kiislamu itatekeleza “majukumu yoyote yanayohusiana” dhidi ya Israel kwa “nguvu na ushujaa”.

Anasisitiza kwamba Iran “haitasita” wala “kutetereka” linapokuja suala la Israel.

Katika sehemu ya kwanza ya hotuba yake aliyoitoa kwa lugha ya Kiajemi, pia alisisitiza “umoja” wa Waislamu duniani kote kwa kuzingatia kanuni za kitabu kitakatifu cha Kiislamu, Quran.

Alisema adui wa Iran ni sawa na adui wa taifa la Palestina, Lebanon na mataifa mengine ya Kiislamu.

Kiongozi mkuu wa Iran atetea shambulio dhidi ya Israel katika hotuba adimu ya umma

Kiongozi Mkuu wa Irani Ayatollah Ali Khamenei, katika hali isiyo ya kawaida, hivi sasa anatoa hotuba katika Msikiti wa Imam Khomeini Mosalla mjini Tehran.

Katika sehemu ya kwanza ya hotuba yake aliyoitoa kwa lugha ya Kiajemi, alisisitiza “umoja” wa Waislamu duniani kote kwa kuzingatia kanuni za kitabu kitakatifu cha Kiislamu, Quran.

Alisema adui wa Iran ni sawa na adui wa taifa la Palestina, Lebanon na mataifa mengine ya Kiislamu.

Khamenei anashikilia rasmi cheo cha imamu wa swala ya Ijumaa ya Tehran, lakini kwa kawaida huwapa mahubiri kundi la wasaidizi wanaomzunguka.

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa vitatoa sehemu ya hotuba yake kwa Kiarabu, akiwahutubia Walebanon na Wapalestina.

Mahubiri ya kiongozi huyo yanakuja siku tatu kabla ya maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel ambayo yalianzisha vita vya sasa vya kikanda.

Pia inakuja siku tatu baada ya Iran kufanya mashambulizi ya kombora dhidi ya Israel kulipiza kisasi mauaji ya Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah na kamanda wa IRGC (Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu) Abbas Nilforoushan, pamoja na yale ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran mwezi Julai.

Mara ya mwisho Khamenei alisalisha sala ya Ijumaa ilikuwa muda mfupi baada ya Jenerali Qasem Soleimani wa Iran kufariki katika shambulio la ndege isiyo na rubani ya Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad mwaka 2020 na baadae shambulio la Iran katika kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq.

India yasema kuharamisha ubakaji ndani ya ndoa ni ‘adhabu kali zaidi’

Mahakama ya Juu inasikiliza maombi ya kutaka kurekebisha sheria inayosema mwanamume hawezi kufunguliwa mashtaka kwa ubakaji ndani ya ndoa.
Maelezo ya picha,Mahakama ya Juu inasikiliza maombi ya kutaka sheria inayosema mwanamume hawezi kufunguliwa mashtaka kwa ubakaji ndani ya ndoa kufanyiwa marekebisho.

Serikali ya India imepinga maombi ya kutaka kuharamishwa kwa ubakaji katika ndoa katika mahakama kuu, ikisema kuwa itakuwa “kali kupita kiasi”.

Wizara ya mambo ya ndani iliiambia Mahakama ya Juu kwamba “mwanamume hana haki ya kimsingi” ya kulazimisha ngono kwa mke wake, lakini kulikuwa na sheria za kutosha kuwalinda wanawake walioolewa dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.

Mahakama kuu inasikiliza maombi ya kutaka kufanyia marekebisho sheria ya kale ya Uingereza inayosema mwanamume hawezi kufunguliwa mashtaka kwa ubakaji ndani ya ndoa.

Unyanyasaji ndani ya ndoa umekithiri nchini India – kulingana na utafiti wa hivi karibuni wa serikali, mmoja kati ya wanawake 25 wamekumbana na ukatili wa kijinsia kutoka kwa waume zao.

Ubakaji katika ndoa umepigwa marufuku katika nchi zaidi ya 100, ikiwa ni pamoja na Uingereza ambayo iliifanya kuwa uhalifu mwaka 1991.

Lakini India ibado ni miongoni mwa makumi ya nchi ikiwa ni pamoja na Pakistan, Afghanistan na Saudi Arabia – ambapo sheria inasalia kwenye vitabu vya sheria.

Shambulio la genge la Haiti lasababisha vifo vya takriban watu 20

g
Maelezo ya picha,Watu walionekana wakikimbia vurugu kwa pikipiki na kwa miguu

Takriban watu 20 wakiwemo watoto wameuawa baada ya genge lenye silaha kushambulia mji mdogo nchini Haiti.

Wengine 50 wamejeruhiwa wakati washiriki wa genge la Gran Grif walipovamia Pont-Sondé katika eneo la kati la Artibonite lililopo takriban kilomita 71 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Port-au-Prince.

Video zinaonyesha makundi ya watu wakikimbia ghasia kwa pikipiki na kwa miguu.

Mwendesha mashtaka wa serikali amelielezea shambulio hilo kama “mauaji,” limeripoti shirika la habari la Associated Press.

Magenge yenye silaha yamechukua udhibiti wa sehemu kubwa za Haiti na ujumbe wa polisi unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, unaoongozwa na maafisa kutoka Kenya, ulianza mwezi Juni katika jaribio la kurejesha udhibiti wa maeneo hayo.

g
Maelezo ya picha,Maafisa wa polisi takriban 1,000 wa Kenya wanastahili kuwa sehemu ya kikosi kazi cha polisi wa mataifa mbalimbali.

Idadi kamili ya waliofariki kutokana na shambulio hilo haijabainika, vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuwa zaidi ya 50 wameuawa, huku kundi la haki za binadamu la Haiti likisema idadi hiyo kuwa 20 au zaidi, AP ilisema.

Kundi la Gran Grif linasemekana kuwa mojawapo ya magenge ya ukatili zaidi ya Haiti. Mnamo Januari 2023 wanachama wake walishtakiwa kwa kushambulia kituo cha polisi karibu na Port-Sondé na kuwaua maafisa sita. Pia linalaumiwa kwa kulazimisha kufungwa kwa hospitali inayohudumia zaidi ya watu 700,000.

Tazama: Milipuko ilipotokea karibu na uwanja wa ndege wa Beirut

Maelezo ya video,Tazama: Wakati milipuko mikubwa ilipotokeakaribu na uwanja wa ndege wa Beirut

Mashambulizi ya mabomu ya Israel yamesababisha milipuko mikubwa nje kidogo ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beirut wakati wa usiku mwingine wa mashambulizi ya anga yaliyolenga Hezbollah katika mji huo.

Haijabainika ni nini kililengwa, lakini uwanja wa ndege unapakana na eneo la Dahieh ambayo ni ngome ya Hezbollah katika mji huo mkuu.Milipuko hiyo ilionekana kudumu muda.

Zelensky amfuta kazi mkuu wa jeshi la anga la Ukraine

f

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfuta kazi kamanda mkuu wa jeshi la anga la Ukraine, Mykola Oleshchuk, tovuti ya rais imechapisha taarifa hiyo

“Nikolai Nikolaevich Oleshchuk ameondolewa kwenye cheo cha Kamanda wa Jeshi la Anga la Jeshi la Ukraine,” inasema.

Zelensky pia alichapisha ujumbe wa video kuhusu taarifa hiyo.

“Nimeamua kubadilisha kamanda wa esjhi la anga la Ukraine. Ninashukuru sana marubani wetu wote wa kijeshi, wahandisi, askari wa kikundi cha wanajeshi wanaohama, wafanyikazi wa ulinzi anga. Kwa wote ambao kusema kweli hupigana kwa ajili ya Ukraine. Muwajali watu. Wajali wafanyakazi. Tuwatunze wanajeshi wetu wote,” alisema.

Luteni Jenerali Anatoly Krivonozhko, ambaye aliongoza kituo cha jeshi la anga la Ukraine, ameteuliwa kuwa kaimu kamanda wa leshi la anga.

Twanawake na watoto wakizama kwenye maji, na mimi mwenyewe nilikuwa kwenye nikielekea kuzama, lakini Mungu alinisaidia.”

Takriban watu 78 wafariki baada ya feri kuzama katika ziwa DRC

f
Maelezo ya picha,Watu wamekusanyika kando ya ufuo wa Ziwa kivu kupata habari kuhsu wapendwa wao

Takriban watu 78 wamefariki dunia baada ya feri kupinduka kwenye na kuzama katika Ziwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, umbali wa mita mia chache tu kutoka ilipopelekwa.

Feri hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji wa Minova huko Kivu Kusini na kuzama ilipokuwa ikiwasili kwenye ufuo wa Goma siku ya Alhamisi asubuhi.

Video inayosambaa mtandaoni inaonyeshamashua ikiinamia upande mmoja na kisha kuzama.

Kulikuwa na abiria 278 ndani yake, kulingana na gavana wa mkoa.

“Itachukua angalau siku tatu kupata idadi kamili, kwa sababu bado miili yote haijapatikana,” Gavana Jean Jacques Purisi aliliambia shirika la habari la Reuters.

Mwanaharakati wa eneo hilo, Aaron Ashuza, ambaye alikuwa katika eneo la tukio, ameiambia BBC kwamba aliona miili ikitolewa nje ya mto na kwamba majeruhi wamepelekwa hospitalini.

Takriban watoto wawili walifariki baada ya kupelekwa hospitalini baada ya ajali hiyo, kulingana na AFP.

Akizungumza kutoka kwenye kitanda chake hospitalini, manusura wa umri wa miaka 51 Alfani Buroko Byamungu, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba hali ya maji ilionekana “tulivu”.

Aliongeza: “Niliona watu wakizama, wengi wakaingia chini. Niliona wanawake na watoto wakizama kwenye maji, na mimi mwenyewe nilikuwa kwenye nikielekea kuzama, lakini Mungu alinisaidia.”

h

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment