Afrika Leo Asubui-4 Oktoba 2024

Karibu katika Matangazo yetu ya Afrika Leo Asubui moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja……………..

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muhtasari

  • Tazama: Milipuko ilipotokea karibu na uwanja wa ndege wa Beirut
  • Melania Trump awa mke wa rais wa hivi karibuni zaidi kutoka Republican kuunga mkono utoaji mimba
  • Zelensky amfuta kazi mkuu wa jeshi la anga la Ukraine
  • Takriban watu 78 wafariki baada ya feri kuzama katika ziwa DRC
  • Biden asema Marekani inajadili uwezekano wa mashambulizi ya Israel dhidi ya vituo vya mafuta vya Iran
  • Milipuko mikubwa yashuhudiwa Beirut baada ya mashambulizi mapya ya anga ya Israel

Tazama: Milipuko ilipotokea karibu na uwanja wa ndege wa Beirut

Maelezo ya video,Tazama: Wakati milipuko mikubwa ilipotokeakaribu na uwanja wa ndege wa Beirut

Mashambulizi ya mabomu ya Israel yamesababisha milipuko mikubwa nje kidogo ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beirut wakati wa usiku mwingine wa mashambulizi ya anga yaliyolenga Hezbollah katika mji huo.

Haijabainika ni nini kililengwa, lakini uwanja wa ndege unapakana na eneo la Dahieh ambayo ni ngome ya Hezbollah katika mji huo mkuu.Milipuko hiyo ilionekana kudumu muda.

Melania Trump awa mke wa rais wa hivi karibuni zaidi kutoka Republican kuunga mkono utoaji mimba

h

Melania Trump anaonekana kuungana na msururu mrefu wa wake wa rais wa zamani wa chama cha Republican ambao wamejitokeza kuunga mkono haki za utoaji mimba, na hivyo kwenda kinyume na maoni ya umma ya waume zao.

Katika klipu fupi ya video inayotangaza kitabu chake kijacho, Bi Melania Trump alionyesha kuunga mkono “uhuru wa kibinafsi” wa wanawake, akielezea kama “haki muhimu ambayo wanawake wote wanayo tangu kuzaliwa”.

Hii inakuja siku moja baada ya sehemu ya kumbukumbu yake ambayo itatolewa hivi karibuni, ambapo inasemekana ana msimamo wa kuunga mkono uchaguzi ulio wazi zaidi, kuchapishwa katika ripoti ya gazeti.

Msimamo dhahiri wa Bi Trump kuhusu suala hilo unaonekana kutofautiana na msimamo wa mumewe, ambaye amejipongeza kwa kusaidia kupindua uamuzi wa kesi ya Roe v Wade, na kupinga haki ya kikatiba ya kutoa mimba.

Lakini msimamo huu wa Melania inafuatia utamaduni wa Wamarekani wa miongo kadhaa ya wake wa marais kutoka chama cha Republican ambao tangu kuamriwa kwa kesi ya Roe v Wade kwa mara ya kwanza mwaka wa 1973 ambao wamesema utoaji mimba kisheria unapaswa kulindwa.

Zelensky amfuta kazi mkuu wa jeshi la anga la Ukraine

f

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfuta kazi kamanda mkuu wa jeshi la anga la Ukraine, Mykola Oleshchuk, tovuti ya rais imechapisha taarifa hiyo

“Nikolai Nikolaevich Oleshchuk ameondolewa kwenye cheo cha Kamanda wa Jeshi la Anga la Jeshi la Ukraine,” inasema.

Zelensky pia alichapisha ujumbe wa video kuhusu taarifa hiyo.

“Nimeamua kubadilisha kamanda wa esjhi la anga la Ukraine. Ninashukuru sana marubani wetu wote wa kijeshi, wahandisi, askari wa kikundi cha wanajeshi wanaohama, wafanyikazi wa ulinzi anga. Kwa wote ambao kusema kweli hupigana kwa ajili ya Ukraine. Muwajali watu. Wajali wafanyakazi. Tuwatunze wanajeshi wetu wote,” alisema.

Luteni Jenerali Anatoly Krivonozhko, ambaye aliongoza kituo cha jeshi la anga la Ukraine, ameteuliwa kuwa kaimu kamanda wa leshi la anga.

Takriban watu 78 wafariki baada ya feri kuzama katika ziwa DRC

f
Maelezo ya picha,Watu wamekusanyika kando ya ufuo wa Ziwa kivu kupata habari kuhsu wapendwa wao

Takriban watu 78 wamefariki dunia baada ya feri kupinduka kwenye na kuzama katika Ziwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, umbali wa mita mia chache tu kutoka ilipopelekwa.

Feri hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji wa Minova huko Kivu Kusini na kuzama ilipokuwa ikiwasili kwenye ufuo wa Goma siku ya Alhamisi asubuhi.

Video inayosambaa mtandaoni inaonyeshamashua ikiinamia upande mmoja na kisha kuzama.

Kulikuwa na abiria 278 ndani yake, kulingana na gavana wa mkoa.

“Itachukua angalau siku tatu kupata idadi kamili, kwa sababu bado miili yote haijapatikana,” Gavana Jean Jacques Purisi aliliambia shirika la habari la Reuters.

Mwanaharakati wa eneo hilo, Aaron Ashuza, ambaye alikuwa katika eneo la tukio, ameiambia BBC kwamba aliona miili ikitolewa nje ya mto na kwamba majeruhi wamepelekwa hospitalini.

Takriban watoto wawili walifariki baada ya kupelekwa hospitalini baada ya ajali hiyo, kulingana na AFP.

Akizungumza kutoka kwenye kitanda chake hospitalini, manusura wa umri wa miaka 51 Alfani Buroko Byamungu, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba hali ya maji ilionekana “tulivu”.

Aliongeza: “Niliona watu wakizama, wengi wakaingia chini. Niliona wanawake na watoto wakizama kwenye maji, na mimi mwenyewe nilikuwa kwenye nikielekea kuzama, lakini Mungu alinisaidia.”

Biden asema Marekani inajadili uwezekano wa mashambulizi ya Israel dhidi ya vituo vya mafuta vya Iran

g

Joe Biden amesema Marekani inajadiliana na Israel uwezekano wa Israel kushambulia miundombinu ya mafuta ya Iran.

Alipoulizwa iwapo angeweza kuunga mkono mashambulizi kama hayo, Bw Biden alisema: “Tunajadili hilo. Nafikiri hilo litakuwa suala dogo… hata hivyo.”

Kauli hizo alizozitoa Bw Biden alipokuwa akiondoka Ikulu ya Marekani, hazikuweka wazi hatahivyo msimamo wa Washington. Bwana Biden hapo awali alisema hataunga mkono mashambulizi ya Israel dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.

Bei ya mafuta ghafi ya Brent ilipanda kwa 5% mara baada ya matamshi hayo na sasa imeongezeka kwa 10% tangu shambulio kubwa la kombora la Iran dhidi ya Israeli mnamo Jumanne.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Iran “italipa gharama kubwa” kwa shambulio la Jumanne, ambapo angalau makombora 180 ya balestiki yakirushwa dhidi ya Israel.

Picha za satelaiti zilizochapishwa na shirika la habari la Associated Press zilionyesha uharibifu wa kituo cha anga cha Nevatim, mojawapo ya maeneo yaliyolengwa katika mashambulizi hayo.

Iran ilisema mashambulizi hayo ni jibu kwa mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh, kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah na kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran Brigadia Jenerali Abbas Nilforoushan.

Milipuko mikubwa yashuhudiwa Beirut baada ya mashambulizi mapya ya anga ya Israel

f

Mashambulizi ya mabomu ya Israel yamesababisha milipuko mikubwa nje kidogo ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beirut wakati wa usiku mwingine wa mashambulizi ya anga yaliyolenga Hezbollah katika mji huo.

Haijabainika ni nini kililengwa, lakini uwanja wa ndege unapakana na eneo la Dahieh ambayo ni ngome ya Hezbollah katika mji huo mkuu.

Kwingineko, jeshi la Lebanon limesema wanajeshi wake wawili wameuawa kusini mwa nchi hiyo wakati wanajeshi wa Israel wakiendelea na uvamizi wao dhidi ya Hezbollah na kuamuru wakazi wa miji na vijiji vingine 20 kuhama.

Jeshi la Israel halijasema lolote, lakini lilisema wanajeshi wake wamewaua wapiganaji wa Hezbollah karibu na mpaka.

Hezbollah ilisema iliwalenga wanajeshi wa Israel katika pande zote za mpaka.

Mashambulizi mawili mabaya dhidi ya wanajeshi wa jeshi la Lebanon yalitofautiana kwa saa chache siku ya Alhamisi, ikiwa ni siku ya tatu ya uvamizi kamili.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema wafanyakazi wake wanne wa kujitolea pia wamejeruhiwa kidogo, na kwamba harakati zao ziliratibiwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Tofauti na jamii zilizoamrishwa kuhama siku ya Jumanne, zote ziko kaskazini mwa mto Litani, ambao uko umbali wa kilomita 30 (maili 18) kutoka mpakani.

Kabla ya uvamizi huo, Israel iliitaka Hezbollah kujiondoa kutoka Litani, kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililomaliza vita vyao vya mwisho mwaka 2006.

Mwamba mkubwa ulioua Dinosaria haukuwa peke yake

DC

Maelezo kuhusu taarifa

  • Author,Georgina Rannard
  • Nafasi,BBC

Mwamba mkubwa (asteroid) ambao uligonga dunia na kuwaangamiza Dinosaria ama Dinosa miaka milioni 66 iliyopita, haukuwa peke yake, wanasayansi wamethibitisha.

Mwamba wa pili, uilianguka baharini karibu na pwani ya Afrika Magharibi na kuunda bonde kubwa katika kipindi hicho hicho.

“Lilikuwa janga,” wanasayansi wanasema, na lilisababisha tsunami ya mita 800 kwenda juu na kusababisha bonde kubwa (kreta) katika bahari ya Atlantiki.

Dk Uisdean Nicholson kutoka Chuo Kikuu cha Heriot-Watt, aligundua bonde la Nadir kwa mara ya kwanza mwaka 2022, lakini haikujuulikana ni kwa namna gani shimo hilo lilivyoundwa.

Sasa Dkt Nicholson na wenzake wana uhakika kwamba bonde hilo la kilomita 9, lilisababishwa na mwamba ulioanguka chini ya bahari.

Hawajui tarehe kamili ya tukio hilo, na wala hawajui ikiwa lilitokea kabla au baada ya mwamba mkubwa ulioweka bonde la Chicxulub lenye upana wa kilomita 180 huko Mexico. Ambalo lilimaliza uhai wa dinosa.

Wanasema mwamba wa pili ulitokea mwishoni mwa kipindi cha Cretaceous (miaka milioni 65.5 iliyopita) wakati dinosa walipopotea. Mwamba huo ulipoingia kwenye angahewa ya dunia, ulitengeneza jiwe la moto.

“Fikiria mwamba huo ukigonga mji wa Glasgow na wewe uko Edinburgh, karibu kilomita 50. Jiwe la moto la karibu mara 24 ya ukubwa wa Jua – linatosha kuteketeza miti na mimea ya Edinburgh,” anasema Dk Nicholson.

Mlipuko mkubwa sana hufuata, kabla ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7 katika kipimo cha Richter.

Kiasi kikubwa cha maji kiliondoka chini ya bahari, na baadaye kilirudi na kuunda alama za kipekee chini ya sakafu ya bahari.

Ni kawaida kwa miamba mikubwa kama hii kuanguka nje ya mfumo wetu wa jua. Lakini watafiti hawajui kwa nini miamba miwili ilipiga dunia katika muda wa kukaribiana.

vc

Mwamba uliounda bonde la Nadir lenye upana wa karibu mita 450-500, wanasayansi wanaamini uligonga dunia kwa kasi ya kilomita 72,000 kwa saa.

Tukio la karibuni zaidi kama hilo ni la Tunguska la 1908 wakati mwamba wa mita 50 ulipolipuka angani juu ya nchi ya Siberia.

Mwamba wa Nadir ulikuwa sawa na ukubwa wa mwamba wa Bennu, ambao kwa sasa ndiyo mwamba hatari zaidi unaozunguka karibu na dunia.

Wanasayansi wanasema tarehe inayokadiriwa ambapo Bennu unaweza kupiga dunia ni 24 Septemba 2182, kulingana na Nasa. Lakini hayo ni makadirio tu.

Ili kuelewa zaidi bonde la Nadir, Dk Nicholson na timu walichanganua data kutoka kampuni ya kijiofizikia iitwayo TGS.

Mabonde mengi humomonyoka lakini hii limejihifadhi vyema, ikimaanisha kuwa wanasayansi wanaweza kuangalia zaidi viwango vya mawe madogo madogo.

“Hii ni mara ya kwanza tumeweza kuona ndani ya bonde kama hii” anasema Dk Nicholson, akiongeza kuwa kuna mashimo 20 tu ya baharini lakini hakuna hata moja ambalo limechunguzwa kwa kina kama hii.

Utafiti wao ulichapishwa katika jarida la Nature Communications Earth & Environment.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment