Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Majira yako ya mateso (Season of Aflliction), ni majira muhimu ya kukusaidia kuwajuwa watu.
Ukipitia majira haya, ambayo mara nyingi utagundua kuwa hauko kwenye hali nzuri aidha kifedha, kiafya au umepoteza kazi n.k
Hapa ndio utajua watu wako wa karibu. Kuna wengi ambao ulikuwa unafikiria kuwa ni watu wako wa karibu sana, utakuja kugundua kuwa sio kama ulivyokuwa unadhani.
Ukweli ni kuwa, mambo yatabadilika na watu ambao wanakuzunguka pia watabadilika.
Uwe makini na kila kinachoendelea kwenye maisha yako na kila anayekuzunguka kwa wakati huo, kwa sababu ukishavuka hapo utahitaji kufanya mabadiliko ya aina ya watu wanaokuzunguka.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.