Rwanda yapiga marufuku  watoto kutembelewa shule kufuatia Marburg

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Serikali ya Rwanda imesema kutembelewa kwa wanafunzi katika shule za mabweni kutaanza tena baada ya Wizara kufanya tathmini ya kina.

Wanafunzi wanaoonyesha dalili za Marburge lazima wapelekwe katika kituo cha afya mara moja/  Picha:  Wizara ya Elimu Rwanda  X

Wizara ya Elimu nchini Rwanda imesitisha kwa muda ziara za kila mwezi kwa wanafunzi katika shule za mabweni ikiwa ni moja wapo ya hatua za kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa homa ya Marburg (MVD), ugonjwa hatari wa kuvuja damu.

Taarifa ya Oktoba 2 kutoka Wizara ya Afya inaonyesha kuwa ugonjwa huo ulikuwa tayari umegharimu maisha ya watu 11.

“Ili kupunguza usambazaji, imesimamisha kuwatembela watoto shuleni kila mwezi,” taarifa kutoka Wizara ya Elimu imesema.

Serikali imesema watoto utaratibu huo utaanza tena baada ya tathmini ya Wizara na Mamlaka ya Afya.

“Katika hali za dharura, wazazi wanaweza kushirikiana na wasimamizi wa shule kutuma vifaa muhimu kupitia mbinu mbadala, ikiwa ni pamoja na njia za kidijitali inapowezekana,” taarifa kutoka Wizara ya Elimu iliongezea.

Kulingana na miongozo mipya, wasimamizi wa shule na walimu lazima wafuatilie wanafunzi iwapo watakuwa na dalili za ugonjwa wa Marburg, ambazo ni pamoja na homa kali, maumivu makali ya kichwa, maumivu ya misuli, uchovu, kichefuchefu, kutapika na kuharisha.

Wanafunzi wanaoonyesha dalili hizi wanatakiwa kupelekwa kwenye kituo cha afya mara moja.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment