Siku za hivi karibuni,niliwai nena na msichana mmoja redioni katika harakati yangu ya kila siku kupakua kipindi kinachohusiana na mahusiano,kufuatia ujumbe alioutuma. Alikua mwenye majonzi tele,hali ya maisha ilivyokua imemzonga na alihitaji kufanya maamuzi mazito. Alianza kwa kusema “Mimi ni msichana wa miaka 24 ndugu mtangazaji,Mimi Ni msichana ambaye nilibakwa na rafiki yangu wakiume ambaye nilikuwa nikimwamini nakumtumaini sana”Hili swala limenikera kwa mda mrefu. Nilimpa nisikio kufahamu mengi,Kijana ambaye alikuwa ni rafiki yangu wa mtaa mmoja kwa muda mrefu sana. Tulikuwa tukiheshimiana kama kaka na Dada. Lakini siku moja tukiwa kwao mida ya jioni alini ingilia kimwili kwa lazima huku akinitisha kunichoma kisu endapo nitaleta ubishi.
Sikumweleza mtu yoyote juu ya tukio ilo baya, ilibaki kuwa siri yangu moyoni nikaendelea na maisha huku nafsi yangu ikiumia sana.
Basi wiki chache baadaye tokea nibakwe nikiwa naanza kurudi katika hali ya kawaida, ghafla nilianza kujihisi kuchoka choka, mara usingizi na kichefu chefu.
Basi nikaamua kwenda hospital ya karibu ili nikafanye vipimo. Katika hali yakushangaza nikaambiwa nina mimba.
Nikamweleza doctor kuwa Mimi ni mwanafunzi bado, na pia sipo tayari kuzaa kwa sasa. Ndipo doctor alishauri tuitoe iyo mimba na akasema itabaki kuwa siri.
Nikaingia chumba cha huduma lakini kabla ya process kuanza, nikamuomba Mungu anisamehe kwa ninachoenda kufanya.
Lakini katikati ya h7iyo operation nilipoteza fahamu, mara nikajiona nainuka juu huku mwili wangu mwingine ukiwa unabaki pale kwenye kitanda cha operation..! Mara ghafla nikasukumwa kurudi chini..chini ambako kulikuwa na shimo lenye kiza nene na lisilo na mwisho! Kulikuwa na kiza tena kiza Nene.! Niliona viumbe wa ajabu kama cell na kila aina ya matisho, nikajua tayari nilikuwa jehanamu.
Niliwaona wanawake wengi wakiwa pale zaidi ya mamia ya miaka wakiwa wanateseka sana, niliona watu kadhaa wa kadhaa wakilia wakijirudi katika maumbo ya kawaida kisha wanakuwa mifupa yani ilikuwa ni kilio, hapo ndio nikaamini sasa nipo kuzimu.
Na Mimi nikaanza kuungua kwa maumivu nikajikuta nazitoa nywere zangu na macho Mimi mwenyewe huku nalia kwa uchungu.! Adhabu ya moto haikuwa na kikomo kabisa. Kadri muda ulivyozidi kwenda nikajikuta Mimi ndio nalia kupita wote pale lakini haikusaidia chochote maana mateso ndio yalizidi zaidi na zaidi. Palikuwa na halufu mbaya, funza, na kila mdudu mwenye sumu kali.
Nilipoona hakuna njia yakuweza kutoka ndipo nikaanza kumlilia MUNGU aniulumie.
Mara nikamuona Yesu akitokea, ndipo nikazidisha kulia nikimuomba anipe sekunde moja nyingine au aniweke sehemu tofauti na hapo jehanamu ili nitubu.
Yesu akajibu:
“kuna sekunde ngapi katika dakika moja?”
kuna dakika ngapi katika saa moja?
kuna masaa mangapi katika siku moja?
kuna siku ngapi katika wiki moja?
kuna wiki ngapi katika mwezi?
na kuna miezi mingapi katika mwaka mmoja? Je; ulishindwa kutubu ukiwa duniani?”
Nilikupa mamilioni ya sekunde katika miaka yako 24, lakini yote uliniangusha..!
Nikalia sana huku nikimuomba Bwana Yesu anirudishe duniani ata bila mikono wala miguu, mladi niwe napumua tu ili niwaeleze watu kuhusu jehanam. Na mateso yake.
Yesu akajibu: “Wengi waliomba kama wewe na nikawarudisha duniani, lakini ata walipo waeleza watu juu ya jehanamu, walipuuzwa tu.
Ila nakusamehe nakurudisha ukatoe ushuuda.”
Yesu alinisamehe nakunionya kama nisipo wahubiria watu atanipa adhabu,
Alisema: “WAAMBIE WATU WANGU, WAACHE KUCHEZA NA MIMI”
Mara nikaamka nakujikuta nipo kwenye chumba cha maiti huku nikiwa nimefunikwa shuka jeupe na pamba puani mwangu.!! Maskini nilikuwa naandaliwa kwenda kuzikwa kama sio kuwekwa kwenye fridge.!
Sasa nipo hai na huu mkasa wangu wa kweli, naomba usipuuze, tubu dhambi zako acha maovu, Naomba ubadilike uingie mwaka 2020 ukiwa mpyaa kwani utapungukiwa nini?
KAMA UMESOMA HAYA MAKALA JUA UNA BAHATI, NA NI NAFASI YAKO KUBADILIKA. PIA NI WAKATI WAKO KUACHA KUCHEZA NA MUNGU.
Kama umebarikiwa na ujumbe wangu, naomba share. Pia waombee wote watakao andika Ameni wafike salama mwaka 2020.
CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo…
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!
Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.