Mambo ya kufahamu kuelekea uchaguzi mkuu wa urais nchini Msumbiji

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Raia wa Msumbiji wiki ijayo wanatarajiwa kuchagua rais na wabunge katika uchaguzi mkuu ambao huenda ukashuhudia chama tawala Frelimo kikiendelea kusalia madarakani huku masuala kadhaa yakitarajiwa kuwa ajenda kuu za wagombea.

Filipe Jacinto Nyusi- Rais wa sasa wa Msumbiji.
Filipe Jacinto Nyusi- Rais wa sasa wa Msumbiji. via REUTERS – Pool

Ni uchaguzi ambao mgombea wa chama tawama Daniel Chapo, mtangazaji wa zamani na mhadhiri wa sheria, anatarajiwa kumrithi rais Filipe Jacinto Nyusi.

Hata hivyo masuala kadhaa yanatazamwa na wagombea ikiwemo vita dhidi ya makundi ya kijihadi kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo maelfu ya raia wameuawa na wengine kukimbia makazi yao kwenye jimbo la cabo Delgado tangu mwaka 2017.

Aidha agenda ya kufufua uchumi kupitia miradi ya gezi ni suala jingine linalozungumzwa na raia, ambapo tangu kuzuka kwa uasi kaskazini mwa nchi hiyo, miradi yenye thamani ya karibu dola bilioni 50 ilisimama, kampuni ya kifaransa ya mafuta TotalErnergies ikilazimika kufunga kabisa opereshen zake nchini humo.

Kasha ya madeni na hasa sakata la kesi ya Tuna Bond, ambapo zaidi ya dola bilioni 1 na laki 5 fedha za mkopo zilizotolewa kwa serikali kwa ajili ya miradi ya uvuvi na benki ya Credit Suisse, zilitumika vibaya katika moja ya ubadhirifu mkubwa uliotia doa nchi hiyo.

Kadhalika suala la mabadiliko ya tabia nchi, ni moja ya jambo linaloangaziwa na wagombea, ambapo athari za mabadiliko ya hali ya hewa zimeathiri watu zaidi ya milioni 1 wanaoshuhudia ukame, hii ni kwa mujibu wa umoja wa Mataifa.

Suala jingine mtambuka ni kuhusu mkataba wa amani kati ya Frelimo na kundi la zamani la waasi lililogeuzwa kuwa chama cha siasa Renamo, ambao tangu maridhiano ya mwaka 1992, pande hizo zimekuwa zikivutana na wakati mmoja kutishia kuitumbukiza tena nchi hiyo kwenye machafuko na hasa wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mkuu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment