Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa
Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania imesitisha kwa muda leseni ya maudhui ya mtandaoni kampuni ya “Mwananchi Communications” inayochapisha magazeti ya Mwananchi na The Citizen, baada ya kuchapisha picha za video zilizoonekana kumuhusisha Rais Samia Suluhu Hassan na matukio ya utekaji na mauji wa wapinzani.

Kufuatia uamuzi huu, tayari umeibua hisia mseto, baadhi ya watetezi wa haki za binadamu wakiukosoa kwa madai kuwa mamlaka zinajaribu kuingilia uhuru wa vyombo vya habari.
Baadhi ya wanahabari nchini humo wameungana na watetezi wa haki za binadamu kukosoa hatua hiyo waliyosema ni wazi inarudisha nyuma hatua ambazo zilikuwa zimeanza kupigwa tangu rais Samia alipoingia madarakani.
Kibonzo hicho kilichapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa gazeti la kila wiki la The Citizen, kikimuonesha rais Samia akitazama video za wakosoaji wa serikali pamoja na waathiriwa wa ukandamizaji wa serikali.

Rais Samia anakabiliwa na shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na tuhuma kwamba maofisa wa usalama wanahusika na matukio ya utekaji na mauji ya wanasiasa wa upinzani.
Jumatano ya wiki hii, gazeti la The Citizen, linalochapisha habari zake kwa lugha ya kiingereza lilitoa taarifa kwamba mamlaka ya mawasiliano ilikuwa imelipiga marufuku kwa muda siku 30.
Awali gazeti hilo lilikuwa limeondoa picha hizo kwa msingi kwamba zilikuwa zimeibua hisia kuhusiana na masuala ya kiusalama.

Rais Samia alichukua madaraka kufuatia kifo cha mtangulizi wake hayati John Magufuli mwaka wa 2021.
Tangu aingie madarakani, ameondoa baadhi ya vikwazo vilivyokuwa vimetangazwa dhidi ya upinzani ikiwemo kufanya mikutano ya kisiasa.
Mashirika ya kiraia na nchi za Magharibi ikiwemo Marekani yamekashifu ukandamizaji wa wapizani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba na ule wa urais wa mwaka wa 2025.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.