Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore
Wanajeshi wanane wa Israel wauawa katika mapigano na Hezbollah ndani ya Lebanon – IDF
Pande zote mbili zimeripoti kukabiliana ndani ya Lebanon siku moja baada ya Israel kutangaza kuwa vikosi vyake vya ardhini vinavuka mpaka.
Muhtasari
- Guterres alaani shambulizi la Iran baada Israel kumpiga marufuku
- Senegal yampiga kalamu kocha wa timu ya taifa Aliou Cisse
- Hezbollah yadai kuisababishia hasara jeshi la Israel
- Urusi yadai kuuteka mji wa Vuhledar mashariki mwa Ukraine
- Wanajeshi wanane wa Israel wauawa katika mapigano na Hezbollah ndani ya Lebanon – IDF
- Abiria 100 hawajulikani walipo kufuatia ajali ya boti Nigeria
- Hezbollah yatangaza kukabiliana upya na wanajeshi wa Israel
- Israel yampiga marufuku katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo
- Iran: Khamenei azisuta nchi za magharibi baada ya kuishambulia Israel
- Jeshi la Sudan laapa kuendelea kupigana licha ya juhudi za amani
- Roketi takriban 100 zimerushwa kaskazini mwa Israel leo asubuhi
- Israel yatuma wanajeshi zaidi katika operesheni ya ardhini ya Lebanon
- Sean ‘Diddy’ Combs akabiliwa na madai mapya zaidi ya 100 ya unyanyasaji
- Mvutano unazidi kuongezeka Mashariki ya Kati huku mashambulizi yakiendelea
- Bei ya mafuta yapanda baada ya shambulizi la Iran
- Iran yanasema inaweza kuishambulia “miundombinu yote ya Israeli” ikiwa Israeli italipiza kisasi
- Tazama: Video inayoonyesha mashambulizi ya makombora ya Iran nchini Israel
- Marekani yasema iliisaidia Israel kuyadungua makombora ya Iran
- Netanyahu asema Iran italipia mashambulizi ya makombora, huku Israel ikianzisha mashambulizi mapya Beirut
Guterres alaani shambulizi la Iran baada Israel kumpiga marufuku

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel, baada ya kupigwa marufuku na nchi hiyo.
Akizungumza na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, António Guterres alisema ni wakati mwafaka kusitisha kile alichokiita “mzunguko mbaya wa ghasia za nipe nikupe” katika Mashariki ya Kati.
Hapo awali Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz alitangaza kuwa Guterres hana ruhusa ya kuingia nchi hiyo kwa kuwa “katibu mkuu anayepinga Israel na anaunga mkono magaidi”.
Maoni hayo yalitolewa kujibu Guterres akitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, lakini bila kutaja haswa shambulio la Iran.
Wakati huo huo Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amelitaja shambulizi la makombora la Iran dhidi ya Israel kuwa ni ongezeko kubwa la mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Linda Thomas-Greenfield anasema baraza la usalama la umoja huo linapaswa kuchukua hatua “haraka”.
Senegal yampiga kalamu kocha wa timu ya taifa Aliou Cisse

Aliou Cisse ameondolewa kwenye nafasi yake ya ukocha wa Senegal baada ya kuinoa timu ya taifa ya Lion of Teranga kwa miaka tisa na nusu.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 aliwaongoza Waafrika Magharibi kutwaa taji lao la kwanza la bara, na kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika la 2021 (Afcon) lililocheleweshwa mnamo Februari 2022.
Ingawa mkataba wake wa awali ulimalizika Agosti, aliingoza Senegal katika mechi mbili za kufuzu Afcon 2025 mwezi uliopita, sare ya 1-1 na Burkina Faso na ushindi wa 1-0 dhidi ya Burundi.
Shirikisho la soka nchini humo (FSF) lilitaka dili la Cisse lirudishwe lakini wizara ya michezo, chini ya serikali mpya ya Bassirou Diomaye Faye, imefanya uamuzi wa kumuachisha kazi kwa kuhudumu kwa muda mrefu siku tisa tu kabla ya mechi ijayo ya mchujo.
Hezbollah yadai kuisababishia hasara jeshi la Israel
Kundi la Hezbollah linadai kuwa wapiganaji wake wamekabiliana na wanajeshi wa Israel ambao walikuwa wakijaribu kuzunguka kijiji cha Yaroun, kusini mwa Lebanon.
Hezbollah inasema wapiganaji wake “waliwashambulia” wanajeshi wa Israel kwa kilipuzi na kusababisha “maafa”.
Haya ni makabiliano ya pili wa moja kwa moja ambayo Hezbollah imedai kufanya.
Hapo awali, kundi hilo lilisema kuwa lilipambana na jeshi la Israel wakati “lilipovamia” mji wa Maroun al-Ras nchini Lebanon – ambao uko umbali wa kilomita 5 kaskazini mashariki mwa Yaroun.
Shambulio hili na mengine hayajathibitishwa na jeshi la Israel.
Lakini pande zote mbili sasa zimeripoti kupambana ”karibu” hii leo.
Netanyahu afanya mazungumzo na wakuu wa usalama
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefanya mashauriano na wakuu wa usalama leo mchana mjini Tel Aviv.
Katika picha hapa chini, anaweza kuonekana ameketi mkabala na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant miongoni mwa wengine.
Netanyahu hapo awali aliapa kuijibu hatua Iran, akielezea shambulio hilo kubwa la jana usiku kama “kosa kubwa” ambalo Tehran “itajutia”.
Urusi yadai kuuteka mji wa Vuhledar mashariki mwa Ukraine

Wanajeshi wa Urusi wameudhibiti kikamilifu mji wa mashariki wa Vuhledar, ambao wanajeshi wa Ukraine wamekuwa wakiulinda tangu kuanza kwa uvamizi wa Moscow miaka miwili na nusu iliyopita.
Kamandi ya kijeshi ya mashariki mwa Ukraine ilithibitisha Jumatano kwamba iliwaambia wanajeshi ambao bado wanapigana katika sehemu za Vuhledar warudi nyuma ili wasije wakazingirwa.
Kwa zaidi ya miaka miwili Urusi imekuwa ikijaribu kuuteka mji huu ili kusonga mbele upande wa kaskazini na kufikia vituo vya usafirishaji vya kikanda kama Kurakhove na Pokrovsk.
Wanablogu wa kijeshi wanaoiunga mkono Kremlin walikuwa wamechapisha video kadhaa siku moja kabla ya kuwaonyesha wanajeshi wa Urusi wakiwa na bendera kwenye paa za majengo tofauti ya mji wa Vuhledar.
Wanajeshi wanane wa Israel wauawa katika mapigano na Hezbollah ndani ya Lebanon – IDF

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limethibitisha kuwa askari wake wanane wa wameua katika makabiliano na wapiganaji wa Hezbillah kusini mwa Lebanon
IDF inasema watatu walikuwa wa kitengo cha Egoz,
Awali ilitangaza katika taarifa kwamba Kapteni Eitan Yitzhak Oster, 22, aliuawa ndani ya Lebanon siku ya Jumatano.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa katika kitengo cha Egoz, cha makomando maalumu wa vita vya ardhini, IDF inasema.
Awali IDF iliripoti kuwa “inapigana maeneo kadhaa” kusini mwa Lebanon.
“Jeshi la Wanahewa la Israeli, waliwatimua magaidi na kuharibu miundombinu ya kigaidi kwa mabomu yaliyoongozwa kwa usahihi na ushirikiano ya karibu.”
Taarifa hiyo inaongeza “zaidi ya miundombinu 150 ya ugaidi” imeharibiwa na katika mashambulizi ya hivi majuzi.
Abiria 100 hawajulikani walipo kufuatia ajali ya boti Nigeria
Mamlaka katika jimbo la Niger ya Kati nchini Nigeria wamesema takriban abiria 100 hawajulikani walipo baada ya ajali ya boti iliyotokea jana usiku kwenye mto Niger.
Boti hiyo ilikuwa safarini kutoka Mundi ikiwa na zaidi ya abiria 300, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Ripoti za vyombo vya habari nchini humo zinasema takriban miili 60 ilipatikana baada ya ajali hiyo.
Abiria wengi walisemekana kuhudhuria tamasha la Waislamu, sherehe za Maulid huko Gbajibo.
Mkuu wa Shirika la Usimamizi wa Dharura wa Jimbo la Niger Abdullahi Baba Arah alisema katika taarifa kwamba mamlaka hiyo imeanza kufuatilia shughuli za utafutaji na uokoaji kwa kutumia watu wa kujitolea na wazamiaji wa ndani.
Bw. Baba Arah alisema kuwa mwitikio wa haraka kutoka kwa wafanyakazi wa kujitolea wa jamii umewezesha zaidi ya watu 150 kuokolewa kufikia sasa.
Alieleza kuwa shughuli ya uokoaji bado inaendelea ili kupata manusura zaidi.
Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana. Hata hivyo matukio ya kupinduka kwa boti katika Mto Niger ni ya kawaida hasa msimu wa mvua ambao hufanya kiwango cha maji mtoni kupanda.
Hezbollah yasema mapigano ya leo ni ‘awamu ya kwanza’ ya vita
Msemaji wa Hezbollah anasema mapambano yao ya leo dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Israel kusini mwa Lebanon ni sehemu ya “duru ya kwanza ya vita”.
“Vikosi vyetu na wapiganaji wamejiandaa kikamilifu kukabiliana na adui,” Mohammad Afif wa Hezbollah aliwaambia waandishi wa habari, kama alivyonukuliwa na mashirik aya habari ya Reuters na NBC.
Afif anaongeza kuwa kundi hilo la wanamgambo lina silaha za kutosha kwa makabiliano na IDF.
Hezbollah na IDF wote wanaripoti mapigano ya ardhini ndani ya Lebanon siku ya Jumatano.
Hezbollah imetangaza hatuao hiyo baada ya wanajeshi wa Israel “kuvamia” mji wa Maroun al-Ras nchini Lebanon.
Mji huo uko karibu kilomita mbili kutoka mpaka wa Israeli-Lebanon.
Kwa mujibu wa Hezbollah, wanajeshi wa Israel waliingia kutoka upande wa mashariki, na mapigano yanaendelea, ilisema saa moja iliyopita.
Haya ni makabiliano ya pili ya moja kwa moja na wanajeshi wa Israel ambayo Hezbollah imedai leo.
Hapo awali, kundi hilo lilisema limefanikiwa kuzima uvamizi wa Israel nchini Lebanon.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.