Israeli imempiga marufuku katibu mkuu wa UN kuingia nchini mwake

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Israel imetangaza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuwa mtu asiyetakiwa, ikimpiga marufuku kuingia katika ardhi ya Israeli kwa kile imesema ni hatua kiongozi huyo kukosa kulaani shambulio la Iran.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Israeli, Israel Katz amemtaja Guterres kama mtu anayetoa msaada kwa magaidi, wabakaji na wauaji.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Israeli, Israel Katz amemtaja Guterres kama mtu anayetoa msaada kwa magaidi, wabakaji na wauaji. © David Dee Delgado / Reuters

Waziri wa mambo ya kigeni wa Israeli, Israel Katz amemtaja Guterres kama mtu anayetoa msaada kwa magaidi, wabakaji na wauaji.

Katz aidha amemtaja Guterres kama kiongozi atakayekumbukwa kama doa kwenye historia ya Umoja wa Mataifa kwa kuwaunga mkono magaidi wa HamasHezbollah, Huthi na sasa Iran.

Baada ya shambulio la Iran nchini Israeli, Guterres alilaani kuongezeka kwa mzozo wa mashariki ya kati akikashifu vitendo vinayozidisha mzozo huo mara kwa mara.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. AP – Pamela Smith

Guterres alitoa wito wa kuwepo kwa usitishaji wa mapigano mara moja mashariki ya kati.

Israel imekuwa mkosoaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa, uhusiano kati ya Israeli na UN ukionekana kuyumba zaidi baada ya shambulio la Hamas la tarehe 7 ya mwezi Oktoba.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment