Bei ya mafuta yapanda baada ya shambulizi la Iran

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Bei ya mafuta ilipanda baada ya Iran kurusha makombora ya balistiki dhidi ya Israel na kuzua hofu ya mzozo mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati ambao unaweza kuvuruga usambazaji wa mafuta.

Brent crude – kigezo muhimu cha bei ya mafuta kimataifa – kilipanda kwa zaidi ya 1% hadi $74.40 kwa pipa.

Wakati wa biashara Jumanne, kigezo hicho kilipanda kwa zaidi ya 5%. Iran ni nchi ya saba kwa uzalishaji wa mafuta duniani, kulingana na Utawala wa Taarifa za Nishati wa Marekani, na mwanachama wa tatu kwa ukubwa wa shirika la wazalishaji wa mafuta la Opec.

Wafanyabiashara pia wanahofia kuongezeka kwa mzozo wa kijeshi katika eneo hilo kunaweza kuathiri usafiri wa meli kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz.

Njia hiyo ya meli – ambayo iko kati ya Oman na Iran – ni muhimu kwa biashara ya kimataifa ya mafuta na 20% ya bidhaa za ulimwengu zinapitia humo.

Wanachama wengine wa OPEC Saudi Arabia, UAE, Kuwait na Iraq pia hutuma mafuta mengi wanayouza nje kupitia Mlango huo wa Bahari.

Iran yanasema inaweza kuishambulia “miundombinu yote ya Israeli” ikiwa Israeli italipiza kisasi

g

Mkuu wa majeshi ya Iran Meja Jenerali Mohammad Bagheri ametishia kulenga miundombinu ya Israel, ikiwa itachukua hatua zozote za kulipiza kisasi dhidi ya Tehran.

“Ikiwa [Israeli]… inataka kuendeleza uhalifu huu au inataka kufanya lolote dhidi ya mamlaka yetu na uadilifu wa eneo, operesheni ya usiku wa leo itarudiwa mara kadhaa kwa nguvu zaidi na miundombinu yao yote italengwa,” Bagheri alisema mapema.

Pia alielezea Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, kitengo cha kijeshi cha wasomi zaidi wa taifa kuwa tayari kujilinda na operesheni kurudia shambulio la kombora la Jumanne dhidi ya Israeli kwa “nguvu nyingi”.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu tayari ameahidi kwamba Iran itakabiliwa na “matokeo” makubwa kwa shambulio hilo.

  1. Tazama: Video inayoonyesha mashambulizi ya makombora ya Iran nchini Israel Play video, “Video shows Iran’s missile attack on Israel”, Muda 1,0201:02Maelezo ya video,Video inayoonyesha mashambulizi ya makombora ya Iran nchini IsraelVideo ya mashambulizi ya makombora ya Irandi nchini Israel inaonyesha makombora ya Iran yakipaa juu ya anga la Israel na baada ya muda mfupi makombora ya kudungua makombora(Interceptors) ya Israel [upande wa kushoto wa video] yalionekana kukabiliana nayoIran ilirusha makombora makubwa dhidi ya Israel – huku jeshi la Israel likisema lilizuia zaidi ya roketi 180 zilizofyatuliwa.Mshirikishe mwenzako, Tazama: Video inayoonyesha mashambulizi ya makombora ya Iran nchini Israel

  1. Marekani yasema iliisaidia Israel kuyadungua makombora ya Irang

Marekani ilifyatua makombora makumi kadhaa ya kudungua nmakombora ya masafa marefu ya Iran yaliyofyatuliwa nchini Israel, Pentagon imesema.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema Marekani “iliunga mkono kwa dhati” ulinzi wa Israel kwa agizo lake. Alisema asubuhi alitumia muda wake mwingi kushughulikia masuala makubwa ya usalama wa taifa katikachumba maalumu cha kushughulikia hali (Situation Room ) katika ikulu ya White House.

Jeshi la Israel limesema takriban makombora 180 yalirushwa dhidi ya Israel, huku mengi yakizuiliwa angani.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ametetea mashambulio hayo , akiyaita “majibu ya uamuzi” “katika kulinda maslahi ya Iran na raia”.

Makombora ya kudungua makombora yaliyadungua makombora ambayo Marekani iliamini kuwa yote yalirushwa kutoka Iran.

Hakuthibitisha iwapo waliyapiga makombora yoyote ya Iran yaliyotumika katika mashambulizi hayo na aliongeza kuwa taarifa hizi bado hazijabainika.

Iran ilirusha makombora 180 kuelekea Israel, jeshi la Israel limesema.

Idadi hiyo ya makombora inaifanya kuwa kubwa kidogo kuliko yale yaliyorushwa mwezi Aprili wakati Tehran iliporusha makombora 110 ya masafa marefu na makombora 30 aina ya Cruise yaliyorushwa kuelekea Israel.

Meja Jenerali Ryder aliongeza kuwa Pentagon haikuwa na taarifa ya tahadhari yoyote kuhusu shambulio hilo.

Rais Biden amesema Marekani inaunga mkono kikamilifu Israel baada ya shambulio la Jumatano.

“Leo, kwa maelekezo yangu, jeshi la Marekani liliunga mkono kikamilifu ulinzi wa Israeli, na bado tunatathmini athari,” alisema.

“Lakini kwa kuzingatia kile tunachokijua sasa, shambulio hilo linaonekana kushindwa na halina ufanisi. Na hii ni ushahidi wa uwezo wa kijeshi wa Israeli na jeshi la Marekani.”

Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu ni yapi yatakuwa majibu kwa Iran, Biden alisema: “Hilo linajadiliwa hivi sasa. Bado tunaendelea kuliangalia.”

Netanyahu asema Iran italipia mashambulizi ya makombora, huku Israel ikianzisha mashambulizi mapya Beirut

g

Ni saa 12.30 kwa saa za Afrika Mashariki, na tuanze kwa kukupa muhtasari wa yale yaliyojiri hadi sasa kufuatia mzozo wa mashambulizi baina ya Israel, Lebanon na Iran:

  • Iran ilirusha makombora makubwa dhidi ya Israel – huku jeshi la Israel likisema lilizuia zaidi ya roketi 180 zilizofyatuliwa
  • Mwanaume mmoja wa Kipalestina aliuawa katika eneo la ukingo wa magharibi wakati wa uvamizi huo, na shule moja katikati mwa Israel na mgahawa mmoja mjini Tel Aviv ulishambuliwa
  • Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Iran “ilifanya kosa kubwa usiku wa leo, na italipia”
  • Washirika wa Israel wamelaani shambulio hilo, huku rais wa Marekani Joe Biden akisema anaiunga mkono kikamilifu Israel
  • Mapema, Jeshi la Ulinzi la Israel lilisema limeanza operesheni ya ardhini “ya ukomo ya ndani na inayolenga” maeneo nchini Lebanon dhidi ya Hezbollah.
  • Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya wamerejelea wito wa kusitisha mapigano, huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kukutana Jumatano wiki hii.
  • Mapigano ya mpakani kati ya Israel na Hezbollah yameendelea, huku zaidi ya watu 50 wakiuawa na mashambulizi ya Israel, kwa mujibu wa mamlaka za Lebanon

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment