Afrika Leo Jioni.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Muhtasari

  • Ndege tatu za kwanza kutengenezwa Tanzania zazinduliwa rasmi
  • ‘Israel inasimama na nyinyi’: Netanyahu awaambia Wairan
  • Rwanda yadhibiti idadi ya wanaohudhuria mazishi kufuatia mlipuko wa virusi vya Marburg
  • ‘Tutatumia nguvu zote kutoka angani, baharini na nchi kavu’ – Waziri wa Ulinzi wa Israel
  • Marine Le Pen ashtakiwa kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha za EU
  • ‘Tuko tayari kwa uvamizi wa ardhini’- Naibu kiongozi wa Hezbollah
  • Makumi ya roketi yalirushwa kutoka Lebanon- Israel
  • ‘Tuko tayari kwa uvamizi wa ardhini’- Naibu kiongozi wa Hezbollah
  • Kiongozi wa Hamas nchini Lebanon auawa katika mashambulizi ya anga ya Israel
  • Watu 100,000 wakimbia Lebanon kuelekea Syria, UN yasema
  • Mashambulizi ya Israel: Tunachokijua kufikia sasa
  • Viongozi watatu wa Palestina wauawa katika shambulio la Israel huko Beirut
  • SpaceX yatua kituo cha anga za mbali kuwachukua wanaanga waliokwama
  • Huenda mashambulizi ya Israel yamewakosesha makazi watu milioni moja – Waziri Mkuu wa Lebanon
  • Israel yazidisha mashambulizi katika maeneo ya Hezbollah huko Bekaa

‘Israel inasimama na nyinyi’: Netanyahu awaambia Wairan

Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa ujumbe wa moja kwa moja kwa watu Iran, wakati nchi yake ikiendelea na mapambano dhidi ya makundi ya Hamas, Hezbollah na Houthi yanayoungwa mkono na Iran.

Katika video ya dakika tatu iliyoshirikishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Netanyahu anawashutumu viongozi wa Iran kwa kutoa hotuba ya kutetea Gaza na Lebanon lakini “kila siku utawala huo unalitumbukiza eneo letu kwenye giza na zaidi katika vita”.

“Hakuna popote katika eneo la Mashariki ya Kati ambapo Israel haiwezi kufika, hakuna mahali ambapo hatutafika kulinda watu wetu na kulinda nchi yetu,” anasema.

“Kadri muda unavyosonga, utawala unawaelekeza nyinyi, watu watukufu wa Uajemi, kuzimu,” anasema.

Netanyahu anasema Iran “hatimaye itakuwa huru” – akisema wakati huo unakaribia “sana kuliko vile watu wanavyofikiri” – na kila kitu kitakuwa sawa na mataifa hayo mawili yatakuwa na amani.

“Iran itastawi kuliko hapo awali,” anasema, na kuongeza: “Usiruhusu kundi dogo la watu kukandamiza matumaini yako na ndoto zako. Unastahili maisha bora zaidi.”

“Watu wa Iran wanapaswa kujua Israel inasimama pamoja nao,” anaongeza kusema.

Rwanda yadhibiti idadi ya wanaohudhuria mazishi kufuatia mlipuko wa virusi vya Marburg

xx

Mamlaka ya Rwanda imedhibiti idadi ya watu wanaohudhuria mazishi ya waathiriwa wa virusi vya Marburg katika juhudi za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo unaoambukiza kwa kasi.

Watu wanane wamefariki wakati wa mlipuko wa kwanza wa virusi hivyo nchini Rwanda, ambao ulithibitishwa siku ya Ijumaa na wizara ya afya ya taifa hilo.

Marburg, anaweza kusababisha kifo kwa hadi 88%, ni sawa na virusi vya Ebola.

Inasambazwa na popo kwa wanadamu mbao huambukizana kwa kukaribiana na watu walioambukizwa.

Katika miongozo mipya ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Marburg, wizara ya afya ilisema watu watu zaidi ya 50 hawapaswi kuhudhuria mazishi ya mtu aliyefariki kutokana na ugonjwa huo.

Virusi vya marburg vinaweza kusababisha kifo kupitia kuvuja damu.

Miongozo ya wizara ya afya ilisema wagonjwa waliolazwa hospitali hawatatembelewa kwa siku 14 zijazo.

Wagonjwa pia wataruhusiwa tu mlezi mmoja kwa wakati mmoja, miongozo ilisema.

Rwanda inasema kuwa inaimarisha ufuatiliaji, upimaji ili kudhibiti kuenea kwa virusi.

Waziri wa afya wa nchi hiyo alisema Jumapili kwamba maafisa wanawatafuta watu 300 ambao walitangamana na watu walioathiriwa na virusi vya Marburg.

Mamlaka imewataka wananchi kuzingatia usafi wa mazingira kama vile kunawa mikono mara kwa mara.

Hii ni mara ya kwanza kwa Marburg kuthibitishwa nchini Rwanda.

Nchi jirani ya Tanzania iliripoti mlipuko wa ugonjwa huo mnamo 2023, watu watatu walifariki nchini Uganda mnamo 2017.

‘Tutatumia nguvu zote kutoka angani, baharini na nchi kavu’ – Waziri wa Ulinzi wa Israel

Yoav Gallant

Waziri wa ulinzi wa Israel, Yoav Gallant, amekutana na wanajeshi karibu na mpaka wa Lebanon, na kuwaambia watawarudisha raia waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Israel kwa “njia zetu zote”.

Yoav Gallant amewaambia wanajeshi “kuuawa kwa [kiongozi wa Hezbollah] Nasrallah ni hatua muhimu sana, lakini sio mwisho wa mapambano”.

Katika video fupi, anaonekana akiwaambia wanajeshi kwamba “tutatumia uwezo wote tulionao na ikiwa mtu hakuelewa nini maana ya uwezo wote – ni uwezo wote.

“Na wewe ni sehemu ya juhudi hizi, tunaamini utaweza kukamilisha chochote.”

Gallant anaendelea kusema “kila kitu kinachohitajika kufanywa – kitafanyika” na kwamba “tutatumia nguvu zote kutoka angani, bahari na nchi kavu”.

Marine Le Pen ashtakiwa kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha za EU

xx

Kiongozi wa muda mrefu wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally nchini Ufaransa Marine Le Pen, amefikishwa mahakamani mjini Paris leo (Jumatatu) akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za bunge la Ulaya.

Vigogo wengine zaidi ya 20 wa chama hicho pia wanakabiliwa na mashtaka sawia na hayo.

Wanatuhumiwa kuajiri wasaidizi waliofanya kazi kwa maslahi ya chama badala ya bunge la Ulaya ambalo liliwalipa.

Iwapo Le Pen atapatikana na hatia, anaweza kukabiliwa na faini na kifungo – na huenda akatangazwa kuwa hana sifa ya kugombea wadhifa wa urais kwa hadi miaka 10, hatua ambayo itaathiri azma yake ya kugombea urais wa Ufaransa.

Amekanusha mashtaka hayo, na msemaji wa chama Laurent Jacobelli alisema “tutathibitisha kwamba hakuna mfumo wa ubadhirifu wa pesa kutoka kwa EU”.

‘Tuko tayari kwa uvamizi wa ardhini’- Naibu kiongozi wa Hezbollah

Naim Qassem

Hotuba ya Naim Qassem iliangaziwa na ofisi ya habari ya Hezbollah takriban saa moja kabla ya kutangazwa

Hii ilikuwa hotuba ya kwanza kutoka kwa afisa wa ngazi za juu wa Hezbollah tangu kuuawa kwa kiongozi wao Hassan Nasrallah.

Ni wazi alitaka kutuma ujumbe kwamba, licha ya mashambulizi makali yasiyo na kifani amabayo Hezbollah imekumbana nayo, kundi hilo litakuwa imara, huku likijipanga upya na kuendeleza mapambano yake dhidi ya Israel.

Kuhusu nani atachukua nafasi ya Hassan Nasrallah, alisema baraza lao litaamua hivi karibuni.

Lakini alisema makamanda hao wote na viongozi wa ngazi za juu walikuwa na manaibu ambao wanaweza kujaza pengo waliloacha.

Pia alisema kuwa Hezbollah inajua kwamba vita “inaweza kuwa ndefu”, na wanajiandaa “kwa lolote”.

“Tuko tayari kwa uvamizi wa ardhini, na tutaibuka washindi,” alisema.

Pia aliwashukuru raia wote wa Lebanon, na serikali.

Hotuba hiyo ilitolewa kwa watu/wapiganaji wa upinzani – kuwahakikishia kwamba, bila kujali nani atakufa, “upinzani” utachukua nafasi yao na kupigana kwa nguvu.

Soma pia:

Israel inaamini imeidhoofisha Hezbollah lakini mzozo unazidi kukuwa

Israel na Hezbollah: Israel inakabiliwa na adui mwenye silaha na hasira

Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah ni nani?

Makumi ya roketi yalirushwa kutoka Lebanon- Israel

Jeshi la Israel limeripoti kuwa roketi 35 zimerushwa kutoka Lebanon kuelekea kaskazini mwa Israel asubuhi ya leo.

Baadhi ya roketi hizi zilizuiliwa huku zingine zikianguka katika maeneo wazi, IDF inasema.

Hezbollah bado haijatoa maoni yoyote – lakini imeendelea kurusha roketi kuelekea Israel katika siku za hivi karibuni, licha ya Israel kushambulia maeneo na miundombinu yake.

Kiongozi wa Hamas nchini Lebanon auawa katika mashambulizi ya anga ya Israel

xx

Kundi la wapiganaji wa Kipalestina la Hamas linasema kuwa kiongozi wake nchini Lebanon Fateh Sherif Abu el-Amin, ameuawa pamoja na baadhi ya jamaa zake katika shambulio la anga la Israel kusini mwa Lebanon.

Hamas inasema aliuawa katika shambulio dhidi ya “nyumba yake katika kambi ya Al-Bass kusini mwa Lebanon”.

Shirika la habari la serikali la Lebanon liliripoti shambulio la anga dhidi ya kambi hiyo karibu na mji wa kusini wa Tiro.

Ingawa Hamas wako Gaza – ambako Israel imekuwa ikipambana nao tangu mashambulizi ya Oktoba 7 – pia wapo nchini Lebanon.

Makundi ya Hamas na Hezbollah zote yanaungwa mkono na kufadhiliwa na Iran.

Iran inasema ‘vitendo vya kihalifu’ vya Israel vitajibiwa

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanaani anasema Iran haitaacha “vitendo” vyovyote vya uhalifu vya Israel bila majibu.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wanahabari wa kila wiki – wa kwanza tangu jenerali mkuu katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran kuuawa katika shambulizi la Israel la siku ya Ijumaa – Kanaani anasema Iran haitafuti vita lakini haiogopi, Reuters inaripoti.

Maoni yake yanalingana na yale ya kiongozi mkuu wa Iran Ali Khamenei, ambaye alisema mwishoni mwa juma kwamba hatua za Israel hazitapita bila “kulipiza kisasi”.

Hezbollah – ambayo Israel inalenga nchini Lebanon – ni moja ya makundi ya wanamgambo katika kanda ya Mashariki ya Kati ambayo inayoungwa mkono na kufadhiliwa na Iran.

Watu 100,000 wakimbia Lebanon kuelekea Syria, UN yasema

XX

Takriban watu 100,000 wamevuka Lebanon na kuingia Syria ili kuepuka mashambulizi ya anga ya hivi karibuni ya Israel, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi Filippo Grandi anasema.

“Wata wanaendelea kuondoka,” anasema, akiongeza kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanatoa msaada katika vivuko vinne vya mpaka.

Hapo jana tuiliripoti kuwa takriban watu 80,000 walikimbilia Syria katika muda wa siku saba zilizopita.

Kati ya hao, 36,000 walikuwa Wasyria na 41,300 walikuwa Walebanon, kulingana na Waziri wa Lebanon Nasser Yassin.

Mashambulizi ya Israel: Tunachokijua kufikia sasa

Athari za mashambulizi

Israel imemuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah katika shambulizi siku ya Ijumaa ambapo Israel ilisema pia iliua watu wengine 20 muhimu katika kundi hilo, kundi linaloungwa mkono na Iran lilithibitisha kifo cha kiongozi huyo siku iliyofuata.

Jenerali mkuu katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, Abbas Nilforoushan, pia aliuawa katika shambulio hilo, vyombo vya habari vya serikali ya Iran vilisema.

Rais wa Marekani Joe Biden alielezea shambulio hilo kama “kipimo cha haki” kwa waathiriwa, lakini kiongozi mkuu wa Iran amesema kifo chake “haitapita bila kisasi” Kiongozi wa Iran, Ali Khamenei, pia aliripotiwa kuhamishwa hadi mahali salama.

Mashambulizi ya kuvuka mpaka kati ya Israel na Hezbollah nchini Lebanon yaliripotiwa mwishoni mwa juma, huku Israel ikisema kuwa iliua vigogo wengine waandamizi kutoka kundi la wanamgambo.

Maafisa wa Lebanon walisema zaidi ya watu 100 waliuawa siku ya Jumapili, na kufanya idadi ya vifo kutoka wiki mbili zilizopita hadi zaidi ya 1,000.

Waziri Mkuu wa Lebanon, Najib Mikati alisema mashambulizi ya anga ya Israel huenda yakawafanya watu wapatao milioni moja kuyahama makazi yao, akieleza kuwa huenda ndio watu wengi zaidi waliokimbia makazi yao katika historia.

Israel pia ililenga kundi jingine linaloungwa mkono na Iran, Houthi, nchini Yemen, ikidai kuwa walikuwa wakijibu mashambulizi ya kundi hilo dhidi yake.

Viongozi watatu wa Palestina wauawa katika shambulio la Israel huko Beirut

Shambulio

Kundi la wanamgambo wa Kipalestina lilisema siku ya Jumatatu kuwa viongozi wake watatu waliuawa katika shambulizi la Israel huko Beirut, likiwa ni shambulio la kwanza ndani ya mipaka ya miji huku Israel ikizidisha uhasama dhidi ya washirika wa Iran katika eneo hilo.

Chama cha Popular Front for the Liberation of Palestine (PFLP) kilisema viongozi hao watatu waliuawa katika shambulio lililolenga wilaya ya Kola ya Beirut.

Shambulio hilo liligonga ghorofa ya juu katika wilaya ya Kola katika mji mkuu wa Lebanon, mashuhuda wa Reuters walisema.

Hakukuwa na maoni ya mara moja kutoka kwa jeshi la Israeli.

Kuongezeka kwa mashambulio ya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon na wanamgambo wa Houthi nchini Yemen kumezusha hofu kwamba mapigano ya Mashariki ya Kati yanaweza kutoka nje ya udhibiti na kuteka Iran na Marekani, mshirika mkuu wa Israel.

PFLP ni kundi jingine la wanamgambo wanaoshiriki katika vita dhidi ya Israel.

Israel siku ya Jumapili ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo wa Houthi nchini Yemen na makumi ya maeneo yanayolengwa na Hezbollah kote nchini Lebanon baada ya awali kumuua kiongozi wa Hezbollah.

SpaceX yatua kituo cha anga za mbali kuwachukua wanaanga waliokwama

Dragon cha SpaceX pichani baada ya kutia nanga kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu

Chombo cha SpaceX kilichotumwa kuwarudisha wanaanga wawili waliokuwa wamekwama kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) kimetia nanga.

Dragon, ambayo ina viti viwili tupu vya Butch Wilmore na Suni Williams, ilitia nanga saa 17:30 saa za mashariki (22:30 BST).

Wawili hao walifika kituoni wakiwa na chombo kipya cha Boeing ya Starliner kwa misheni ya siku nane mwezi Juni, lakini walilazimika kubaki hapo kwa sababu ya hitilafu iliyogunduliwa wakati wa safari. Sasa wanatarajiwa kurejea duniani mwezi Februari.

Chombo hicho cha Dragon kiliinuliwa kutoka Cape Canaveral, Florida siku ya Jumamosi kikiwa na mwanaanga wa Nasa Nick Hague na mwanaanga wa Urusi Alexander Gorbunov.

Hague, ambaye amefanya kazi hapo awali kwenye ISS, na Gorbunov wataungana na wafanyakazi wa kituo cha anga za juu kabla ya kuwarudisha Wilmore na Williams Duniani.

Safari ilikuwa umepangwa kufanyika Alhamisi lakini ilicheleweshwa kwa sababu ya Kimbunga cha Helene, ambacho kimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la kusini-mashariki mwa Marekani, ikiwa ni pamoja na Florida, katika siku za hivi karibuni.

Picha kutoka ndani ya ISS zilionyesha Hague na Gorbunov wakitabasamu na kupiga picha na wafanyakazi wengine baada ya kuwasili.

Huenda mashambulizi ya Israel yamewakosesha makazi watu milioni moja – Waziri Mkuu wa Lebanon

Familia nyingi kutoka kusini mwa Lebanon sasa zinaishi katika mitaa ya Beirut baada ya kukimbia mashambulizi ya anga ya Israeli

Mashambulizi ya anga yanayoendelea Israel huenda tayari yamewalazimu takribani watu milioni moja kukimbia makwao kote Lebanon, waziri mkuu wa nchi hiyo amesema.

“Ni harakati kubwa zaidi ya watu kuhama ambayo inaweza kuwa ilitokea,” Najib Mikati alisema.

Wizara ya afya ya Lebanon iliripoti zaidi ya watu 50 waliuawa katika shambulio Jumapili, siku mbili baada ya Israel kumuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah huko Beirut.

Wakati huo huo, Hezbollah ilirusha makombora zaidi kaskazini mwa Israel.

Katika hatua nyingine, Israel ilisema imefanya mashambulizi ya anga “makubwa” katika maeneo ya kijeshi ya vuguvugu la Houthi linaloungwa mkono na Iran nchini Yemen.

Hezbollah ilithibitisha Jumapili kwamba kamanda mkuu wa kijeshi Ali Karaki na kasisi mkuu, Sheikh Nabil Qaouk, pia waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel.

“Tunahitaji kuendelea kuipiga Hezbollah vikali,” mkuu wa jeshi la Israel Herzi Halevi alisema.

Shambulizi jingine la Israel katika kitongoji cha kati cha Beirut cha Kola mapema Jumatatu liliua wanachama watatu wa chama cha Popular Front for the Liberation of Palestine (PFLP), kundi hilo lilisema katika taarifa yake.

PFLP ni mwanachama wa Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina, muungano unaotambuliwa katika Umoja wa Mataifa kama mwakilishi rasmi wa Wapalestina.

Kundi hilo pia linachukuliwa kuwa shirika la kigaidi na Marekani na EU. Taarifa hiyo iliwataja waliouawa kuwa ni mkuu wa usalama wa kijeshi Mohammad Abdel-Aal, kamanda wa kijeshi Imad Odeh, na mpiganaji Abdel Rahman Abdel-Aal.

Israel yazidisha mashambulizi katika maeneo ya Hezbollah huko Bekaa

Moto

Jeshi la Israel liliendelea, siku ya Jumatatu, kufanya mashambulizi mapya kadhaa kwenye “maeneo ya Hezbollah” nchini Lebanon, siku chache baada ya kuuawa kwa Hassan Nasrallah.

Hezbollah ilitoa maoni yake juu ya kile ilichokiita “habari zinazosambazwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuhusu hatua za shirika ndani ya uongozi wa Hezbollah baada ya kifo cha kishahidi cha Nasrallah,” ikisema kwamba “sio muhimu na hauwezi kutegemewa isipokuwa tamko rasmi litatolewa kuhusu uongozi wa Hezbollah.”

Saa chache baada ya saa sita usiku, jeshi la Israeli lilisema kuwa ndege yake ilishambulia maeneo kadhaa ya Hezbollah katika Bonde la Bekaa la Lebanon.

Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni “vipande vya kurushia roketi na majengo ambapo Hezbollah ilihifadhi silaha,” gazeti la Times of Israel liliripoti, likinukuu jeshi.

Limeongeza kuwa jeshi la Israel lilishambulia kwa mabomu maeneo mengine kusini mwa Lebanon “yanayotumiwa na Hezbollah kutekeleza operesheni za kigaidi” dhidi ya Israel.

Katika saa za mwisho za Jumapili, msemaji wa jeshi la Israel alisema kupitia Telegram kwamba ndege za jeshi la anga “zilishambulia makumi ya shabaha za magaidi nchini Lebanon, ikiwa ni pamoja na majukwaa ya kurusha makombora yaliyoelekezwa katika eneo la Israel na maghala ya kuhifadhi silaha.”

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment