Jeshi la Israel liliendelea, siku ya Jumatatu, kufanya mashambulizi mapya kadhaa kwenye “maeneo ya Hezbollah” nchini Lebanon, siku chache baada ya kuuawa kwa Hassan Nasrallah.
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa
Mashambulizi ya Israel: Tunachokijua kufikia sasa

Israel imemuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah katika shambulizi siku ya Ijumaa ambapo Israel ilisema pia iliua watu wengine 20 muhimu katika kundi hilo, kundi linaloungwa mkono na Iran lilithibitisha kifo cha kiongozi huyo siku iliyofuata.
Jenerali mkuu katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, Abbas Nilforoushan, pia aliuawa katika shambulio hilo, vyombo vya habari vya serikali ya Iran vilisema.
Rais wa Marekani Joe Biden alielezea shambulio hilo kama “kipimo cha haki” kwa waathiriwa, lakini kiongozi mkuu wa Iran amesema kifo chake “haitapita bila kisasi” Kiongozi wa Iran, Ali Khamenei, pia aliripotiwa kuhamishwa hadi mahali salama.
Mashambulizi ya kuvuka mpaka kati ya Israel na Hezbollah nchini Lebanon yaliripotiwa mwishoni mwa juma, huku Israel ikisema kuwa iliua vigogo wengine waandamizi kutoka kundi la wanamgambo.
Maafisa wa Lebanon walisema zaidi ya watu 100 waliuawa siku ya Jumapili, na kufanya idadi ya vifo kutoka wiki mbili zilizopita hadi zaidi ya 1,000.
Waziri Mkuu wa Lebanon, Najib Mikati alisema mashambulizi ya anga ya Israel huenda yakawafanya watu wapatao milioni moja kuyahama makazi yao, akieleza kuwa huenda ndio watu wengi zaidi waliokimbia makazi yao katika historia.
Israel pia ililenga kundi jingine linaloungwa mkono na Iran, Houthi, nchini Yemen, ikidai kuwa walikuwa wakijibu mashambulizi ya kundi hilo dhidi yake.
Viongozi watatu wa Palestina wauawa katika shambulio la Israel huko Beirut

Kundi la wanamgambo wa Kipalestina lilisema siku ya Jumatatu kuwa viongozi wake watatu waliuawa katika shambulizi la Israel huko Beirut, likiwa ni shambulio la kwanza ndani ya mipaka ya miji huku Israel ikizidisha uhasama dhidi ya washirika wa Iran katika eneo hilo.
Chama cha Popular Front for the Liberation of Palestine (PFLP) kilisema viongozi hao watatu waliuawa katika shambulio lililolenga wilaya ya Kola ya Beirut.
Shambulio hilo liligonga ghorofa ya juu katika wilaya ya Kola katika mji mkuu wa Lebanon, mashuhuda wa Reuters walisema.
Hakukuwa na maoni ya mara moja kutoka kwa jeshi la Israeli.
Kuongezeka kwa mashambulio ya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon na wanamgambo wa Houthi nchini Yemen kumezusha hofu kwamba mapigano ya Mashariki ya Kati yanaweza kutoka nje ya udhibiti na kuteka Iran na Marekani, mshirika mkuu wa Israel.
PFLP ni kundi jingine la wanamgambo wanaoshiriki katika vita dhidi ya Israel.
Israel siku ya Jumapili ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo wa Houthi nchini Yemen na makumi ya maeneo yanayolengwa na Hezbollah kote nchini Lebanon baada ya awali kumuua kiongozi wa Hezbollah.
SpaceX yatua kituo cha anga za mbali kuwachukua wanaanga waliokwama

Chombo cha SpaceX kilichotumwa kuwarudisha wanaanga wawili waliokuwa wamekwama kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) kimetia nanga.
Dragon, ambayo ina viti viwili tupu vya Butch Wilmore na Suni Williams, ilitia nanga saa 17:30 saa za mashariki (22:30 BST).
Wawili hao walifika kituoni wakiwa na chombo kipya cha Boeing ya Starliner kwa misheni ya siku nane mwezi Juni, lakini walilazimika kubaki hapo kwa sababu ya hitilafu iliyogunduliwa wakati wa safari. Sasa wanatarajiwa kurejea duniani mwezi Februari.
Chombo hicho cha Dragon kiliinuliwa kutoka Cape Canaveral, Florida siku ya Jumamosi kikiwa na mwanaanga wa Nasa Nick Hague na mwanaanga wa Urusi Alexander Gorbunov.
Hague, ambaye amefanya kazi hapo awali kwenye ISS, na Gorbunov wataungana na wafanyakazi wa kituo cha anga za juu kabla ya kuwarudisha Wilmore na Williams Duniani.
Safari ilikuwa umepangwa kufanyika Alhamisi lakini ilicheleweshwa kwa sababu ya Kimbunga cha Helene, ambacho kimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la kusini-mashariki mwa Marekani, ikiwa ni pamoja na Florida, katika siku za hivi karibuni.
Picha kutoka ndani ya ISS zilionyesha Hague na Gorbunov wakitabasamu na kupiga picha na wafanyakazi wengine baada ya kuwasili.
Huenda mashambulizi ya Israel yamewakosesha makazi watu milioni moja – Waziri Mkuu wa Lebanon

Mashambulizi ya anga yanayoendelea Israel huenda tayari yamewalazimu takribani watu milioni moja kukimbia makwao kote Lebanon, waziri mkuu wa nchi hiyo amesema.
“Ni harakati kubwa zaidi ya watu kuhama ambayo inaweza kuwa ilitokea,” Najib Mikati alisema.
Wizara ya afya ya Lebanon iliripoti zaidi ya watu 50 waliuawa katika shambulio Jumapili, siku mbili baada ya Israel kumuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah huko Beirut.
Wakati huo huo, Hezbollah ilirusha makombora zaidi kaskazini mwa Israel.
Katika hatua nyingine, Israel ilisema imefanya mashambulizi ya anga “makubwa” katika maeneo ya kijeshi ya vuguvugu la Houthi linaloungwa mkono na Iran nchini Yemen.
Hezbollah ilithibitisha Jumapili kwamba kamanda mkuu wa kijeshi Ali Karaki na kasisi mkuu, Sheikh Nabil Qaouk, pia waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel.
“Tunahitaji kuendelea kuipiga Hezbollah vikali,” mkuu wa jeshi la Israel Herzi Halevi alisema.
Shambulizi jingine la Israel katika kitongoji cha kati cha Beirut cha Kola mapema Jumatatu liliua wanachama watatu wa chama cha Popular Front for the Liberation of Palestine (PFLP), kundi hilo lilisema katika taarifa yake.
PFLP ni mwanachama wa Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina, muungano unaotambuliwa katika Umoja wa Mataifa kama mwakilishi rasmi wa Wapalestina.
Kundi hilo pia linachukuliwa kuwa shirika la kigaidi na Marekani na EU. Taarifa hiyo iliwataja waliouawa kuwa ni mkuu wa usalama wa kijeshi Mohammad Abdel-Aal, kamanda wa kijeshi Imad Odeh, na mpiganaji Abdel Rahman Abdel-Aal.
Israel yazidisha mashambulizi katika maeneo ya Hezbollah huko Bekaa

Jeshi la Israel liliendelea, siku ya Jumatatu, kufanya mashambulizi mapya kadhaa kwenye “maeneo ya Hezbollah” nchini Lebanon, siku chache baada ya kuuawa kwa Hassan Nasrallah.
Hezbollah ilitoa maoni yake juu ya kile ilichokiita “habari zinazosambazwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuhusu hatua za shirika ndani ya uongozi wa Hezbollah baada ya kifo cha kishahidi cha Nasrallah,” ikisema kwamba “sio muhimu na hauwezi kutegemewa isipokuwa tamko rasmi litatolewa kuhusu uongozi wa Hezbollah.”
Saa chache baada ya saa sita usiku, jeshi la Israeli lilisema kuwa ndege yake ilishambulia maeneo kadhaa ya Hezbollah katika Bonde la Bekaa la Lebanon.
Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni “vipande vya kurushia roketi na majengo ambapo Hezbollah ilihifadhi silaha,” gazeti la Times of Israel liliripoti, likinukuu jeshi.
Limeongeza kuwa jeshi la Israel lilishambulia kwa mabomu maeneo mengine kusini mwa Lebanon “yanayotumiwa na Hezbollah kutekeleza operesheni za kigaidi” dhidi ya Israel.
Katika saa za mwisho za Jumapili, msemaji wa jeshi la Israel alisema kupitia Telegram kwamba ndege za jeshi la anga “zilishambulia makumi ya shabaha za magaidi nchini Lebanon, ikiwa ni pamoja na majukwaa ya kurusha makombora yaliyoelekezwa katika eneo la Israel na maghala ya kuhifadhi silaha.”
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.