Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Kwa Mbrazili Daniel Guerra aliyetamani kuwa baharia ili kusafiri ulimwenguni, tangazo la kazi lilikuwa ni kutimia kwa ndoto yake.
Mmiliki wa boti la kifahari wa Uingereza alikuwa akitafuta watu wawili wa kumsaidia kusafiri kutoka Brazili kupitia Bahari ya Atlantiki, mojawapo ya safari kuu za baharini.
Hakutakuwa na mshahara, lakini gharama zote zililipwa – na, muhimu zaidi, Bw Guerra angepata uzoefu wa baharini aliouhitaji ili afuzu kama nahodha wa baharini.
“Ndoto yangu ilikuwa kuwa nahodha na kwenda kufanya kazi Ulaya,” anakumbuka kijana huyo mwenye umri wa miaka 43, ambaye aliona tangazo hilo kutoka kwa wakala wa ajira za mabaharia mtandaoni.
“Kwa hivyo nilifurahi sana, nikijua ndoto yangu ilikuwa inaanza.”
Mambo yalionekana kuwa mazuri zaidi wakati Bw Guerra na muajiriwa mwenzake, Rodrigo Dantas, 32, walipokutana na mwajiri wao mpya Muingereza.
Walikuwa na hofu kwamba anaweza kuwa mmiliki mwenye majivuno au mwenye maringo, ambaye angehakikisha kuwa wanajua yeye ndiye bosi.
Lakini haikuwa hivyo, George Saul alikuwa mtu mwenye tabasamu, alionekana kuwa rafiki , ambaye hakuweka masharti ya kufuata utaratibu. Mabaharia, alisema, wanaweza hata kumuita kwa jina lake la utani – “Fox”.
“Nilikuwa nikifanya kazi kwenye baadhi ya boti nyingine na wamiliki wazee, wakorofi sana na walinidharau,” anaongeza Bw Dantas. Lakini yeye “alikuwa mzuri, na rafiki sana.”
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.