Rwanda: Serikali yatoa muongozo mpya kupambana na msambao wa virusi vya Marburg

Wizara ya Afya nchini Rwanda, imetoa mwongozo mpya unaolenga kuzuia kuenea kwa virusi vya Marburg nchini Rwanda, wakati huu idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huu ikiongezeka kufikia 8.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Dalili kuu za homa hii ni pamoja na maumivu makali ya kichwa, misuli, kutapika, na kuhara, raia wakitakiwa kifika kwenye vituo vya afya pindi wakionesha dalili hizi.
Dalili kuu za homa hii ni pamoja na maumivu makali ya kichwa, misuli, kutapika, na kuhara, raia wakitakiwa kifika kwenye vituo vya afya pindi wakionesha dalili hizi. © CDC/ Dr. Frederick Murphy

Katika taarifa ya wizara ya afya iliyotolewa jana jioni, watu 26 wameripotiwa kuambukizwa virusi hivi tangu Septemba 27 wakati mlipuko wa kwanza kabisa wa Marburg ulipothibitishwa nchini humo.

Waziri wa Afya Sabin Nsanzimana amesema wanawafuatilia zaidi ya watu 300 ambao wanadaiwa kuwa waligusana na wagonjwa waliofariki na wale waliothibitishwa kuambukizwa.

Baadhi ya miongozi iliyotolewa ni pamoja na kusimamishwa kwa muda kuwatembelea wagonjwa hospitalini, kudumisha usafi binafsi na kuepuka kugusana na watu wanaoonyesha dalili za virusi vya Marburg, hata hovyo shughuli za biashara zitaendelea kama kawaida.

Aidha shughuli za mazishi na maombolezo ya nyumbani pia zimepigwa marufuku wafiwa wakitakiwa kuepuka msongamano inayoweza kuongeza hatari ya kueneza virusi hivyo, ambapo pia ufunuaji wa jeneza hautaruhisiwa katika nyumba, makanisa na misikiti.

Dalili kuu za homa hii ni pamoja na maumivu makali ya kichwa, misuli, kutapika, na kuhara, raia wakitakiwa kifika kwenye vituo vya afya pindi wakionesha dalili hizi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment