Agano linavyosaidia kujibiwa kwa maombi.

Kila mtu anayemuomba Mungu anategemea na anapenda kujibiwa maombi yake. Na kuna njia nyingi zinazoweza kumfanya mtu ajibiwe na kupokea. Mfano tunategemea anayemuomba Mungu ampe mtoto atachukua hatua ya kuoa na kuzaa mtoto, hii ikiwa ni kanuni ya kawaida kabisa, maana Mungu kaweka kanuni ya uzazi kati ya mume na mke wakutane na wazae.

Pia mtu aweza jibiwa na Mungu kwa Mungu kuamua kufanya jambo ili ajitukuze, hii ni kesi ya watu wachache wanaopata neema ya kujibiwa, rejea mfano wa wajane, WALIKUWEPO WAJANE WENGI SAREPTA ILA ALIYEPOKEA NI MMOJA, WALIKUWEPO WENYE UKOMA WENGI WALIOTAKASWA WACHACHE.

Kuna kanuni ya tatu nataka niiongelee hapa.
Nimesikia watu wengi wakitumia maneno kujiunganisha na madhabahu, wengine wakiomba kwa kuita Mungu wa Wachungaji wao, Baba zao wa kiroho, Nabii wao, Mtume nk. UNAWEZA KUWALAUMU UKIHISI WANAMTUKUZA MTU BADALA YA MUNGU ILA UKWELI NI KWAMBA WANAJIUNGANISHA NA AGANO AMBALO MUNGU KAINGIA NA HIZO OFISI KWA AJILI YA KUWAPATIA MAJIBU YAO. (Mtihani unakuwa je! Una uhakika kama huyo ana AGANO kweli na Mungu?).

Tumwangalie Daniel kidogo
Daniel 6:10

Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa KUKABILI YERUSALEMU;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.

Huyu nabii alijua siri hii, kuwa kanuni ya kwanza isingefanikiwa kupokea majibu, maana ili wafanikiwe kurudi nyumbani ilibidi achukue hatua ya kuunda jeshi kitu ambacho kilikuwa kigumu, Pia hakutaka kusubiri kukutana ana KWA ana na Mungu, AKATUMIA KANUNI YA TATU YA KUJIUNGANISHA NA MJI WA YERUSALEMU AKIKUMBUKA MAOMBI YA MFALME SULEMANI ALIPOOMBA SIKU YA KUDEDICATE HEKALU. Angalia maombi haya kisha uelewe nini Daniel alikuwa anakifanya.
1 Wafalme 8:33-34

Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea tena kwako, na kulikiri jina lako wakikuomba na kukusihi katika nyumba hii;

basi, usikie huko mbinguni, ukawaachilie watu wako Israeli dhambi yao, ukawarejeze tena katika nchi uliyowapa baba zao.

Daniel alifungua madirisha kuelekea Yerusalemu kujiunganisha na maombi ya kiagano ambayo Sulemani aliomba ILI KUMFANYA MUNGU ATENDE KWA KULIKUMBUKA AGANO LA SIKU WANAWEKA WAKFU HEKALU.

Ni vizuri sana kuelewa siri hii maana imetumika sana kibiblia mambo yalipokwama, Elisha aliyapiga maji akamuita Mungu wa Eliya, Sulemani alijiunganisha na AGANO la Daudi baba yake nk. IPO mifano mingi sana kuelewa siri hii ya maombi. SASA WEWE DHARAU WATU WENYE AGANO NA MUNGU UKITEGEMEA KUJIBIWA, HUKU HUJUI KWAMBA WANASEHEMU YA MAJIBU YAKO AMBAYO MUNGU HUYAPITISHIA KWAO. Barikiwa sana



CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com, cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!

Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.




Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment